Mama Anna Tibaijuka atangaza kutogombea tena ubunge, asema nchi ilikuwa inasubiri kiongozi na sio Rais

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,441
7,780
Mbunge wa Muleba Kusini, Prof. Anna Tibaijuka akihojiwa wakati wa ziara ya Rais Magufuli kiwanda cha sukari Kagera, amesema hii itakuwa awamu yake ya mwisho kugombea ubunge na anang'atuka Kama msemo wa Mwalimu Nyerere.

Amesema ataendelea kuwepo kwenye jamii lakini ni wakati wa kuwapa nafasi vijana na maarifa yao yataendelea kutumika kwenye ushauri katika kusonga mbele.

Kuhusu utawala wa Rais Magufuli, amesema nchi ilikuwa inasubiri kiongozi na sio Rais. Tibaijuka amesema Rais inabidi pia awe kiongozi kwa sababu inawezekana kuwa Rais kwa nafasi lakini anaongoza?

Amedai kinachoonekana sasa Tanzania ni uongozi na umefika wakati wa kujua tofauti, amesema ujasiri unatokana na ukweli kwani mtu hawezi akawa muongo na jasiri kwani anaweza kuja mtu akamuumbua hivyo akiongea anabakiza maneno kwa kuhofiwa kuumbuliwa.

Mbunge wa Muleba Kusini, Prof. Anna Tibaijuka akihojiwa wakati wa ziara ya Rais Magufuli kiwanda cha sukari Kagera, amesema hii itakuwa awamu yake ya mwisho kugombea ubunge na anang'atuka Kama msemo wa Mwalimu Nyerere.

Amesema ataendelea kuwepo kwenye jamii lakini ni wakati wa kuwaachia vijana.
Umenikumbusha Msekwa na Makinda, nashauri tuweke akiba ya maneno. 2020 hachelewi kurudi huyu na kusema wazee wamemuomba agombee kupitia Chadema!!
 
Back
Top Bottom