Mama huyu anayeishi jirani na Ikulu asaidiwe na rais | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama huyu anayeishi jirani na Ikulu asaidiwe na rais

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Anold, Sep 2, 2010.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2010
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Katika baadhi ya mabango ya CCM nimeona moja ambalo linaonyesha jinsi rais alivyo mtu wa watu, baadhi ya mabango yanaonyesha rais akiingia katika nyumba za vikongwe pia akikutana na baadhi ya makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu n.k. huenda amewatatulia shida zao kwa kiasi kikubwa ndiyo maana mabango hayo yaewekwa ili watanzania tumfahamu zaidi rais wetu jinsi alivyo karibu na watu hususan wale wenye matatizo.

  Naamini hivyo ndivyo alivyo rais wetu pia ndivyo alivyomgombea wa CCM. Kwa wale ambao wanapita barabara ya ocean road au nyuma ya Hospitali ya ocean road watakubaliana na mimi kuwa kuna mama pamoja na watoto wake watano ambaye anahitaji huruma. Mama huyo hayo yamekuwa makazi yake ya kudumu yeye na watoto wake watano ambapo naamini hata hao watoto amewapatia akiwa eneo hilo hilo. mvua na jua na kila hatari zimemzunguka mama huyu na watoto wake watano. Eneo la ocean road ni eneo ambalo mheshimiwa rais anapita kila siku na ninaimani mama huyu anamuona, shida ambayo mama huyu na watoto wake watano ni kubwa ambayo inastahili huruma. Niliposoma mabango haya ambayo yanaonyesha huruma rais aliyonayo kwa watanzania nikasukumwa kuuliza kwamba huruma hizo kwanini zisimuone mama huyu na watoto wake watano? mama huyu yuko jirani sana na Ikulu ni vipi asisaidiwe?

  Ukiachilia mbali rais, kuna hii taasisi ya mke wa rais iitwacho WAMA ambapo kila kukichwa tunaona misaada mbalimbali inatolewa na waandishi wa habari wamealikwa kushuhudia misaada ikitolewa ni dhambi kwa taasisi kama WAMA ikitoa msaada kwa watu wenye matatizo maalumu kama mama huyu na watoto wake watano? watotohawa ambao mama huyu analala nao nje nani anawalinda dhidi ya vitendo vya ubakaji na udhalilishaji?

  Nakubaliana na ukweli kuwa sio mama huyu tu hapa jijini mwenye matatizo wapo wengi, lakini kwa maisha ambayo mama huyu ambaye nimemzungumzia yanasikitisha sana na anahitaji kusaidiwa. Mama huyu kila nikimuona amekuwa akiniharibia siku yangu kwa uchungu na huruma zinazouzigira moyo wangu. hivyo kwakuwa rais inaonyesha anawajali watanzania basi aanze kwa jirani yake huyu ambaye nafikiri ameamua kuishi karibu na Ikulu ili iwe rahisi kwa rais kumuona na kumsaidia, kama kampeni zimezidia basi atoe maagizo kwa wizara inayohusika na watoto au manispaa ambazo kwa pamoja zingechukua hatua lakini zimelala usingizi na inavyoelekea tatizo la mama huyu hawajui kuwa linawahusu.
   
 2. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Pole sana but labda nikuulize umejiuliza umaskini na tabu anazozipata mama huyo zitaisaidia vp CCM Dar? wenzio wanasaidia maskini mikoani kuwapumbaza wanavijiji wanawajali wapate kura zao. Huyo mama hapo hata akisaidiwa impact ya kusaidiwa huyo mama kutawaconvince kwa kiwango gani wapiga kura Dar hasa maeneo hayo??? Ukipata jibu la swali hilo utajua kwanini hawamuoni huyo mama!!!!
   
 3. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Kuna wengi tu tena huyu mama unayemsema ni afadhali - ukitaka tukumwagie picha zao hapa nakwambia utatoka machozi? wewe badala ya kuongelea ni sera gani ya CCM ambayo inawasaidia wazee, vilema na watoto yatima ambayo ipo kwenye ilani yenu ya uchaguzi (inaonekana na wewe ni mmoja wao) wewe unakuja na hoja ya mama mmoja maskini kisa yupo karibu na Ikulu na wewe unamwona kila siku.

  Sioni hoja yako ya msingi.
   
 4. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,990
  Likes Received: 3,739
  Trophy Points: 280
  Thx. Kweli inaleta simanzi hali, especially watoto wanaumiza sana nikiwa kama mzazi!
   
 5. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  poleni sana but kuna jitihada zozote za binafsi mmefanya kumsaidia huyo mama
   
 6. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Aisee huyu mama huwa ananitisha sana,najiuliza analala wapi na wale watoto,ni karibia mwaka sasa,ukiwaangalia watoto wamechangamka na wanabadilisha nguo kama kawa,sijui wanakula wapi,alafu ni kama amechanganyikiwa maana nilishamkuta anakojoa mbele ya watoto wake,kuna jamaa alishajaribu kumfuata amuulize matatizo yake alichoambulia ni matusi ya nguoni.
   
 7. A

  Anold JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2010
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  ELNINO huwezi kuona hoja maana hata wewe ni walewaleeeee.ungesoma habari yote ungegundua kuwa sio huyo mama tu anayezungumziwa.
   
 8. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Anold, Umetumia mfano wa huyu mama, lakini hoja yako ingejikita zaidi kwenye sera za vyama vyetu ni kwa njisi gani wame address issue hii. hapo hoja yako ingekuwa na wigo mkubwa.

  Hoja yenyewe ina heading ya ajabu ajabu " Mama huyu anayeishi jirani na Ikulu asaidiwe na rais "

  ungejaribu kuweka hivi:-

  Kuelekea uchaguzi mkuu - Sera ya CCM na CHADEMA na CUF zinasemaje kuhusu kuwasadia
  a) Mama wajawazito na watoto
  b) Watoto yatima
  c) Wazee wasiojiweza
  d) Vilema & Walemavu wa ngozi ?

  Hapo sasa ungepiga na huo mfano wako wa huyu mama kukoleza hoja yako. sasa wataalam wa sera wangefumuka huko waliko na tungeona chama gani kimeadress issues hizi vizuri na hapo unakuwa mmemsaidia mpiga kura.
   
 9. m

  mkulu Member

  #9
  Sep 3, 2010
  Joined: Mar 27, 2009
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  tatizo kweli kweli ...... hata yale ambayo tunaweza kufanya sisi wenyewe (kama wewe uliyemuona) tunasubiri Rais aje!! Mwisho utasema hata mimi sina Vogue na Rais nakaa nae jirani pale hajanisaidia. Kama uliguswa na hilo ungesaidia kdg kuliko kulaumu tu
   
 10. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Rais au ikulu haiwezi kuwa suluisho la kila kitu. Kuna watu wameajiriwa na kazi zao ndio hizo. Waulize Maofisa ustawi wa jamii wilaya ya ilala au mkoa wa dar -es-saalam wamefanya nini. Je wanamjua huyo mama? Uhalisia wake ? Tatizo lake kitaalamu.ni lipi. Hi ni responsibility ya U USTAWI WA JAMII.

  Kuna watu hawako creative wala hawajitumi . Wanafanya kazi kwa mazoea tu .kazi zao ni kukaa kwenye madesk wakati wanatakiwa wawe frontline.kujua jinsi society yetu inavyopukutika. Siku hizi hata kesi za watoto wadogo kupigana zinapelekwa polisi. Inashangaza

  Sasa wana JF tuanze mfumo wa kwenda mbele zaidi kutafuta solutionkwa kuwasumbua moja kwa moja wale tunaodhani wanatakiwa kuwa na majibu. Kwa kuanza naomba mwenye number za simu za ofisi za ustawi wa jamii wilaya ya ilala au Mkoa wa dar es salaam.Ikiwezekana mwenye general line ya ofisi Wilaya

  Sasa hata watu binafsi atamsaidiaje watu kama hawa wakati hakuna source inayoweza kuamnikika kuelezea matatizo yao.

  Naamin ofisi hii ikipokea simu mbili tatu zinaulizia matatizo ya huyu mama watashtuka . wanaweza wasitoe suluhisho lakini some good change might happen
   
 11. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,076
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  inasikitisha!... kipindi alichopewa raisi wetu kidogo sana, inabidi tumuongezee mitano! mtaona mabadiliko watanzania
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Sep 4, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu, WAMA inatoa misaada kwa picha na kuita wanahabari ili michango yao zichapishwe ktk magazeti na TV. Ndani ya Uislaam/Ukristu, hii ni dhambi kubwa sana kujitangaza unapotoa msaada hasa ikiwa ni jukumu lako kulifanya. Kwa hiyo, maadam haya mambo yanakwenda kilaana laana ndio maana huyo mama haonekani kuwa muhimu kwa viongozi wetu ambao wanampita pale kila siku ya Mungu.
  Mwenyezi Mungu kawafumba macho yao..
   
 13. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #13
  Sep 4, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Picha na habari magazetini ni evidence za physical kuonnyesha WAMA inafanya kazi ili wapate misaada nje!!!
   
 14. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #14
  Sep 4, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kamanda... kikwete ni mtu wa watu, kaangalie yale ma-billboard yalivyotapakaa mjini akicheka na wazee na watoto... usitegemee zaidi ya hapo mkuu
   
 15. w

  wikama Member

  #15
  Nov 21, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM nia yao ni ikulu na sio kusaidia watu kama hawa ingekuwa ivyo ingekuwa imeondoa umaskini kwa kiwango kikubwa lakini angalia kila siku Rais anapita hapo anamuona lakini hajali we unafiri vipi hapo ? hii ni aibu we acha tu !!
   
 16. w

  wikama Member

  #16
  Nov 21, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ikulu ibadilike au ndio inajikusanyia ikijua kuwa uchaguzi ujao haitapata tena maana wananchi sasa hawataki kudanganywa CCM ikitaka iwatimizie yote tene kwa ufanisi wa hali ya juu la sivyo itapigwa chini kama mbuyu uangushwavyo kwa msumeno wa umeme !
   
 17. m

  matawi JF-Expert Member

  #17
  Nov 21, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mdondoaji umeongea point sana. Zile picha ni geresha tu za rais angekuwa na huruma angemshauri Chenge achukue vile visenti vije visaidie watanzania lakini wapi huwa wanajifanya hawaoni
   
Loading...