Mama Diamond anywea kwa Zari

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080


Mama Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ‘Sandra’,


Stori: Mayasa Mariwata, Risasi Jumamosi

DAR ES SALAAM: Imevuja! Baada ya muda mrefu kusambaa kwa habari kuwa mama wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Sanura Kassim ‘Sandra’, ‘haivi’ na mwandani wa msanii huyo, Zarinnah Hassan ’Zari The Boss Lady’, imedaiwa kuwa kwa sasa bi mkubwa huyo amenywea kwa kumkubali Zari.



Mpenzi wa Diamond, Zarinnah Hassan ’Zari The Boss Lady’


Taarifa hizo zilizopenyezwa na chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya familia ya Diamond zimeeleza kuwa, hivi karibuni mama Diamond amesalimu amri na kutamka hadharani kuwa Zari ni kiboko kuliko wanawake wote ambao mwanaye amewahi kuwa nao.

“Mama Diamond kanywea kwa Zari na wala hana lolote la kusema, unajua Zari kamtuliza sana Diamond! Si kama alivyokuwa huko nyuma. Huwezi amini juzikati mama Diamond katamka kabisa kwamba hakuna mwanamke kama Zari maana amemtuliza Diamond vilivyo,” kilichonga chanzo hicho.


Diamond


Baada ya kuunyaka ubuyu huo wa motomoto, Risasi Jumamosi lilimpandia hewani mama Diamond ili kumsikia anazungumziaje ubuyu huo ambapo baada kuelezwa kila kitu bi mkubwa huyo alijibu kwa kifupi na kukata simu:

“Eeeh mwanangu…eee..”

Risasi Jumamosi liliendelea kumpigia simu mama Diamond baada ya kukata lakini hakuweza kupokea tena.

Zari na mama Diamond wamedaiwa kuwa katika msuguano wa chinichini kutokana na kutoelewana tabia na kila mmoja kutomzungumzia mwenzake kwa mazuri hivyo kwa mama Diamond kudaiwa kusema anamkubali mkwewe huyo, ni dhahiri kwamba amekubali yaishe! Chanzo.GBP
 

Attachments

  • mama-D.jpg
    mama-D.jpg
    21.4 KB · Views: 366
  • ZARII.jpg
    ZARII.jpg
    25.4 KB · Views: 512
  • diamond.jpg
    diamond.jpg
    28.5 KB · Views: 256
Habari za Diamond ukishasema ( chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya familia umemaliza maana familia yake Mondi napo kumejaa wambeaa"
 
Ndio udaku ila wamejitahidi kuuandika kwa mazuri, sijui wamekuwaje kweli la shingogo bado gazeti hili au? :rolleyes:
 
so what?
Mitanzania mibwege {sio kila Mtanzania ni bwege} haina cha kufanya zaidi ya kumuwaza na kumfikiria Zari. Instance, FB, JF, blog, magazeti, mama mkwe zuzu, na wengine wengi hawana agenda isipokuwa zari
na we pia kufatilia vitu kama hiv ungepita kimy
 
Back
Top Bottom