Mama huyu ufukweni Ocean Road ana kazi gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama huyu ufukweni Ocean Road ana kazi gani?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by buguruni, Aug 5, 2010.

 1. b

  buguruni Member

  #1
  Aug 5, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JAMANI NISAIDIENI. KUNA MAMA MMOJA ANA WATOTO WATANO, KILA SIKU ASUBUHI MAPEMA SANA LAZIMA, NASISITIZA LAZIMA, UTAMKUTA MAENEO YA UFUKWE WA BAHARI YA HINDI ENEO LA OCEAN ROAD NA WATOTO WAKE WOTE. HUWAGA ANAKAAGA MPAKA AROUND SAA TANO THEN HUONDOKA.

  wATOTO WAKE WANA AFYA NJEMA TU NA WANAVAA VIZURI SANA ALWAYS UTAWAKUTA WAMEVAA TRAKI SUTI NZURI.

  WATOTO HAO WENGI NI WA UMRI WA KUWA SHULE MAANA YAKE HAWASOMI SABABU KILA SIKU ASUBUHI WAKO HAPO.

  Kuna ambaye ameshamuona?

  Ana dili gani pale?

  au akili si njema? kama ndio wanatunzwa na kuvalishwa vizuri na nani?

  Kama haujawaju kumuona na njia yako asubuhi ni ocean road, ukipita angalia kwenye ule msingi uliojengwa kuzuia maji ya bahari utamwona
   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Kwa nini wewe unaemwona kila siku usimuulize haya maswali yako?
   
 3. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Mkuu, ikiwa anaonekana mtulivu, ni vyema siku moja ukamuuliza. unaweza kuwa msaada mkubwa, ukamtafuta hata baba/mibaba ya hao watoto.
   
 4. b

  buguruni Member

  #4
  Aug 5, 2010
  Joined: Feb 5, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sijamuuliza nadhani inawezekana kuna aliyeshawahi kuuliza ili anisaidie. My concern ni wale watoto. Acha ulofa safari
   
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Mbona wanitusi yakhe...mimi nimetoa ushauri tu sidhani kama nastahili kuwa lofa kwa hilo...samahani ndugu kama nimekutia hasira...kwaheri bana
   
 6. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wasiliana na Gazeti la Mwananchi watakupa "details zote" za huyo Mama:

  Pale hana kazi: alikuwa Mwalimu wa Shule za Msingi miaka ya 70 katikati, unfortunately MME wake wa ndoa alifariki late 70s na baada ya hapo maisha yakaenda mrama! Hapo alipo anadai "mafao" yake ya ualimu takribani sh 11m lakini alishawahi kulipwa laki 7 tu!

  Kila mtoto aliyenae pale yupo na baba tofauti tofauti: As of late amejifungua mtoto wa 5!
   
 7. JS

  JS JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nimemuona leo ananyonyesha pale asubuhi. Kuna siku Kibonde wa Clouds kwenye kipindi cha JAhazi alisema angemuongelea ila sikupata chance ya kusikiliza tena baaade
   
 8. S

  Simbamwene JF-Expert Member

  #8
  Aug 5, 2010
  Joined: Jun 22, 2008
  Messages: 287
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Buguruni, nakushukuru kwa hadhari uliyonayo juu ya huyu mama na watoto, kuna siku Naibu Waziri, Dr. Lucy Nkya alisimama akaongea nae, nilijua mateso ya yule mama na watoto yameisha? lakini bado wapo palepale, ni vyema yule mama akapelekwa hospitali ya wagonjwa wa akili na watoto wakapelekwa kituo cha malezi Kurasini. Ila ni vyema watu wa Ustawi wa Jamii wakafanya kazi yao, kuhusu huyu mama kwa kweli wamelala. Kama bado anaongeza watoto pale plae pwani huku hana uwezo wa kuwatunza basi ni vyema afungwe kizazi?
   
 9. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,795
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Thanx, baba E for the information. So it seemz nobody cares. Naibu Waziri, Kibonde na wengine wote hakuna ambaye ameishafanya la maana kumhusu. namuunga mkono aliye-suggest afungwe uzazi. shame on the midume inayomzalisha! :rant:
   
 10. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Tatizo sio kufunga kizazi, tatizo ni wale wanaomzalisha au baba watoto watafutwe ili wawajibike kulea.
   
 11. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama ni sahihi kwa vyombo vya dola kuachilia mambo haya yaende kiholela hivi. Kuna mwingine (njemba) yupo pale daraja la kawe (karibia na JKT makao makuu) anaishi palepale na naona makazi yake yanaongezeka kila siku.
   
 12. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nipo tofauti kidogo,, kwasababu mtoas mada kaomba kujua Yule mama anafanyya nini,, hata mimi huwa najiuliza the sama Question lakini sijapata jib Mpaka leo hii.. mimi ninachoomba kwa wale ambao wapo karibu na members walio Selikalini muwazpdoe basi maana mi naona kama hana akili timam vile,, na kuhusu watoto ndo kitu kinaniuma sana maana wanapata shida wasiyo stahili kabisaaaa

  kama inawezekana basi si Jamaa wa ustawi wa jamii wamshughulikie? au wawachukue watoto wakawatunze since ewanahitaji kusoma na kuenjoy na watoto wenzao ili kubadilisha uwezo wa kufikiri..

  Mimi huwa nasema Mtu anapo ingia Majukumuni Selikalini huwa na Displine nzuri sana na anawajibika ile mbaya, lakini kadiri sikuzinapozidi kuisha Majukum speed ya kazi inapungua mpaka inafikia Zero.. naongea hivi kani kukaa kwake pale mimi nailaum Selikali tu!! kwani they know what to do but they dont like to show their Reactions tena kwa makusudi mazima..

  hii inachosha sana ni AFAZALI TUSIWE NA SELIKALI TU, maana hata sioni uwajibikaji wakee:disapointed:
   
 13. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kama Mnyika uko hapa au viongozi wa Chadema ambao nafahamu mnakuwa hapa mara kwa mara basi hebu jaribuni kuliangalia hilo swala. Ila tu labda msilitumie kisiasa na mlifanye tu kama binadamu.

  Michuzi pia ukiweza basi hebu nenda na utupatie habari kamili kwa video ikibidi.

  Nakubaliana na swala la wale watoto waende shule.
   
 14. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Tatizo la nchi hii ndo hili, hakuna anayejua mipaka ya kazi yake haikuwa necessary kwa waziri kuongea naye na kisha ashindwe kutatua tatizo lake. Ina maana waziri hakuelewa tatizo lake na kama alilielewa basi alishindwa kulitatuaau alipuuza.

  Swali linakuja kwa nini alipuuza na au alishindwa? Serikali ipo, wafanyakazi wapo chini ya idara yake, kama suala linahusu wizara nyingine angeweza kuwasiliana na waziri mwenzie kusaidia kumaliza tatizo hilo. Hii issue sio mara ya kwanza kuandikwa na au kuzungumzwa viongozi wetu hawataki kuona na hawataki kusikia.

  Kiti kimoja kuhusu huyu mama ni kuwa kiashiria cha maisha ya watanzania wengi wanavyopuuzwa na viongozi wao.

  Kwa mfano yule mtoto mchanga ana miezi sio zaidi ya mitatu serikali kweli inashindwa kumuweka kwenye makazi ya wenye shida. Je ni watoto wangapi wako kama kale kachanga vijijini na nani anawasemea?????

  Amedhulumiwa: serikali, NGO etc kweli inashindwa kuangalia dhuluma imeanzia wapi, kazini mahakamani nduguze etc. Ni watanzania wangapi wanadhulumiwa makazini, mahakamani na ndugu zao na hawana sauti na hawaonekani?

  Watoto: umri wa wale watoto ni umri wa kwenda shule endapo mikoani kutompeleka mtoto shule ni kosa la jinai kwa nini serikal asiact against her? Ni watoto wangapi wanaotakiwa kwenda shule lakini hawaendi wanafunzi wangapi wanashindwa kujiunga na vyuo kwa vile bodi haitaki nani anawasemea????

  Katiba inasema kila raia anastahili hifadhi ya maisha yake toka kwa jamii. Kwa nini basi serikali inaona haitaki kufanya kazi.
   
 15. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Nyange mimi naona Tatizo ni serikali ambayo ina uwezo na bado imemneglect yeye na watanzania wengine mamilioni.
   
 16. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,045
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160

  Huwa najiuliza kama yule mama anajali hata kuwa kuna ukimwi maana kila kukicha anazaa na mwanaume mwingine (if at all this is true).
  Jamani yale ni maeneo nyeti sana, na sioni sababu kama angeachwa hivi hivi mpaka leo ikiwa serikali haitaki. Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wanapita pale kila siku. Hata kama magari yao ni tinted lakini wanamuona.
  Nashauri muacheni tu, itafika wakati ataondoka. Watoto wana afya, ukipita pale wanakula chipsi mchana, au jioni Azam ice creams, mara pipi.
  Gazeti moja liliandika kuwa anahitaji kama kiasi cha Tshs 1 million arudi kwao Kigoma, labda hajapata bado...............
   
 17. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #17
  Aug 5, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Sasa ana kichanga kipyaaaaaaa.
  Sijui kazaa na nani?
  Halafu sijui hilo tendo walilifanyeje maana yule mama kila aendako huongozana na kundi la wanawe.
   
 18. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #18
  Aug 5, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,045
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwa kuongezea tu alisema ana watoto 3 kwa mumewe wa kwanza ambao ndugu za mumewe wanawatunza ila hajui wapo wapi na anadhani wanaendelea vizuri. Utata wa story yake ktk gazeti ulikuwa hivi:
  1. Anasema amestaafu na anadai mafao yake - je alistaafuje, kwa hiari au umri wa lazima? Mtu anayestaafu ana uwezo wa kuzaa hadi leo kama yeye?
  2. Ana watoto watatu kwa mumewe wa kwanza (achilia mbali watano hao alionao) na Tanzania yetu hii hajui wako wapi wala wanaendeleaje?
  3. Watoto wana afya na yeye anavuta fegi kila saa (may be bangi-sijui) anatoa wapi hela?
  4. Watoto wanakula chips na wana afya njema ila hana baba wala nini, anatoa wapi?
  5. Kasema analala pale pale beach, mbona watoto hawajafa na pneumonia?
  Wale watoto wanapendwa sana na mama yao na ukimwangalia kwa mbali hana matatizo ya akili.
  Ndio pia tatizo la wanahabari wetu na reported speech zao,wakipata taarifa wanaileta kama ilivyo, kwanini hawakufuatilia kama ni kweli alifundisha shule aliyosema, aliondokaje, aliolewa na nani, wapi, nk. Wao wameongea naye wakaibandika kama ilivyo!!!
  Pia alisema mtoto wa mwisho alijizalisha mwenyewe pale pale ufukweni!!!
  Msaidieni kama mnaweza, ila sidhani kama anahitaji msaada.
   
 19. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #19
  Aug 5, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ccm ccm ccm ccm ccm ccm... Ccm
   
 20. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #20
  Aug 5, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wanajamii tuangalie jinsi tunavyoweza kumsaidia huyu mama kama kuna mtu yuko tayari tuwasiliane ili tupange cha kufanya ili tuweze kumrudisha kwenye msitari japo kwa asilimia chache email yangu ni oldmoshi@gmail.com au tunaweza kuwasiliana kupitia mada hii kuona jinsi tunavyoweza kukutana kati kati ya jiji na kufanikisha mengine
   
Loading...