Mama Anne Makinda awapa 'makavu' Mawaziri wa Rais Magufuli

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,533
2,000
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa na ambayo pengine inaweza ' kuwashtua ' wengi hatimaye aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na sasa Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Mifuko ya Bima ya Afya Mama Anne Makinda amesema maneno ambayo wengi ' waliogopa ' kuyasema ila Yeye ' amethubutu '.

Akiwa ' mubashara ' jana usiku muda wa Saa 2 katika Kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha runinga ' mahiri ' kabisa nchin Tanzania Super brand cha ITV Mama Makinda alisema kuwa Mawaziri wa Serikali ya Dkt. Magufuli waache tabia za UNAFIKI, KUJIPENDEKEZA na UWOGA hasa katika ' utendaji ' wao wa Kazi zao za kila siku.

Huku akionekana ' kukerwa ' kabisa na hizi tabia ambapo hata uso wake tu ulitanabaisha hivyo Mama Makinda aliulizwa swali na Mtangazaji wa zamu wa jana Sam Mahela kuwa je anaonaje utendaji wa sasa wa Mawaziri wa awamu hii ya tano ndipo Mama nae bila kupepesa, kutikisa wala kumung'unya akayanyoosha vizuri sana maneno yake kama vile ambavyo nitamnukuu hapa chini.

" Mahela sina shida kabisa na utendaji wa Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwani ninamjua tokea akiwa Waziri ila tatizo langu kubwa na lazima hili niseme ukweli ni kwamba nawaomba Mawaziri wa sasa waache kuwa Wanafiki, waache tabia ya Kujipendekeza halafu wasipende kufanya Kazi zao kwa hofu au uwoga ".

" Utakuta Mtu anajua kabisa kuwa jambo fulani si zuri lakini analikubali kwa kujikosha halafu kuna wakati utaweza kuona kabisa kuwa Mtu fulani anaibua tu jambo fulani ambalo kimantiki unaona kabisa haliwezekani lakini atalilazimisha tu kwa Bwana Mkubwa ili mradi tu ajipendekeze kwa maslahi.Hata sasa hivi kuna baadhi ya Mawaziri ukiwaangalia tu sura zao utagundua zimejaa hofu tupu na Mimi nashangaa kama kweli unajiamini na unajua unatenda Kazi zako vizuri kwanini uwe na hofu? Kama unaona jambo fulani limekushinda kuliko Kuogopa kwanini usiende tu kwa Mheshimiwa Rais ukaomba ushauri wake ili akuelekeze na kisha ulitende kwa ubora zaidi? "

Maneno haya ningesema Mimi 'mngenishupalia ' humu sasa kayasema jana Kada kabisa wa ' Kutukuka ' wa Chama Tawala ( namaanisha CCM ) na mmoja wa Viongozi wanaoheshimika kabisa hapa nchini na kama kuna yoyoye anataka kuyathibitisha haya asubiria marudio ya hiki Kipindi kati ya leo mchana au Kesho mchana au aingie tu YouTube ili aone ' mzigo ' kamili jinsi Mama wa Watu alivyofunguka na kuamua kuwapa ' makavu ' mubashara Mawaziri wa Serikali ya Rais Dkt. Magufuli.

Nawasilisha.
 
MeinKempf

JF-Expert Member
Jun 11, 2013
11,107
2,000
Umaarufu kazi kweli kweli ...kila kauli unayoitoa inafunguliwa uzi au kutafutiwa
heading katika magazeti , radio , tv na mitandao ya kijamii.
Ngoja nami nijitahidi kuwa maarufu labda ntakumbukwa maana haya maneno angeyasema
Hasimu Rungwe au mrema yangeonekana ya kawaida sana wala yasingekuwa mada hapa jamvini.
 
MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,743
2,000
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa na ambayo pengine inaweza ' kuwashtua ' wengi hatimaye aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na sasa Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Mama Anne Makinda amesema maneno ambayo wengi ' waliogopa ' kuyasema ila Yeye ' amethubutu '.

Akiwa ' mubashara ' jana usiku muda wa Saa 2 katika Kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha runinga ' mahiri ' kabisa nchin Tanzania Super brand cha ITV Mama Makinda alisema kuwa Mawaziri wa Serikali ya Dkt. Magufuli waache tabia za UNAFIKI, KUJIPENDEKEZA na UWOGA hasa katika ' utendaji ' wao wa Kazi zao za kila siku.

Huku akionekana ' kukerwa ' kabisa na hizi tabia ambapo hata uso wake tu ulitanabaisha hivyo Mama Makinda aliulizwa swali na Mtangazaji wa zamu wa jana Sam Mahela kuwa je anaonaje utendaji wa sasa wa Mawaziri wa awamu hii ya tano ndipo Mama nae bila kupepesa, kutikisa wala kumung'unya akayanyoosha vizuri sana maneno yake kama vile ambavyo nitamnukuu hapa chini.

" Mahela sina shida kabisa na utendaji wa Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwani ninamjua tokea akiwa Waziri ila tatizo langu kubwa na lazima hili niseme ukweli ni kwamba nawaomba Mawaziri wa sasa waache kuwa Wanafiki, waache tabia ya Kujipendekeza halafu wasipende kufanya Kazi zao kwa hofu au uwoga ".

" Utakuta Mtu anajua kabisa kuwa jambo fulani si zuri lakini analikubali kwa kujikosha halafu kuna wakati utaweza kuona kabisa kuwa Mtu fulani anaibua tu jambo fulani ambalo kimantiki unaona kabisa haliwezekani lakini atalilazimisha tu kwa Bwana Mkubwa ili mradi tu ajipendekeze kwa maslahi.Hata sasa hivi kuna baadhi ya Mawaziri ukiwaangalia tu sura zao utagundua zimejaa hofu tupu na Mimi nashangaa kama kweli unajiamini na unajua unatenda Kazi zako vizuri kwanini uwe na hofu? Kama unaona jambo fulani limekushinda kuliko Kuogopa kwanini usiende tu kwa Mheshimiwa Rais ukaomba ushauri wake ili akuelekeze na kisha ulitende kwa ubora zaidi? "

Maneno haya ningesema Mimi 'mngenishupalia ' humu sasa kayasema jana Kada kabisa wa ' Kutukuka ' wa Chama Tawala ( namaanisha CCM ) na mmoja wa Viongozi wanaoheshimika kabisa hapa nchini na kama kuna yoyoye anataka kuyathibitisha haya asubiria marudio ya hiki Kipindi kati ya leo mchana au Kesho mchana au aingie tu YouTube ili aone ' mzigo ' kamili jinsi Mama wa Watu alivyofunguka na kuamua kuwapa ' makavu ' mubashara Mawaziri wa Serikali ya Rais Dkt. Magufuli.

Nawasilisha.
Mama makinda sio Mwenyekiti wa bodi ya mifuko ya hifadhi ya jamii, ni Mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa taifa wa bima ya afya. Naamini ameonyesha mfano mzuri kwa viongozi wastaafu kujifunza kusema kweli kwa viongozi walio madarakani
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,533
2,000
Mama makinda sio Mwenyekiti wa bodi ya mifuko ya hifadhi ya jamii, ni Mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa taifa wa bima ya afya. Naamini ameonyesha mfano mzuri kwa viongozi wataafu kujifunza kusema kweli kwa viongozi walio madarakani

Akhsante Mkuu wa hiyo observation yako ya ' kutukuka ' kabisa na nimesharekebisha hapo juu. Big up sana kwani Mwanamume ' nilikengeuka ' ki Kimbukumbu.
 
Cathode Rays

JF-Expert Member
Nov 3, 2011
1,738
1,250
Umaarufu kazi kweli kweli ...kila kauli unayoitoa inafunguliwa uzi au kutafutiwa
heading katika magazeti , radio , tv na mitandao ya kijamii.
Ngoja nami nijitahidi kuwa maarufu labda ntakumbukwa maana haya maneno angeyasema
Hasimu Rungwe au mrema yangeonekana ya kawaida sana wala yasingekuwa mada hapa jamvini.

Rungwe na Mrema its a non story au hata ikiwa story haiwi na uzito kwa sababu wanajulikana kuwa ni opposition na opposition wanachotafuta ni point of weakness ya aliyeko madarakani
 
Getang'wan

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
2,525
2,000
Mama makinda sio Mwenyekiti wa bodi ya mifuko ya hifadhi ya jamii, ni Mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa taifa wa bima ya afya. Naamini ameonyesha mfano mzuri kwa viongozi wataafu kujifunza kusema kweli kwa viongozi walio madarakani
Kusema ukweli ukiwa umeshatoka kwenye madaraka hakukufanyi uonekane wa maana zaidi ya mnafiki kwasababu wakati akiwa madarakani na katika nafasi nzuri ya kukemea mabaya na kushauri namna ya kuenenda hakufanya hivyo. Naye atabaki kuwa mnafiki tu. Akumbuke ufedhuli aloufanya kukilinda chama chake wakati ule akiwa spika. Mijadala muhimu ya kitaifa akafanya figisufigisu za kutosha tu.
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,533
2,000
Mama kaongea point sana, naamini mawaziri wamemsikia watalifanyia kazi hasa mawaziri hawa wafuatao Nchemba, Ummy Mwalimu, P Mpango, Ndalichako, Mwakyembe, Mbarawa, Angela kairuki, Mhagama, Simbachawene.

Na nimesikia kuwa katika hao uliowataja hapo kuna ' Njemba ' moja hivi inataka ' Kumrithi ' Magufuli coming 2025. Kazi ipo hakyanani!
 
sawabho

JF-Expert Member
Feb 25, 2011
5,295
2,000
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa na ambayo pengine inaweza ' kuwashtua ' wengi hatimaye aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na sasa Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Mifuko ya Bima ya Afya Mama Anne Makinda amesema maneno ambayo wengi ' waliogopa ' kuyasema ila Yeye ' amethubutu '.

Akiwa ' mubashara ' jana usiku muda wa Saa 2 katika Kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha runinga ' mahiri ' kabisa nchin Tanzania Super brand cha ITV Mama Makinda alisema kuwa Mawaziri wa Serikali ya Dkt. Magufuli waache tabia za UNAFIKI, KUJIPENDEKEZA na UWOGA hasa katika ' utendaji ' wao wa Kazi zao za kila siku.

Huku akionekana ' kukerwa ' kabisa na hizi tabia ambapo hata uso wake tu ulitanabaisha hivyo Mama Makinda aliulizwa swali na Mtangazaji wa zamu wa jana Sam Mahela kuwa je anaonaje utendaji wa sasa wa Mawaziri wa awamu hii ya tano ndipo Mama nae bila kupepesa, kutikisa wala kumung'unya akayanyoosha vizuri sana maneno yake kama vile ambavyo nitamnukuu hapa chini.

" Mahela sina shida kabisa na utendaji wa Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwani ninamjua tokea akiwa Waziri ila tatizo langu kubwa na lazima hili niseme ukweli ni kwamba nawaomba Mawaziri wa sasa waache kuwa Wanafiki, waache tabia ya Kujipendekeza halafu wasipende kufanya Kazi zao kwa hofu au uwoga ".

" Utakuta Mtu anajua kabisa kuwa jambo fulani si zuri lakini analikubali kwa kujikosha halafu kuna wakati utaweza kuona kabisa kuwa Mtu fulani anaibua tu jambo fulani ambalo kimantiki unaona kabisa haliwezekani lakini atalilazimisha tu kwa Bwana Mkubwa ili mradi tu ajipendekeze kwa maslahi.Hata sasa hivi kuna baadhi ya Mawaziri ukiwaangalia tu sura zao utagundua zimejaa hofu tupu na Mimi nashangaa kama kweli unajiamini na unajua unatenda Kazi zako vizuri kwanini uwe na hofu? Kama unaona jambo fulani limekushinda kuliko Kuogopa kwanini usiende tu kwa Mheshimiwa Rais ukaomba ushauri wake ili akuelekeze na kisha ulitende kwa ubora zaidi? "

Maneno haya ningesema Mimi 'mngenishupalia ' humu sasa kayasema jana Kada kabisa wa ' Kutukuka ' wa Chama Tawala ( namaanisha CCM ) na mmoja wa Viongozi wanaoheshimika kabisa hapa nchini na kama kuna yoyoye anataka kuyathibitisha haya asubiria marudio ya hiki Kipindi kati ya leo mchana au Kesho mchana au aingie tu YouTube ili aone ' mzigo ' kamili jinsi Mama wa Watu alivyofunguka na kuamua kuwapa ' makavu ' mubashara Mawaziri wa Serikali ya Rais Dkt. Magufuli.

Nawasilisha.
Mtu akiwa nje ya uwanja ni rahisi sana kuona makosa ya mchezaji fulani anayecheza.
 
GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,533
2,000
Mtu akiwa nje ya uwanja ni rahisi sana kuona makosa ya mchezaji fulani anayecheza.

Kwahiyo ndiyo kusema kuwa nanyi hamkubaliani na hayo aliyoyasema ' Bidashi ' Anne Makinda? Mbona ' kafunguka ' vizuri sana tu Mkuu?
 
Getang'wan

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
2,525
2,000
Kwani ' kuwakemea ' akina Mnyika, Lissu na Wenje wakati ule alipokuwa Spika Bungeni nalo halitoshi kuwa moja ya jambo lake jema alilolifanya Mkuu?
Gentamycine (Gentamicin) we ni kiboko. Kweli we ni dawa ya binadamu na mifugo. Alivyowadhibiti wale vijana hawakuona kama alifanya jema
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom