Elections 2010 Mama kikwete aingia kimya kimya kigoma na kuondoka

Salas

JF-Expert Member
Feb 15, 2009
382
82
Mpiga debe ambaye pia ni mke wa rais wa Tanzania ameingia katika simanzi ya aina yake pale idadi ya watu waliohudhuria kampeni alizokuwa akiziendesha katika ukumbi wa kibo kuzidiwa na wale walihudhuria kwenye promotion ya balimi ambazo zilifanyika katika ukumbi wa website ambao uko karibu na ukumbi huo.
Mama huyo akiwa anapaza sauti za chagua CCM mara kwa mara (huenda alisahau kwamba mumewe kauthibitishia umma wa watanzania kwamba urais ni swala la kifamilia) bora hata angekuwa anasema mchague familia yetu.

Wachilia mbali hayo yaliyo jiri, nilijaribu kujisogeza kwenye baa za karibu ili niweze kung'amua watu wanajua ni nini kinachoendelea la hasha wanasema tumeona magari ya serikali yanapita na mgombea ubunge wa ccm tu nadhani ni kampeni ya kawaida hapo kwenye ukumbi na watu sio wengi, nilielezwa na muhudumu mmoja wa faith bar.

Ninaogopa fikra zangu ila ninaamini hizi gharama zinazotumika katika hii familia kutafuta urais wa kifamilia bora zingehifadhiwa kwa ajili ya kuandaa kustaafu kwa mheshimiwa huyu na familia yake.

Nachelea kusema ndio huyu mrithi wa nyerere au ni mtarajie mwingine go slaa go slaa neema ya Mungu iwe juu yako na ulinzi wa malaika wa bwana wanao ilinda bustani ya edeni wa kuzingira tuko mbele yako kwa maisha yetu, hata nikipigwa bomu mimi ni mmoja ila maelfu wanao kufa kila siku kwa magonjwa ya kuzuilika, mamia wanaopata ukimwi kila siku kwa sababu ya kukata tamaa kwa ajili ya ugumu wa maisha wataishi.

Nyerere alitembea kwa baiskeli na punda hakuwa mwenyewe, sisi tuko nawe hata ukamilifu wa dahari.

Mungu tudumishie amani yetu, na upendo wetu pasipo kujali udini wala ukabila sisi ni ndugu na afrika ni moja.

Mwaka huu nitasafiri kwa gharama isiyo pungua laki 2 kwenda kupiga kura ya mbunge na rais na ninamjua rais wangu na mbunge wangu.
 
Vipi Mkuu, wewe hukukaribishwa kwenye kampeni za Shuka kwa Shuka?

Hii ukikaribishwa na kimwana wa CCM, au mtoto wa Fisadi, mambo yanaweza kuwa mazuri.

Unafaidi na tarehe 31/10/2010 unapeleka chama cha Kimwana na Rais wao kuwa Chama cha Upinzani.......
 
Sasa naanza kuamini kwanini Msekwa, Mkapa na Mzee Mwinyi wamekimbia Kikwete amefanya swala la kuingia Ikulu ni lake na familia yake ndio maana wakubwa wenzake wamwemwachia kampeni za urais, watanzania muda wa mabadiliko ni sasa fanyeni maamuzi.
 
Sasa naanza kuamini kwanini Msekwa, Mkapa na Mzee Mwinyi wamekimbia Kikwete amefanya swala la kuingia Ikulu ni lake na familia yake ndio maana wakubwa wenzake wamwemwachia kampeni za urais, watanzania muda wa mabadiliko ni sasa fanyeni maamuzi.

Mmesahau usemi wa Makamba kuwa Kikwete ni mtaji kwa CCM, kwa sababu ya kura za REDET zilizosema wakati fulani kuwa Kikwete ni maarfu kuliko CCM. Naona wazee wa chama wameamua kumuachia ionekane kama dhana hii ni kweli au la....
 
Mwaka huu nitasafiri kwa gharama isiyo pungua laki 2 kwenda kupiga kura ya mbunge na rais na ninamjua rais wangu na mbunge wangu.

Hivi haya ndiyo kauli ya kiutu uzima. Kwenye hili tupo wote mia kwa mia.
 
duu ngoma nzito kweli sijui atarudi kwenye ualimu huyu mtu!??
 
Hivi haya ndiyo kauli ya kiutu uzima. Kwenye hili tupo wote mia kwa mia.

Wandugu nami niko pamoja na nyie nitasafiri kutoka Kigoma kwenda Shy kupiga kura yangu ya uhakika kwa Rais anayeelewa! Ulishaona wapi urais unapiganiwa na familia??? Wa-TZ tuamke tuiangushe hii familia inayolilia Ikulu!! PALE KUNA NINI MBONA WANAHANGAIKA HIVI??
 
Kweli inashangaza, sijamwona Mzee Mwinyi, na si kawaida yake...kweli hapa kuna jambo, naona ya Kubenea ni ya kweli kabisaa!
 
Back
Top Bottom