Mama Diamond: Diamond hakuja kwenye msiba wa Godzilla kwa sababu angesababisha vurugu na watu wange zimia.

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,182
42,001
Wasalaam wana jamvi.

Mama wa msanii maarufu na tajiri kuliko wote nchi Diamond Platimuz ameweka wazi sababu za mwanae kutoonekana kwenye msiba na mazishi ya msanii mwenzie Godzilla.

Mama Diamond akihojiwa na moja ya chombo cha habari nchini aliulizwa kwanini Diamond hajaonekana kwenye msiba wa msanii mwenzie au hata kwenda kutoa pole?

Mama Diamond akijibu swali hilo kwa ufasaha amesema kuwa sababu ya mwanae kutokuja ni kutokana na mwanae kuwa msanii mkubwa sana nchini na hivyo kama angelifika pale angelisababisha tafrani na watu wote wangeacha kuhani msiba wangebaki kumuangalia yeye tuu
Pia aliongezea kuwa kama mwanae angelifika pale basi kungelitokea baadhi ya watu kuzimia .

Mama Diamond aliongezea kwa kusema hata kwenye msiba wa Kanumba mwanae alipotokea alisababisha vurugu na watu wengine kuzimia kwakuwa kila mtu alitaka kumuangalia Diamond.

Hata hivyo Mama Diamond alisema kuwa yeye kuja kwake ni kama amemuwakilisha mwanae.

Wasalaam
 
Mama Diamond sasa amekuwa msemaji wa mwanae!!!! Diamond ajue yeye ni brand maneno kama haya yanasemwa na mzazi yanampunguzia sana mashabiki na yanaaminika moja kwa moja kwa vile yametoka kwa Mama Diamond ivo awe makini na pia atoe katazo kwa wana ndugu kutoa taarifa zozote ni hatari sana


Pili mama Diamond sijui Amewahi kumshuhudia mtu anaitwa Mr Nice;?? Akajifunze kitu kutoka kwa mama mr nice
 
Back
Top Bottom