Mama apotea ghafla salendar bridge

nyaunyau

Senior Member
Oct 28, 2009
132
26
mama aliyepotea ghafla pale palmbeach surrender bridge amepatikana,mama huyo jina halijafahamika alikuwa akiendesha gari alipofika kwenye mataa alisimama aliamua kumsaidia mlemavu ombaomba kwa kumpa pesa,baada ya kitendo hicho alishanga kuona manyoya yameota mkononi ndipo alipomwita askari wa usalama barabarani,askari akamuuliza yule mlemavu ndipo mlemavu akasema kama mama huyo anataka kupona atoke garini amkumbatie,mama kusikia hivyo akaona easy akaenda kumkumbatia ndipo kufumba na kufumbua wakatoweka machoni pa askari na mashuhuda wengine.leo hii wachungaji wamefika eneo la tukio wamekemea nguvu hiyo hadi mama huyo amepatikana akiwa uchi na akili yake si nzuri yupo muhimbili hospitali kwa uchunguzi.source: praise power radio
 
hatari lakini salama
Maajabu ya dunia haya hivi hii habari na ya kuaminika ?
 
Yah,mpaka juzi nasikia hiyo habari kutoka kwa askari wa surrender bridge,ilikuwepo gari lake pale kituoni.Ni tukio gumu sana kuliamini lakini limetokea,kama kapatikana MUNGU ashukuriwe maana ilinitisha sana
 
Mh, jamani inabidi Jiji la Dar-es-Salaam liweke bayana jina la hilo daraja manake leo ndio nasoma hapa kumbe linaitwa "surrender" bridge?

:) Enjoy the weekend
 
Hii habari inachanganya sana, mbona kuna thread moja ilikuja hapa na kumnukuu mkuu wa polisi mkoa wa kipolisi wa kinondoni kuwa hizo habari si za kweli na zimeenea sana na polisi hawajapata hiyo taarifa? Je nje ya praise power kuna sehemu nyingi tena wametangaza? Mtujuvye vizuri jamani
 
uchawi-uchawi, uchawi.
hiki ni kielezo cha umasikini, uduni, shule haba, mawazo dhalili, na ndio maana hiyo habari imehit nnchi nzima kwa haraka..........kama unaandika kiwango cha ujinga wa nnchi hii ujue hiko ndicho kiashiria chake cha kwanza....unataka nini tena.?
achaneni na hizo habari, zinachochea ufukara na mtindio wa ubongo, ni UONGO na UONGO.
 
Wakuu hii ni story ya kijiweni nimefuatilia polisi wanasema si kweli na wamekanusha.
 
Stori ya abuwasi
Si story mkuu ni habari ambayo ilitangazwa hata kwenye radio,mtu wa kwanza kuniambia alikuwa mfanyakazi mwenzangu nilimbishia kabisa,wa pili akawa muuza duka naye nilimbishia ikabidi nimpigie jamaa yangu ni askari surrenderbridge,yeye alianza kunihadithia hata kabla sijumuulizia mwisho nikaja kuprove kwenye kipindi cha jahazi cha clouds.Ni kisa cha kushangaza sana.
 
Ni tatizo ya dini kufungamana na biashara katika karne hii. Tutasikia mengi sana.
 
yale yale ya mtu kageuka Chatu nakumbuka sana stori hii i think it was late 80s or early 90s!! maana mpaka sasa hata huyo trafiki wanaemsema alikuwepo hajatajwa jina wala hakuriport habari hiyo!!
 
Si story mkuu ni habari ambayo ilitangazwa hata kwenye radio,mtu wa kwanza kuniambia alikuwa mfanyakazi mwenzangu nilimbishia kabisa,wa pili akawa muuza duka naye nilimbishia ikabidi nimpigie jamaa yangu ni askari surrenderbridge,yeye alianza kunihadithia hata kabla sijumuulizia mwisho nikaja kuprove kwenye kipindi cha jahazi cha clouds.Ni kisa cha kushangaza sana.

Hassani,
Take it from me, hiyo habari sio ya kweli na haitakaa kuwa ya kweli. it is basically a hoax!
 
Hassani,
Take it from me, hiyo habari sio ya kweli na haitakaa kuwa ya kweli. it is basically a hoax!
Inawezekana unachosema mkuu,maana sources zangu zote ni hearsay,lakini nilichokuwa najiuliza ni kwa vipi hii habari isambae hivi,au ndo kama ya babu seya na JK.
 
Wakuu hii kitu haijatokea kabisa na haipo story imetungwa hiyo.
inasambaa haraka ni kwasababu ya jamii inataka kusikia miujiza, maluweluwe, ajabu na kila ushenzi,
ukitaka kujua jamii inakula nini ktk sekta ya habari na mawasiliano ya umma, wewe tazama namna habari za udaku zinavyo pokelewa, simple mind inatokana na elimu legelege, malezi ya hovyo hovyo..............hakuna lolote, ni ujinga mtupu.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom