Mama atumia picha ya binti yake kuwasiliana na wanaume mtandaoni

Nafaka

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
12,156
31,039
Mama mmoja huko Marekani, alijiunga kwenye mtandao mmoja wa kijamii na kuweka picha ya mwanae mwenye umri wa miaka 18. Kisha alianza kuwasiliana na wanaume huku akijifanya kuwa yeye ndiye huyo binti kwenye hiyo picha.

Kutokana na urembo wa binti wanaume wengi mtandaoni hawakusita kumfuata Inbox wakimtongoza, mmojawapo akiwa Brian, ambaye alikuwa na umri wa miaka 45, akiwa na mke na watoto wawili. Mama alimkubari na wakaendelea kuwasilaina mtandaoni, na Brian wakiwa wanachat kwenye chatrooms huku wakiwatambia members wengine. Uhusiano wao uliendelea kwa muda mrefu pasipo kuwahi kukutana kwasababu walikuwa wanaishi miji tofauti.

Brian alikolea kwa penzi la mtandaoni kiasi kwamba, akaamua kumwambia siri hiyo rafiki yake aliyekuwa akifanya kazi naye ofisi moja. Rafiki yake huyo ambaye naye alikuwa member wa mtandao huo, alitambulishwa kwa huyo mpenzi mpya wa Brian, kumbe naye akaanza kumtamani.

Kila siku akawa anachat naye pasipo Brian kujua.

Baada ya muda mapenzi ya huyo mama yakahamia kwa rafiki yake Brian, akamwambia kuwa hamtaki tena ameanza kumpenda rafiki yake. Brian aliumia sana akaona kama amesalitiwa sana lakini alivumilia.

Lakini hawakuishia hapo, hao wawili waliendelea kuonyesha mahaba kwenye chatrooms (ni kama magroups kwenye whatsapp yalivyo kwa wale waliowahi kutumia the grid, yahoo messenger, mig33 enzi hizo mtakuwa mnaelewa).

Hilo suala lilimkera sana Brian, akaona isiwe kesi, akaamua kufanya jambo juu ya hilo. Usiku mmoja, Brian alichukua bunduki yake na kwenda kwa rafiki yake. Akamdanganya na kwenda naye kwenye parking ya Magari kisha rafiki yake akiwa amempa mgongo akamlamba shaba ya utosini na kummaliza pale pale. Hakuishia hapo usiku huo huo akawasha gari na kuanza sfari ya kuelekea kwenye mji alipokuwa anaishi yule mama aliyehisi ni binti.

Huku nyuma polisi waligundua mauaji yale, na kutambua mtekelezaji wa mauaji hayo, walienda mbali zaidi kwa kuchunguza computer ya Brian na kugundua nini kilipelekea kufanya mauaji hayo, hivyo wakawa na hofu kuwa huenda Brian anamfuatilia yule dada hivyo uhai wake uko mashakani.

Ikabidi wawataarifu askari wa mji huo wawahi kumweka dada katika sehemu salama, polisi wakaelekea mpaka kwao yule binti, nyumbani wakamkuta mama yake, na kumwambia kuwa mwanae yu wapi.

Akawambia kuwa yuko shule, ikabidi wamweleze kuwa yuko hatarini kutokana na wivu wa kimapenzi. Mama akaona haina haja bora awaeleze ukweli. Ndipo alipowambia kuwa yeye ndiye aliye nyuma ya ile picha na wala mtoto wake hajui lolote kuhusu lile.

Polisi walipigwa butwaa, na kushangaa inakuaje mzazi anafanya vile.

Mwisho wa siku Brian alikamatwa kushtakiwa na kufungwa.

Mama Hakushitakiwa na mtoto anasema mama yake alikuwa anatabia anamfuata na camera anamwambia aweke pozi mbalimbali saa nyingine akiwa kavaa nguo ya kulalia nyepesi anampiga picha bila kujua anzipeleka wapi.

Kuna watu wanatumia identies za watu wengine sana mtandaoni, sometimes dume lajifanya jike.
 
Back
Top Bottom