Mama Karume hakuchelewa kutuma ujumbe wake kwa 'aina ya waliokuwepo' Diamond Jubilee

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,193
25,504
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Yanga Mama Karume amewataka wanasiasa kutojibanza kwenye mpira kwa ajili ya maslahi yao binafsi. Amewakemea na kuwataka kutoutumia mpira kama ngazi zao za kusaka ngazi mbalimbali za uongozi.

Mama Karume, akiwa ni nembo nyingine ya Wazanzibari ya kutoacha kuusema ukweli popote walipo, hakutoa ujumbe huo kwa bahati mbaya. Katika meza yake alipokuwapo Mgeni Rasmi na hata Mgeni Maalum, Mama Karume alijionea 'mtu' akiwa amevaa fulana ikiandikwa mgongoni 'MAKONDA'.

Mama Karume hakuchelewesha. Alipopata tu nafasi akatuma ujumbe wake mkavu na wa moja kwa moja. Kumbe kuna watu walijiandaa kutafuta umaarufu wa kisiasa kwenye Shughuli ile ya Yanga. Ujumbe wa Mama Karume ukawafikia wahusika palepale.

Ninamuweka Mama Karume kwenye kundi la akina Mzee Moyo, Juma Duni Haji na Maalim Seif kama alama za Wasemakweli Wazanzibari.
 
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Yanga Mama Karume amewataka wanasiasa kutojipanza kwenye Moira kwa ajili ya maslahi yao binafsi. Amewakemea na kuwataka kutoutumia mpira kama ngazi zao za kusaka ngazi mbalimbali za uongozi.

Mama Karume, akiwa ni nembo nyingine ya Wazanzibari ya kutoacha kuusema ukweli popote walipo, hakutoa ujumbe huo kwa bahari mbaya. Katika meza yake alipokuwapo Mgeni Rasmi na hata Mgeni Maalum, Mama Karume alijionea 'mtu' akiwa amevaa fulana ikiandikwa mgongoni 'MAKONDA'.

Mama Karume hakuchelewesha. Alipopata tu nafasi akatuma ujumbe wake mkavu na wa moja kwa moja. Kumbe kuna watu walijiandaa kutafuta umaarufu wa kisiasa kwenye Shughuli ile ya Yanga. Ujumbe wa Mama Karume ukawafikia wahusika palepale.

Ninemuweka Mama Karume kwenye kundi la akina Mzee Moyo, Juma Duni Haji na Maalim Seif kama alama za Wasemakweli Wazanzibari.
Yanga kweli mnapewa Uwanja na mwanasimba mnakubali? JK aliwapa Simba mchango kama Rais tena aliwapea Ikulu
 
Hilo ni kombora la uso ingawa Bashite hawezi kuelewa ni kama mtu zoba.
Naona siku hizi Bashite kila aingiapo anatwangwa ujumbe. Ilianza kwa msiba wa Ruge, ikaja kwa Mengi nako akatwangwa live na sasa mama Karume naye kampa.
Kweli laana ikikuangukia hata aibu haikuachi salama
 
Juzi pia niliona jezi za Taifa Stars zina jina la Mtu. Kweli nimejiunga kuombea timu hii ishindwe tena asubuhi kweupe.

Its rubbishness, so to say.
 
Sasa nyinyi mnashabikia huku mtandaoni mnajikuta mnajuaaaa..puzii kabisa

Ukipata fursa unaitumia popote pale, huyo mama achongee tuu habadili lolotee..

Yanga fanyeni kazi acheni kuombaomba na kupiga vijembe sababu hamtabadili chochote kama nyny hamtobadilika na mawazo yenu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom