Mama Anne Kilango | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama Anne Kilango

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mzito Kabwela, Dec 12, 2009.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Dec 12, 2009
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Na Imelda Mtema

  Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela ameamua kufunua ya ndani kuhusu maisha yake, kuanzia biashara, siasa, kazi, mapenzi, ndoa na familia kwa jumla...

  Gazeti lisilopitwa na kitu, Risasi Jumamosi linadondosha kila kitu kuhusu Anne na mume wake, Waziri Mkuu Mstaafu, John Samuel Malecela kama mahojiano yao yalivyorushwa na Televisheni ya Taifa, TBC1 Jumatano iliyopita.

  Akihojiwa na mtangazaji, Susan Mungi katika kipindi cha Ua Letu, Anne alisema kuwa mapenzi yana siri kubwa na kwamba yeye kufikia alipo sasa, ameona na kukutana na mengi.

  Alisema, mapenzi yanatesa na kusisitiza kuwa anaona ni vizuri kuweka kila kitu kweupe kwa lengo la kuwapa muongozo na ujasiri wanawake wengine ili waweze kujifunza hali halisi ya maisha kupitia kwake.
  Aliongeza, kabla ya kutua kwa Malecela, alikumbana na msoto wa kimapenzi kwa mume wake wa kwanza anayeitwa Hans Nyange, baada ya mwanamke mmoja kuingilia ndoa yake.

  "Alikuwa ni mwanaume mwenye uwezo mzuri, alikuwa Financial Controller (Msimamizi wa Fedha) wa TBL, ndoa ilikuwa na amani lakini ghafla amani ikaanza kutoweka, ndani hakukuwa na maelewano.

  "Nilipoona hivyo, nikajua kuna mtu wa tatu ameingia kwenye ndoa yetu, nikapeleleza na kumgundua huyo mwanamke kuwa ndiyo tatizo. Baada ya kugundua hilo, sikutaka matatizo, nilidai talaka tukaachana," alisema Anne na kuongeza:

  "Sikudai kitu chochote, niliacha vyote ila nikapigania haki ya kulea wanangu nikapewa. Tulikuwa na nyumba mbili, nikahamia kwenye moja pamoja na wanangu lakini magari na vitu vingine niliviacha na kwenda kuanza maisha upya.

  "Wakati huo nilikuwa Mhasibu Air Port, ili kumudu kulea familia, nikawa naamka saa 10 usiku, nakaanga maandazi na samaki kisha nikawa naenda kuuza kazini kwangu (Uwanja wa ndege).

  "Pale nyumbani nikafungua genge kubwa la kuuza bidhaa mbalimbali, hiyo yote ni katika kutafuta pato la ziada. Ni wakati huo nikaanza kuwafundisha wanangu kupanda daladala kwa sababu walikuwa wamezoea magari yao.

  "Maisha yakawa yanaendelea hivyo hivyo kwa tabu, lakini nikazoea na wanangu wakazoea, tukawa tunakula bila matatizo na ada ya shule ilipatikana bila tabu."

  Aliendelea kusema kuwa wakati anafanya uamuzi huo wa kupambana na maisha, lengo lake lilikuwa ni kuuonesha umma kwamba mwanamke anaweza, hivyo kubaki mjane haina maana safari ya mafanikio kimaisha ndiyo mwisho.

  Kuhusu alivyoingia kwenye siasa, Anne alisema kwamba siku zote alipenda kupigania haki za watu, hivyo aliamua kujitosa moja kwa moja ili kutimiza malengo yake ya kuwa mtetezi wa wanyonge.

  Alisema kuwa alikutana na Malecela wakati akiwa kwenye harakati za kisiasa, akavutiwa naye kabla ya kuamua kuwa wapenzi na baadaye ndoa.

  "Nilivutiwa na Malecela kwa sababu sikuona kama natenda dhambi, nilimkuta hana mke, na mimi katika maisha yangu sipendi kuingia kwenye dhambi ya kuingilia ndoa ya mtu," alisema Anne na kuongeza:

  "Nilianza na Malecela kama marafiki, lakini tukawa tuna amani kwa sababu hatukuwa tunamdhulumu mtu, mimi sikuwa na mume na Malecela alikuwa singo, na urafiki wetu ulikuwa wazi. Baadaye tukaona si vizuri kuendelea kutenda dhambi, kwahiyo tukafunga ndoa."

  Alisema, kabla ya ndoa kilifanyika kikao cha familia ambapo yeye na Malecela, kila mmoja aliita watoto wake hata wale wanaoishi nje ya nchi na kuwaeleza dhamira yao ya kuoana, ambapo waliwakubalia kwa moyo mmoja.
  Kuhusu maisha yake ya kifamilia, Anne alisema kuwa hivi sasa yeye ni mwenye amani tele, akiamini kwamba Malecela ndiye mwanaume wa maisha yake.

  Anne alionya wanawake kuwa hakuna kitu kibaya kwenye maisha kama kutembea na mume wa mtu, na akasisitiza kwamba ataendelea kumlaani yeyote anatakayejiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi na mume wa mtu.

  "Mimi nilishaonja machungu ya ndoa kuingiliwa na mtu wa tatu, siku zote ndoa ikishakuwa na mtu wa tatu huwa haidumu kwa sababu migogoro haiishi," alisema.

  Katika kipindi hicho, Anne alionesha mazingira ya nyumba yao na mtindo wa maisha yao kama familia iliyo imara na yenye upendo.

  Anne pia, aliingia jikoni na kuandaa chakula, akibeba uhalisia kama mama wa nyumba na baadaye malecela aliitwa mezani kwa ajili ya maakuli ambapo kabla ya yote, alitumia muda mfupi kuomba na kumshukuru Mungu kwa ajili ya kukibariki chakula.

  Source: Risasi
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Dec 12, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  This is the NEWS to me...

  Not anything else.

  Absolutely nothing!..huh!
   
 3. g

  grandpa Senior Member

  #3
  Dec 12, 2009
  Joined: Aug 24, 2008
  Messages: 185
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Walimhoji kuhusu tuhuma alizorushiwa na Sofia Simba kuwa alikutwa na dawa za kulevya. Hio biashara ya dawa za kulevya aliifanya akiwa na Hans Nyange au wakati akiwa singo au wakati yuko na mzee mzima Malecela? Sijasikia huyu mama akikanusha kuwa tuhuma za Sofia Simba ni uongo zaidi ya Malecela kusema Sofia Simba aende Mirembe. Her silence about that zinatufanya wengine tuewele kuna ukweli fulani kuhusu hiyo tuhuma ya dawa za kulevya.
   
 4. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #4
  Dec 12, 2009
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280

  wake wa vigogo wengi ni vicheche
   
 5. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #5
  Dec 12, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,054
  Likes Received: 752
  Trophy Points: 280
  Hivi kweli wewe ni grandpa???Unataka ajibishane na mwehu????Don't argue with a fool......malizia hapa ndo utapata jibu kwa nini alikaa kimya.Katika mawaziri bogus huyo mama Lion mie naona ndie nambari one.....bisha???
  .....ndio hio.
   
 6. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Maisha yake ni changamoto kwa wanawake woooote wajane hai (yaani wale walioochika). Sometimes tunang'ang'ania hizi ndoa end of the day inakuwa unhealth. Unatakiwa kama mwanamke ungangamale tu kivyako mambo yakiwa vice versa.

  Hatusemi muchike, ila ikishindikana mwenzangu toka tu ukaanze life afresh.
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Dec 14, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,157
  Trophy Points: 280
  mama...mamaaa ..maaaaaaa.mama huyoooo mama ...mamama huyooo
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  bogus aliyemchagua kuwa waziri..yeye hana kosa
   
Loading...