GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,516
- 108,791
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa na ambayo pengine inaweza ' kuwashtua ' wengi hatimaye aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na sasa Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Mifuko ya Bima ya Afya Mama Anne Makinda amesema maneno ambayo wengi ' waliogopa ' kuyasema ila Yeye ' amethubutu '.
Akiwa ' mubashara ' jana usiku muda wa Saa 2 katika Kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha runinga ' mahiri ' kabisa nchin Tanzania Super brand cha ITV Mama Makinda alisema kuwa Mawaziri wa Serikali ya Dkt. Magufuli waache tabia za UNAFIKI, KUJIPENDEKEZA na UWOGA hasa katika ' utendaji ' wao wa Kazi zao za kila siku.
Huku akionekana ' kukerwa ' kabisa na hizi tabia ambapo hata uso wake tu ulitanabaisha hivyo Mama Makinda aliulizwa swali na Mtangazaji wa zamu wa jana Sam Mahela kuwa je anaonaje utendaji wa sasa wa Mawaziri wa awamu hii ya tano ndipo Mama nae bila kupepesa, kutikisa wala kumung'unya akayanyoosha vizuri sana maneno yake kama vile ambavyo nitamnukuu hapa chini.
" Mahela sina shida kabisa na utendaji wa Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwani ninamjua tokea akiwa Waziri ila tatizo langu kubwa na lazima hili niseme ukweli ni kwamba nawaomba Mawaziri wa sasa waache kuwa Wanafiki, waache tabia ya Kujipendekeza halafu wasipende kufanya Kazi zao kwa hofu au uwoga ".
" Utakuta Mtu anajua kabisa kuwa jambo fulani si zuri lakini analikubali kwa kujikosha halafu kuna wakati utaweza kuona kabisa kuwa Mtu fulani anaibua tu jambo fulani ambalo kimantiki unaona kabisa haliwezekani lakini atalilazimisha tu kwa Bwana Mkubwa ili mradi tu ajipendekeze kwa maslahi.Hata sasa hivi kuna baadhi ya Mawaziri ukiwaangalia tu sura zao utagundua zimejaa hofu tupu na Mimi nashangaa kama kweli unajiamini na unajua unatenda Kazi zako vizuri kwanini uwe na hofu? Kama unaona jambo fulani limekushinda kuliko Kuogopa kwanini usiende tu kwa Mheshimiwa Rais ukaomba ushauri wake ili akuelekeze na kisha ulitende kwa ubora zaidi? "
Maneno haya ningesema Mimi 'mngenishupalia ' humu sasa kayasema jana Kada kabisa wa ' Kutukuka ' wa Chama Tawala ( namaanisha CCM ) na mmoja wa Viongozi wanaoheshimika kabisa hapa nchini na kama kuna yoyoye anataka kuyathibitisha haya asubiria marudio ya hiki Kipindi kati ya leo mchana au Kesho mchana au aingie tu YouTube ili aone ' mzigo ' kamili jinsi Mama wa Watu alivyofunguka na kuamua kuwapa ' makavu ' mubashara Mawaziri wa Serikali ya Rais Dkt. Magufuli.
Nawasilisha.