Mama Anne Kilango na Ajira za Emirates

Bungeni patamu!

Muda mfupi uliopita mama Anne Kilango amemaliza kuchangia hoja ya jinsi gani vijana wasaidiwe kupata ajira. Kama kawaida yake ameirarua serikali.Amesema kuna siku amesafiri na ndege ya shirika la Emirates, mle ndani alikutana na mfanyakazi mtanzania anaitwa Felister.

Mama Anne Kilango alimdadisi yule dada hadi akamwambia kati ya wafanyakazi 15,000 wa shirika lile wapo watanzania 9, wakenya 800, sababu ni kuwa wakenya nafasi zikitoka serikali yao inaintervene kuwatafutia vijana wake. Mama Kilango anasema huo ni uzembe wa serikali yetu.

Mara palepale mbunge MACHALI akaomba kutoa taarifa na bahati mbaya naibu spika akamruhusu, Machali akampa taarifa mama Kilango kuwa "Kenya wamefikia pale kwa sababu walifanikiwa kukiondoa chama tawala madarakani".

Majibu ya mama Kilango yalikuwa ya aibu maana kwa kujivuta na ile sauti yake ya mkwara akasema."Taarifa hiyo naifuta na wala sitaki kuisikia"

Nimeipenda hiyo. Na kwa bahati mbaya naibu spika akamruhusu...
 
Well Said mkuu - binafsi swala hili nilisha liona mapema sana - Serikali yetu isipo jitahidi kumaliza kero za ndugu zetu Waislaam sitashangaa siku moja Nchi hii ukakuta inagawanyika mara mbili kama ilivyo gawanyika Sudan - kusini Wakristo na Kasikazini Waislaam. Labda nieleweke kwamba sio kwamba nataka/pendekeza hilo litokee lakini tukumbuke binadamu wana kikomo cha kuvumulia, hamuwezi kuapuuzia malalamiko ya kweli ya kundi la madhehebu fulani miaka yote - tusije tukajidanganya hapa.

Historia inaonyesha hii si mara ya kwanza nchi moja kugawanyika kwa misingi ya Dini - India kwa mfano: Wakati India inatawaliwa na Waingereza hapakuwepo nchi inayo julikana kama Pakistani wala Bhangladeshi, katika harakati za kutaka kukomboa India, Kiongozi wa Kislaam aliye julikana kwa jina la Mohammed Ali Jinnah alimwendea rafiki na mwanaharakati mwenzake wa madhehebu ya kihindu aliyejulikana kwa jina la Mohandas Karamchand Gandhi (wote walisomea Sheria Chuo kikuu London kweye miaka ya mwishoni mwa 1800). Jinnah kamweleza kinaga ubaga Ghandi kwamba India ukinyakua uhuru basi nchi hiyo ingawane sehemu mbili - moja iwe kwa Wahindu na nyingine kwa ajili ya Waislaam, Gandhi alijitahidi sana kumsihi Jinna kwamba wawe kitu kimoja wasigawe nchi, Jinna alimkatalia akisema Waislaam wananyanyaswa sana hawewezi kukubali kuwa chini ya Wahindu, kapeleka swala lake UN na akakubaliwa kuhunda Taifa la Pakistani na yeye kuwa Waziri mkuu wa kwanza wa Taifa jipya la Pakistani, kama sikosei tatizo hili limekuja kujirudia tena miaka ya hivi karibuni nchini Yugoslavia ilikuja kugawanywa kwa misingi hii hii.

Kwa hiyo ninapo toa tahadhali nafikilia vitu kama hivyo, lakini kwa bahati mbaya kuna baadhi ya Watanzania wenzangu kwenye forum hii ambao aidha awanielewi au ni watu wenye dhalau zisizo na tija kwa kukosa kutafakali mambo kwa kina, oh yes kuna mmoja wao amediriki kusema mimi ni MPUMBAVU!!! - hizo ndio hulka za baadhi ya Watanzania wenzetu tulivyo, you can't blame 'em! Can U? inategemea walivyo kuwa brought UP - wana thrive kutokana na MATUSI waliyo ya-acquire utotoni.
mkuu kwanza nashukuru kwa historia ya pakstan, bangladesh na India, sikuwahi hata kufikiria kitu kama hicho.
pili asante pia kwa ujumbe murua, kwamba binadamu analevel ya uvumilivu baada ya hapo liwalona liwe
na tatu nikuambie tu, wengi wanaosoma humu wanajua sana kutokana na elimu ya uraia tunayoitoa humu ila wanajifanya vichwa maji. lakini pia wapo wachache ambao hawajui chochote kwa hiyo hata unapoandika kitu kama hicho wao wanaona ni uchochezi tu. hawa ni wakusamehewa bure na ipo siku wataelewa.
All in all, thanks.
 
Pamoja mkuu, Godbless.
 
​Bungeni patamu!

Muda mfupi uliopita mama Anne Kilango amemaliza kuchangia hoja ya jinsi gani vijana wasaidiwe kupata ajira. Kama kawaida yake ameirarua serikali.Amesema kuna siku amesafiri na ndege ya shirika la Emirates, mle ndani alikutana na mfanyakazi mtanzania anaitwa Felister.

Mama Anne Kilango alimdadisi yule dada hadi akamwambia kati ya wafanyakazi 15,000 wa shirika lile wapo watanzania 9, wakenya 800, sababu ni kuwa wakenya nafasi zikitoka serikali yao inaintervene kuwatafutia vijana wake. Mama Kilango anasema huo ni uzembe wa serikali yetu.

Mara palepale mbunge MACHALI akaomba kutoa taarifa na bahati mbaya naibu spika akamruhusu, Machali akampa taarifa mama Kilango kuwa "Kenya wamefikia pale kwa sababu walifanikiwa kukiondoa chama tawala madarakani".

Majibu ya mama Kilango yalikuwa ya aibu maana kwa kujivuta na ile sauti yake ya mkwara akasema."Taarifa hiyo naifuta na wala sitaki kuisikia"
Sio kweli kabisaaaaaaaaa watanzania wapo zaidi ya hao anao wataja hakua na lakusema huyo mama na huyo alomwambia, aanze na crew mpaka ground staff wa Emirates ataona alitaka kujihashua tu na yeye....
 
Japokuwa idadi hatuna uhakika nayo but wakenya wanachukua sana nafasi zetu,,

Nimeshatumia qatar airways,, ile inayotoka Dar to doha and then connection to final destination ina wakenya wengi kuliko watanzania.. Kampuni za ndege za kiarabu zina utaratibu wa kuweka natives kwenye cabin crew team ili kusaidia lugha wasafiri wasiojua kiingereza,,, sasa kwenye ndege ya kuja Tanzania unakuta wakenya ndio wametawala wakati kiuhalisia walitakiwa wawe Watanzania... Unakuta ndege ya dar wakenye ndio wanahudumia Passenger wasiojua kiingereza ambayo hiyo nafasi walitakiwa wawe Watanzania..
 
Wakenya wengi sikatai lakini na wa Tanzania pia wamo na sio kila filght ya dar nilazima uwakute wanakwenda safari nyengine,na watanzania wengi customer service yao sio nzuri kabisa na English ndio hivyo tena,sasa tukubali yote,vile vile kama umeshawahi kupita Dubai Airport check inn staff wengi wa TZ bording gate sema sura zao hazijulishi mpaka waongee...
 
Back
Top Bottom