Mama JK karibu sana sokoni Tandale. Maharagwe kg 1 sh 2000! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama JK karibu sana sokoni Tandale. Maharagwe kg 1 sh 2000!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jumakidogo, Dec 12, 2011.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Dec 12, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Karibu sana mama, hapa ni TZ pia. Katikati ya jiji la Dar! Panaitwa Tandale sokoni, halafu ficha hiyo blackberry yako. Eneo hili watu hawachati katika facebook itakwenda na maji. Watu wengi wanakuja huku kwa sababu bidhaa zetu tunauza kwa bei nafuu sana, yaani bei ya kutupa. Maharagwe mbeya sh 2000 kwa kg haya ya Iringa sh1800. Mchele supa huu kilo ni sh 2100 kutoka Mbeya mama, huu wa Shinyanga kilo ni sh 1850. Kifuko cha njegere hizo, zimo mia humo utapata kwa buku. Aha kitunguu swaumu kimoja ni sh 300 ......mbona unaondoka tena mama? Bado naendelea kutaja bei!
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Subutu!! Ulishawahi wapi kugongana naye huko sokoni hata siku moja kama akina mama wengine kama si matani zako tu? Sana sana pale utasikia:

  1. Kama ni maji ya kunywa basi ni yale kutoka kwenye kisima chochote jangwani (Oasis).
  2. Maziwa na Juisi made in Saudia
  3. Maharage produce of Israel
  4. Mtandio toka kiwanda cha Iran
  5. Tende toka Tunisia,
  6. Sukari ya Malawi
  7. Samaki toka Visiwa vya Comoro
  8. Dagaa za kwa Mzee Gwebuza
  9. Dhahabu za Angola na Zambia ...

  ... wenzetu fedha zao hazitumiki hapa kwenye hizi soko zetu za Ki-Matumbi hivo ugumu wa bei hapa nyumbani kwao wao ni simulizi tu
   
 3. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #3
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Lowasa akiwa Rais ndio atashusha hizo bei?
   
 4. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #4
  Dec 13, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Haswaa, umeuliza jibu.
   
Loading...