Mama Beatrice Shelukindo peleka hoja binafsi bungenii nyumba za serikali zirudishwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama Beatrice Shelukindo peleka hoja binafsi bungenii nyumba za serikali zirudishwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Jun 22, 2012.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,972
  Likes Received: 37,537
  Trophy Points: 280
  Mama Shelukindo, awali ya yote nakupongeza sana kwa mchango wako wa jana bungeni kuhusu bajeti.Umeonyesha ukomavu wa hali ya juu kisiasa kwa kutambua mchango wa upinzani ktk maendeleo ya taifa lolote tofauti na wale wanaojiita wachumi wa daraja la kwanza lakini kisiasa,kimaadili,na hata kiungozi wametuthibitishia ni bure kabisa au tuseme ni zero.Wamesoma lakini hawajaelimika!
  Katika jambo moja uliloligusia ktk kuchangia bajeti jana, ni juu ya uamuzi ambao kwa kweli, una harufu ya ubinafsi na jambo hilo si lingine bali ni kuhusu uuzaji wa nyumba za serikali.Mimi binafsi nilisikitishwa na kuumizwa sana na huu uamuzi.Nachokushauri mama yangu ni kuwa hebu peleka hoja binafsi juu ya swala hili ili ikiwezekana nyumba hizi zirudishwe.Wabunge mkiamua jambo hili linawezekana kabisa.
  Nakumbuka mh.Christopher Ole Sendeka aliwahi kuahidi pale bungeni kuleta hoja binafsi juu ya swala hili lakini nashangaa mpaka leo yuko kimya.Sasa sijiu alitoa kauli ile kisiasa tu kutupiga changa la macho au bado ana nia ya kufanya hivyo mimi sijiu.
  Mama Shelukindo, maadamu umeligusia swala hili, ni vizuri ulifanyie kazi kwa uzito unaostahili na utakumbukwa siku zote za maisha yako kama ulivyofanya juu ya bwana Jairo.Najua hata huko bungeni wako wengi waliofaidika na uamuzi huu ila wewe timiza wajibu wako tu.
  Mwisho nasema mungu akupe nguvu na ujasiri na sisi wazalendo tuko nyuma yako ktk maombi.
   
 2. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2012
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mleta mada, sikutegemea kama ungeweza kupotosha hivi kwa jinsi ulivyomwelewa Beatrice Shelukindo. Mimi nilisikiliza hotuba yote aliyoitoa bungeni.

  Mwanzoni wakati nasoma thread yako nikadhani mama Shelukindo ametoa speech nyingine mbali na ile niliyosikia. Ni kweli mama Shelukindo alisema kuwa CHADEMA hotuba yao ni nzuri. Lakini ungemsikiliza vizuri mama Shelukindo aliendelea alisema hivi:

  {..tusiwachukie wapinzani wanapotukosoa. Kwa sababu kukosoa kwao si kwamba hawatupendi CCM. CHADEMA wangekuwa hawatupendi CCM wasingetukosoa hata kwa neno moja na badala yake hayo wanayotukosoa wangesubiri kuyasema kwenye kampeni 2015 na wakatuondoa madarakani.

  Lakini CHADEMA wanatukosoa sasa na bajeti zao nzuri ili tujirekebishe. Na tukijirekebisha basi tunaendelea kuwepo madarakani. Hivyo CHADEMA wanapenda tuendelee kuwepo madarakani kwa hiyo hata mimi Shelukindo nawahimiza waendelee kutukosoa na watuletee michango na bajeti nzuri ili tudumu madarakani..
  }

  Sasa tafakari mwenyewe hapo, kama kweli wewe ni mpenzi wa CHADEMA, huoni hapo umepigwa dongo la mwaka.

  Na kama mama Shelukindo huwa anasoma JF basi huko aliko atakuwa anacheka kupita maelezo.
   
 3. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,972
  Likes Received: 37,537
  Trophy Points: 280
  Mkuu ni wajibu wa chadema kukosoa maana bila kufanya hivyo watakuwa hawana umuhimu kwani mapungufu ni mengi na ya wazi na wao kama upinzani ndio jukumu lao.Vinginevyo hata umma utawadharau kama watakaa kimya au kuunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.
  Mkuu we hujagundua tu, kuwa hawa magamba ni sikio la kufa halisikii dawa.Hawana tofauti ni kina Gaddafi,Mubarraka na wengineo waliokuwa wamelewa madaraka na kujisahau na ndio maana kila mwaka wanaandaa bajeti za zima moto.Usikonde kiama chao kinakuja na wakishutika itakuwa tayari too late.
   
 4. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #4
  Jun 22, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Kurudisha nyumba zilizokuwa za SERIKALI? I bet my neck kama ataweza Mama Shelukindo mimi nitarudi CCM. Ninaomba umtumie hayo mapendekezo yako ktk email yake binafsi inapatikana kwenye tovuti ya bunge.

  If you have a short memory allow me to refresh you. Wakati JK anagombea 2005, mojawapo ya ahadi yake ilikuwa kurudisha nyumba zote za Serikali zilizouzwa. You know what happened.

  Mwaka huu Magufuri akatamba kwamba atawanyang'anya nyumba wale wote ambao hawajamaliza kuzilipia. I stand to be corrected hakuna hata mmoja aliyekwishanyang'anywa.

  Mark my words nyumba za serikali zinaweza kurudi tu kama Chama kingine kitaingia madarakani tumeoma Zambia under Satta, tunaona Malawi under Joyce Banda. lakini sio under Serikali ya CCM tuache kuota ndoto za alinacha.

  Under CCM wimbo wa nyumba za serikali utakuwa na chorus kama ile ya Serikali kuachana na mashangingi, Serikali kuhamia Dodoma etc.
   
 5. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,972
  Likes Received: 37,537
  Trophy Points: 280
  Ulichosema kwakweli kinawezekana na sina sababu ya kukupinga.
   
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,699
  Likes Received: 12,750
  Trophy Points: 280
  Yan hapo ana mpigia mbuzi gitaa,yan kweli serikali hii ni ya kurudisha nyumba?
   
 7. Zawadi B Lupelo

  Zawadi B Lupelo JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2017
  Joined: Jul 19, 2015
  Messages: 1,865
  Likes Received: 2,262
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja
   
 8. Yamakagashi

  Yamakagashi JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2017
  Joined: Sep 19, 2016
  Messages: 4,420
  Likes Received: 7,559
  Trophy Points: 280
  Huyo mama anapeleka hiyo hoja akiwa kaburini?
   
 9. Zawadi B Lupelo

  Zawadi B Lupelo JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2017
  Joined: Jul 19, 2015
  Messages: 1,865
  Likes Received: 2,262
  Trophy Points: 280
  Najua lakini hoja ya Ruttashoborwa ni nzuri sana
   
 10. Yamakagashi

  Yamakagashi JF-Expert Member

  #10
  Jun 14, 2017
  Joined: Sep 19, 2016
  Messages: 4,420
  Likes Received: 7,559
  Trophy Points: 280
  Haha sawa mkuu
   
 11. B

  BADO MMOJA JF-Expert Member

  #11
  Jun 14, 2017
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 1,767
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  HUYU MAMA BADO YUKO DUNAN AU HATA KUZMU KUNA JF??
   
 12. M

  Mlanga JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2017
  Joined: Jun 7, 2014
  Messages: 972
  Likes Received: 448
  Trophy Points: 80
  Mkuu umeelewaje hapo kwenye nyekundu?
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2017
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Zirudi serikalini zote ule ni wizi
   
 14. P

  Potassium Senior Member

  #14
  Jun 14, 2017
  Joined: May 12, 2014
  Messages: 118
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  wakirudisha hizo nyumba nahama ccm
   
Loading...