Mama Kijijini kaniambia haya. Sikuyajua mwanzo

DAVID PALMER

JF-Expert Member
Jan 19, 2020
285
1,447
Nimekuja kijijini kwetu huku kwa mapumziko mafupi. Katika kuongea na watu leo nimekaa na maza mmoja. Katika story story akaniambia mambo haya ambayo yamenishangaza.

1. Kama mtu ana mimba. Basi hatakiwi kuhudumiwa na mama yake mzazi, ikiwa mama yake huyo ameolewa na kuzaa zaidi ya ndoa mbili. Yaan kama aliolewa na baba huyu ndo akakuzaa wewe, akaachika akaolewa tena, akaachika tena akiolewa tena basi hatakiwi kumuuguza bintie alie mjamzito. Sababu kunakua na possibility kubwa mtoto kuzaliwa na hitilafu, au mtoto na mama kufa. So vifo vingi vya watoto leba hutokea kwa sababu hii. By chance kunae watoto husavaivu pia.

2. Majority hudhani vyakula vya siku hizi na lifestyle ndo hupelekea wajawazito wengi hufanyiwa operation. Sawa huwa ni sababu, lakini sio sababu kuu. Sababu kuu ni baba mwenye mimba kulala na wanawake wa nje na kuja kulala na mkewe mjamzito. Hii huwa sababu kubwa kwann hujifungua kwa kisu, au watoto kuzaliwa na tabia mbovu, na upeo na ufahamu wa mtoto kuwa mdogo.

3. Maisha ya wengi yameathiriwa kwa sababu ya kushuhudia au kusikia vitu wasivopaswa kusikia kutoka kwa wazazi wao. Ikitokea wazazi wanatukanana matusi ya nguoni, ile mtoto kusikia basi kunae namna maisha ya mtoto yanaathirika. (Laana). Au labda mtoto kaona tupu ya mzazi, au kaona wakiwa wana-sex. Utakuta kazi hapati, haoi, ulevi, nuksi nk.

4. Haya mambo yote juu sio ya kudumu. Kunae namna ya kukata link hiyo isidhuru watoto. Kienyeji kuna dawa na kidini pia.
 
Sijawahi sikia baba na mama wanatukanana sembuse kupigana wala kubishana

Lao ni moja always...!

Kuna siku nljifanya nabishana na mama nkashangaa mzee ananiita ananiuliza ushawahi ona namfokea mama yako



Mkulima wa mahindi
 
Back
Top Bottom