Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,894
- 31,103
MBUNGE wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela ametoa tahadhari juu ya uwezekano wa kutokea umwagaji damu katika uchaguzi mkuu wa 2010 iwapo mbegu za chuki za ukabila na udini alizosema zinapandwa sasa, hazitadhibitiwa mapema.
Kilango, mmoja wa wabunge wenye hoja nzito wakati wa kujadili masuala mbalimbali bungeni, pia alisema viongozi hawana budi kuwa makini katika kutoa kauli zao wakati wa kujadili mambo muhimu kwa taifa, ingawa hakutaja ni kauli na masuala gani.
Mbunge huyo wa Same, ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, alisema umwagaji damu uliotokea Zanzibar wiki iliyopita ni cheche tu na kwamba kama hali hiyo haitadhibitiwa haraka cheche zinaweza kuzaa moto.
Vurugu hizo zilitokea wiki iliyopita kisiwani Zanzibar wakati wafuasi wa CCM na CUF waliposhambuliana kwa silaha za jadi, yakiwemo mapanga na visu wakati wa zoezi linaloendelea la kuandikisha wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Magogoni.
Hali ya Zanzibar inabidi tuikemee wote na kwa nguvu zote. Hivi kama leo wakati wa kujiandikisha tu, tunakatana mapanga... ikifika kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 itakuwaje, alihoji Kilango wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana.
Mbunge huyo alikemea ubaguzi kwa misingi ya kabila ambayo alisema inaanza kujitokeza sasa na kutaka iwe marufuku kwa mtu yeyote kumuita Mtanzania mwenzake kuwa ni wa kuja pale anapojitokeza kugombea nafasi ya uongozi eneo ambalo hakuzaliwa.
Kuhusu kauli za kushambuliana ambazo zinatolewa wakati wa kujadili masuala muhimu ya kitaifa, Kilango alisema matamshi mengine yanachochea kuvuruga amani iliyopo.
Bila kumtaja kiongozi yeyote, Kilango alisema anakubaliana na watu wenye misimamo thabiti kwenye mambo muhimu ya kujenga nchi, lakini akashauri watumie ndimi zao vizuri ili matamshi yao yalenge kuimarisha amani.
Kukosoana ni lazima... tukosoane ili tujenge lakini swali linakuja tunakosoleana wapi, alihoji Kilango.
Suala la azma ya serikali kununua mitambo ya Kampuni ya Dowans Tanzania Limited liliibua mjadala mkubwa baada ya kamati mbili za bunge kutofautiana, moja ikitaka jenereta hizo za kuzalisha umeme wa dharura isinunuliwe kwa sababu ni kukiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma na huku kiongozi wa kamati nyingine akishauri inunuliwe ili kulinusuru taifa na uwezekano wa kuingia gizani.
Tofauti hizo zilisababisha wabunge kurushiana maneno makali, ikiwemo kauli ya kumuelezea mmoja wa wabunge kuwa anajifunza siasa bungeni na kwenye kamati za bunge, kuhusisha mpango huo na ufisadi, kuhusisha msimamo na Operesheni Sangara ya Chadema na madai kuwa wanaounga mkono suala hilo walilipwa "posho posho kubwa".
Kilango alitahadharisha kuwa amani iliyopo leo ikitoweka itachukua miaka mingi kuirejesha na kutoa mfano wa nchi ya Rwanda ambayo tangu mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, bado hawajaweza kuijenga nchi hiyo.
Kilango alisema kuwa Tanzania imekuwa ikisifiwa ulimwenguni kutokana na kuwa na amani na kiongozi mzuri wa nchi, lakini zinazoanza kujitokeza sasa nchini hasa Zanzibar, Tanzania inataka kujiondoa kwenye nafasi hiyo.
Source:Mwananchi