Mama Fatma Karume athibitisha Karume hakushiriki Mapinduzi ya Jan, 1964! TBC Live

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
Pengine tumekuwa tukishindwa kuelewa historia kamili ya mapinduzi ya zanzibar ya January,12 1963.
Wengi tulidhani mapinduzi yaliongozwa na Hayati Abeid Amani Karume.
Namsikia mjane wa Marehemu Karume akiojiwa na Susan Mungi katika TBC mama amekuwa wazi kueleza kuwa siku ya mapinduzi Hayati Karume alikuwa nyumbani amelala na milio ya risasi aliisikia wakiwa nyumbani na alimsikia mumewe akidai ni "vijana wake hao"
Baada ya muda milio ya risasi ilipokwisha,gari lilifika nyumbani kwao na kumchukua mumewe lakini yeye hakuweza kujua mpaka leo ni nani aliehusika kuongoza mapinduzi hayo.
 
Mama huyo ni mwanasiasa mzuri sana. Anajua upepo wa Zanzibar sasa unavuma kuyapinga mapinduzi kuwa hayakufanywa na wazanzibari.
Kaamua kwenda na upepo kujivua jukumu
 
Mama huyo ni mwanasiasa mzuri sana. Anajua upepo wa Zanzibar sasa unavuma kuyapinga mapinduzi kuwa hayakufanywa na wazanzibari.
Kaamua kwenda na upepo kujivua jukumu

hiki nacho kichekesho..........

siku ya mapinduzi alikuwa kalala.

siku ya kupigwa shaba alikuwa akicheza bao.

jamaa alikuwa masihara sana inaelekea.
 
kama ni hivyo inaonesha wazi kwamba kuna baadhi ya watu wachache wanaokula jasho na maumivu ya watu wengi zanzibar.je,ki nani hasa wanastahili kufaidi matunda ya mapinduzi hayo?
 
Pengine tumekuwa tukishindwa kuelewa historia kamili ya mapinduzi ya zanzibar ya January,12 1963.
Wengi tulidhani mapinduzi yaliongozwa na Hayati Abeid Amani Karume.
Namsikia mjane wa Marehemu Karume akiojiwa na Susan Mungi katika TBC mama amekuwa wazi kueleza kuwa siku ya mapinduzi Hayati Karume alikuwa nyumbani amelala na milio ya risasi aliisikia wakiwa nyumbani na alimsikia mumewe akidai ni "vijana wake hao"
Baada ya muda milio ya risasi ilipokwisha,gari lilifika nyumbani kwao na kumchukua mumewe lakini yeye hakuweza kujua mpaka leo ni nani aliehusika kuongoza mapinduzi hayo.
 
kama ni hivyo inaonesha wazi kwamba kuna baadhi ya watu wachache wanaokula jasho na maumivu ya watu wengi zanzibar.je,ki nani hasa wanastahili kufaidi matunda ya mapinduzi hayo?

wanyamwezi walokuwa wanahasiwa na kupelekwa oman
 
hiki nacho kichekesho..........

siku ya mapinduzi alikuwa kalala.

siku ya kupigwa shaba alikuwa akicheza bao.

jamaa alikuwa masihara sana inaelekea.

Mama kadanganya Karume alikuwa Tanganyika siku ya Mapinduzi pamoja na Babu
 
Nanajaribu kurafuta wapi niliisoma stiry ya siku yenyewe ya mapinduzi iliandikwa na mwandishi wa habari mmoja Mzanzibari, lakini siyo kama ambavyo tumekuwa tukisikia na kuambiwa na wanasiasa wetu.
Kwanza ona link hii kuhusu Field Marshal John Okello

Kama kuna mtu mwenye historia hii atuwekee hapa.

Rarely told story of John Okello « WAXSPELL
 
Pengine haijulikani kwa nini Okello hakuwahi kupewa wadhifa wowote wala kuingizwa katika orodha ya watu wa kuenziwa katika historia ya SMZ? Ni kwamba alisigana na Karume au alitumiwa tu kufanya uharamia kwa Serikali ya Sultan kisha kulipwa chake na kuondoka?
Mama huyu mtu mzima amegusia historia hii tata ya mapinduzi ya Zanzibar kwa hisia ya ajabu. Akieleza wanae akina Aman walikuwa vijana wadogo wanasoma ng'ambo (Malawi) zama zile za ukoloni wa sultan kumbe hii familia ilikuwa njema kiasi cha kusomesha watoto nje ya nchi?.
 
Hawa wanyamwezi waliohasiwa na kupelekwa Oman ilikuwa lini?

Nitajie mwaka tafadhali

Nenda Mji Mkongwe utakuta ki-chemba chanye mnyororo ulojaa kutu. pembeni yake kuna vyumba vya kiza kinene vyenye kitundu kidogo cha kupitishia hewa na mwanga kwa juu.
 
Pengine haijulikani kwa nini Okello hakuwahi kupewa wadhifa wowote wala kuingizwa katika orodha ya watu wa kuenziwa katika historia ya SMZ? Ni kwamba alisigana na Karume au alitumiwa tu kufanya uharamia kwa Serikali ya Sultan kisha kulipwa chake na kuondoka?
Mama huyu mtu mzima amegusia historia hii tata ya mapinduzi ya Zanzibar kwa hisia ya ajabu. Akieleza wanae akina Aman walikuwa vijana wadogo wanasoma ng'ambo (Malawi) zama zile za ukoloni wa sultan kumbe hii familia ilikuwa njema kiasi cha kusomesha watoto nje ya nchi?.

Ndio ukitazama video za baada ya mapinduzi walipoilizwa wapinduzi kwa nini walipindua jibu ni walipata majority of the votes japo kuwa walipata viti vichache vya bunge na hivyo kuamua kupindua.

Hizo dhana za utumwa na mengineyo ni dhana mpyampya.

Pia mapinduzi Zanzibar sasa hayana thamani yake kama zamani kwa sababu generation ya watawala sasa ni watoto wa wanamapinduzi waliozaa na waliopinduliwa.

Amani Karume ndugu zake wote nusu 'waarabu'

Shadya Karume na ndugu yake Mansour Yussuf Himid (waziri) mama yao ni kutoka ukoo watawala Wa kisultan

Mahmoud Thabit Kombo mama yake 'mhindi'

Hawawezi kutukuza mapinduzi sasa, wakati ushawapiga chenga.
 
Nenda Mji Mkongwe utakuta ki-chemba chanye mnyororo ulojaa kutu. pembeni yake kuna vyumba vya kiza kinene vyenye kitundu kidogo cha kupitishia hewa na mwanga kwa juu.

Historia naijua vyema, soko la watumwa lilikuwepo eneo lilipojengwa kanisa la Anglikana Mkunazini Unguja

Kanisa hilo limejengwa zaidi ya miaka mia moja naa sasa (limeanza kujengwa kwenye 1890)

Mapinduzi hayakuja kuondoa utumwa kwa kuwa haukuwepo 1964 sema sababu nyengine
 
Wanabodi,

Leo tunapoandhimisha Karume Day, kwa wale wenye access ya TV, please watch TBC Live, Mjane wa Karume, Bi. Fatma Karume, anahojiwa na Susan Mungi kuhusu kifo cha Karume.

Mahojiano hayo yalifanyika miaka ya nyuma na leo ni marudio, kwa kumbu kumbu yangu, nilipoyaona kwa mara ya kwanza, ndipo mbele ya safari alipotoboa siri ya Karume kutoshiriki Mapinduzi actively ambapo alitorokea bara.

Kipindi kimekatishwa, sijui kama kitaendelea.

More up date comming!.
 
Mahojiano hayo yako so emotional. kama una machozi ya karibu, lazima, utabubujikwa, Mama Karume, anatoa machungu ya moyoni jinsi alivyotelekezwa baada ya kifo cha mumewe, hakusaidiwa hata senti tano na viongozi wa SMS hata kumtembelea tuu na kumfariji kwa kumpa pole.

Msaada wake ulikuwa ni wanae Amani na Ali ambao wote walikuwa wanafanya kazi, ndio walimsupport.

Ukafikia wakati SMZ ikawatimua kazi wanae wote wawili na hapo ndipo maisha ya dhiki, taabu na mateso makuu yakamfika mama huyu...

Mkombozi pekee aliyejitokeza kumsaidia, alikuwa ni Julius, ndie alimpatia pesa, akamnunulia nyumba na kumpatia matumizi.

Mama Karume anazungumza kwa uchungu, machozi yanamtoka...Kipindi kikatishwa!
 
Sehemu ambayo haikuonyeshwa ni pale alipokuwa akizungumzia siku ya Mapinduzi, Karume aliondoka alifajiri ya mkesha wa Mapinduzi, aliwachukua wanae Ali na Amani, akaondoka nao kwa na mtumbwi kuja bara kushukia Bagamoyo ili kuwapeleka wanae hao shule ambako walikuwa wakisoma (kwao alikozaliwa Karume) Malawi!.
 
Kusema ukweli, huyu mtangazaji Susan Mungy, ni mtangazaji mahiri, mwenye kipaji cha hali ya juu, kuweza kufanya mahojiono ya kiwango hicho. Kama ni uwezo wangu, ningependa afanya mahojiano kama hayo na Mama Maria na waasisi waliopo hai, na kuyatunza mahojiano hayo kama sehemu ya huistoria kwa vizazi vijavyo.
 
Sehemu ambayo haikuonyeshwa ni pale alipokuwa akizungumzia siku ya Mapinduzi, Karume aliondoka alifajiri ya mkesha wa Mapinduzi, aliwachukua wanae Ali na Amani, akaondoka nao kwa na mtumbwi kuja bara kushukia Bagamoyo ili kuwapeleka wanae hao shule ambako walikuwa wakisoma (kwao alikozaliwa Karume) Malawi!.
Umejuaje kama sehemu unayoisema ilikuwepo lakini haikuonyeshwa, tupe clip ya hiyo part
 
Back
Top Bottom