Mama Fulani, Nitakupenda Mpaka Kifo Kitakapotutenganisha!

Alfred

JF-Expert Member
Apr 13, 2008
1,632
1,875
Najua Bado sijakuoa ila Nina uhakika wa Kukuoa Kwa Mapenzi yake Mwenyezi Mungu!

Ulikuja Katika Maisha yangu wakati ambao nahitaji mapenzi ya mwanamke kwa kiasi kikubwa!

Ni wewe uliyerudisha Nafsi ya upendo iliyopotea baada ya kutokea kuumizwa na wanawake niliowahi kuwapenda!

Ni wewe uliyerudisha thamani ya upendo ndani ya Nafsi yangu!

Mwili na Nafsi yangu imenenepa kwa sababu yako, umenifanya kuwa bora mpaka wanawake wengine wananitamani!

Siku zote nakuombea kwa Mwenyezi Mungu azidi kukupa uzima wa Afya ya mwili na roho!

Si Juzi ulinambia Nisome wakorintho 1, 13...4-7, nimesoma mama na kilichomo mle ntakitimiza!

Nami Nakuahidi, Nitakupenda Kama Mke Wangu, Nitakulinda Kama Binti Yangu na Nitakuheshimu Kama Mama Yangu!

Nitakupenda Mpaka Kifo Kitakapotutenganisha!

Ni mimi Alfred!
 
Dogo umejulia mapenz ukubwan...leo kakuambia ya wakorintho kesho utajua sumu ya panya inauzwa kias gani

Empty set kabisa
 
hahahahahaha mapenzi yakiwa kwenye kilele unaweza toa ahadi zote mkuu, ngoja yayumbe kidogo ndo utajua utampenda milele ama.
 
Hiyo Wakorinto inasemaje!?
Screenshot_20171111-210258.png

Soma 4-7
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom