Mama Anna Mghwira, Mradi wa maji UBWS (Machame Mashariki) kuna ufisadi Mbowe kashindwa

Mleta mada ama unapotosha au Hujui miradi ya maji iliyopo. machame

Inawezekana hufahamu vyanzo vyake pamoja na mamlaka
Inayosimamia kila chanzo na usambazaji wake .
Freeman Mbowe ni mwakilishi tu ,wa wanchi , ,anayeongoza seikalia ni jamaa zako,

Lakini ninachofahamu IPO miradi mingi ya maji inapangwa na Kamati za maji baada ya mkutano na wanachi.

Kwa hiyo kama kuna maeneo wameweka Kampuni ya kusambaza maji na bei ya kuunganisha ni kubwa ni Halimashauri imeingia . Hata hivyo najua halimashauri haiwezi kupanga being pasipo kushirikisha wananchi kwenye miradi inayowahusu
Muhimu Eleza Freeman amehusikaje ? wakati wenye serikali unawajua !
 
Mleta mada inaonesha ni masikini wa kutupwa,unashindwa tsh.600000 then unaingiza siasa !?, huo mradi ni wa mbowe !?, inaonesha kichwani mwako umejaa mabonzo ya ulanzi badala ya akili
 
sioni Uhusika wa mbowe hapo maana siku hizi mkurugenzi ,mkuu wa wilaya,wanachama wa nyinyiemu wana amri kushinda baraza la madiwani na mbunge
 
Heshima yako mkuu ,

Sisi wakazi wa Mkoa wa kilimanjaro tumefarijika sana kukupata mama ,maana tuna imani na wamama katika kuzingatia matatizo ya jamii kwa dhati kabisa na kuyatafutia ufumbuzi ,hakuna mama atakayefurai kuona wanae wanateseka naamini unatumia muda wako mwingi kuhakikisha unabadilisha maisha ya wana kilimanjaro Hongera na mungu akutie nguvu, ujasiri na hekima.

Kwa kifupi kuna mradi wa maji unaitwa UBWS ambao uko kwenye kata ya Machame mashariki huu mradi umefika mpaka boma. tatizo la huu mradi ni gharama za kufunga maji ni kubwa sana mimi nataka kufunga maji hapa nyumbani nyuma ya nymba kuna mfereji mbele ya nyumba kuna mfereji umbali wa 200M kuna mfereji na umbali wa 400M kuna mto kifupi hamna shida ya maji lakini Bomba la maji ambalo lipo umbali wa 40M naambiwa gharama za kuunganisha haya maji safi ya bomba ni 600,000 hii ni haki kweli utafikiri tupo jangwani gharama za kufunga maji zinazidi za kufunga umeme .

Hawa watu wa huu mradi wanatuonea wanajilimbikizia hela tu wakati hata visima wameshindwa kujenga huko boma vya kutosha .tunaomba wachunguzwe watumbuliwe wameshazoea. juzi juzi nimeskia DAWASCO wanafungia wananchi maji kwa mkopo alafu gharama za kufunga maji DAWASCO sio kubwa kama hizi.

nitangulize shukurani zangu za dhati maana nina imani na uwajibikaji wa viongozi wa hi sirikali.
Malizia stori yako mbona kama haijaisha!!!!
 
Mleta mada inaonesha ni masikini wa kutupwa,unashindwa tsh.600000 then unaingiza siasa !?, huo mradi ni wa mbowe !?, inaonesha kichwani mwako umejaa mabonzo ya ulanzi badala ya akili
sawa tajiri wa kutupwa, nisaidie basi kulipia hayo maji
 
Nchi hii iko chini ya ccm toka kupata uhuru zaidi ya nusu karne na imeshindwa kupambana na hao maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na umasikini pamoja na ccm yenyewe kuwa sehemu ya maadui wa nchi hii na kufika wanne
hii inanisaidiaje mimi kupata maji
 
Mleta mada ama unapotosha au Hujui miradi ya maji iliyopo. machame

Inawezekana hufahamu vyanzo vyake pamoja na mamlaka
Inayosimamia kila chanzo na usambazaji wake .
Freeman Mbowe ni mwakilishi tu ,wa wanchi , ,anayeongoza seikalia ni jamaa zako,

Lakini ninachofahamu IPO miradi mingi ya maji inapangwa na Kamati za maji baada ya mkutano na wanachi.

Kwa hiyo kama kuna maeneo wameweka Kampuni ya kusambaza maji na bei ya kuunganisha ni kubwa ni Halimashauri imeingia . Hata hivyo najua halimashauri haiwezi kupanga being pasipo kushirikisha wananchi kwenye miradi inayowahusu
Muhimu Eleza Freeman amehusikaje ? wakati wenye serikali unawajua !

usirudie kusema tena sielewi miradi ya maji ya huku maana ndo naishi humu alafu sio miradi ni mradi mmoja tu ,na hakuna mwananchi anayekubali kulipia maji hela nyingi hivyo na mbowe ndo mtetezi wetu tumempigia kura yeye anaangalia tu hafanyi lolote
 
Mleta mada wewe unasema unaishj hapo ,mimi nimezaliwa ,nimekulia hapo na kuishi hapo zaidi ha miaka 20

Kuonyesha kusema mradi ni mmoja tu wa maji machame yote unakosea.
Pili ulitakiwa kueleza Freeman Mbunge amenyamazia je gharama za kuunganisha maji mpaka zimekuwa kubwa wakati mambo yote ya utawala yako na rangi ya kijani !

Huyu mama aliyepewa ulkuu umemtaja na kumsfia ili iweje ? Au ndo mpango wa kumpaka mtu matope ili ccm waliopanga bei washushe bei?.

Laikini nijuavyao maamuzi ni ya Halimashauri au Baraza LA madiwani na mkurugenzi baadaya ya mashauriano na kamati husika.

Eleeza alipozembea
 
nazungumzia kata ya machame magharibi mradi wa UBWS to be specific ......bei ya kufunga maji ni kubwa sana hata wakija watu wenye weledi wakachunguza huu mradi watagundua ufisadi mkubwa sana... mbowe nimempigia kura mimi lakini kwa hili la maji naona nilipoteza kura yangu kabisa
 
Back
Top Bottom