Mama Anna Malecela Nae Tumchunguze!

Mtimti

JF-Expert Member
Feb 23, 2008
942
644
watanzania sasa wamekuwa na matumaini sana na wabunge wao kwa ujasiri waliounesha bungeni kwa kuweka maslahi ya taifa mbele bila ya kujari itikadi ya vyama,lakini ni jambo la kusikitisha kama baadhi ya wabunge watakuwa wanafanya hivyo kwa sababu ya jazba au chuki binafsi.nasema hivi kwa sababu kuna ushahidi tosha kuwa mama malecela(anna kilango)alikuwa na ugomvi mkubwa na mama anna mkapa kiasi kwamba mama anna mkapa aliwahi kumlipoti kwa viongozi wa juu wa chama,na kisa cha ugomvi huo ni juu ya mama anna malecela alikuwa anamtambia mama mkapa kuwa zamu yake(mama malecela)first lady imefika na hivyo mama mkapa aaanze kufungafunga virago na kuondoa ofisi yake kabisaa kwenye maeneo ya ikulu.kwani mama malecela alikuwa anajua kuwa mumewe atakuwa mgombea wa urais kwa ticket ya CCM na hivyo kuwa RAIS.hivyo nasi tuwe makini ktk kuwashabikia hawa wabunge kwani wengi kwa sasa wanajifanya wanayaweka maslahi ya nchi mbele kwa sababu ya hasira zao,ina maana kipindi chote walichokaa kwenye bunge walikuwa wamefungwa midomo?tuendelee kuwamulika ili tuone kama wataendelea kukemea?au ndio wanajitengenezea mazingira ya kula vizuri?
 
Huu ndo umbeya wenyewe.

Kama anahasira au ana ghubu sisi hatujali ili mradi ameamua kusema yote yaliyo ya kweli mwache aseme.
Huo umbeya wa nani ni mke rais na nani ni mke wa kabwela huko huko kwenye mitaa ya mipasho.
 
mwenzenu anajitahidi kukata ishu bin kumkoma nyani mchana kweupeee nyie mnamshushua!!! LOL

mtimti,
karibu kaka kwenye kijiwe dume!! hearsay nyepesi nyepesi hapa si mahali pake!!.
 
watanzania sasa wamekuwa na matumaini sana na wabunge wao kwa ujasiri waliounesha bungeni kwa kuweka maslahi ya taifa mbele bila ya kujari itikadi ya vyama,lakini ni jambo la kusikitisha kama baadhi ya wabunge watakuwa wanafanya hivyo kwa sababu ya jazba au chuki binafsi.nasema hivi kwa sababu kuna ushahidi tosha kuwa mama malecela(anna kilango)alikuwa na ugomvi mkubwa na mama anna mkapa kiasi kwamba mama anna mkapa aliwahi kumlipoti kwa viongozi wa juu wa chama,na kisa cha ugomvi huo ni juu ya mama anna malecela alikuwa anamtambia mama mkapa kuwa zamu yake(mama malecela)first lady imefika na hivyo mama mkapa aaanze kufungafunga virago na kuondoa ofisi yake kabisaa kwenye maeneo ya ikulu.kwani mama malecela alikuwa anajua kuwa mumewe atakuwa mgombea wa urais kwa ticket ya CCM na hivyo kuwa RAIS.hivyo nasi tuwe makini ktk kuwashabikia hawa wabunge kwani wengi kwa sasa wanajifanya wanayaweka maslahi ya nchi mbele kwa sababu ya hasira zao,ina maana kipindi chote walichokaa kwenye bunge walikuwa wamefungwa midomo?tuendelee kuwamulika ili tuone kama wataendelea kukemea?au ndio wanajitengenezea mazingira ya kula vizuri?

Ndugu Mtimti, karibu sana JF.

Hoja zako ziwe na mantiki na uzito unaostahili kwa sababu tunajaribu kukwamua nchi kwa mijadala yenye utata. Hiyo mada inaonyesha unataka kila mtu aamini kuwa mama Kilango ana visa na mama Mkapa, na huangalii kama hata hoja za Kilango ni za kweli au la.

Unatutisha, Unataka watu waanze kuogopa kusema ukweli kwa kuwa nao wataumbuliwa? au una maana wenye matatizo hawana hali ya kuwasema wenzao, wanyamaze kimya hata kama wanaona nchi inateketea?

Kama walichoelezana ni mambo ya gubu, hayo ni yao, na hayafai kujadiliwa hapa. Wewe tuletee matatizo yanayoisibu nchi, na si kwa nini fulani asiseme matatizo hayo...

Ukijenga tabia ya thread za namna hiyo, ghafla itajenga imani kuwa wewe ni mmmoja wa watu waliotumwa kuja kusafisha majina ya wengine na kuchafua ya wengine...hiyo haitalisadia taifa letu.
 
watanzania sasa wamekuwa na matumaini sana na wabunge wao kwa ujasiri waliounesha bungeni kwa kuweka maslahi ya taifa mbele bila ya kujari itikadi ya vyama,lakini ni jambo la kusikitisha kama baadhi ya wabunge watakuwa wanafanya hivyo kwa sababu ya jazba au chuki binafsi.nasema hivi kwa sababu kuna ushahidi tosha kuwa mama malecela(anna kilango)alikuwa na ugomvi mkubwa na mama anna mkapa kiasi kwamba mama anna mkapa aliwahi kumlipoti kwa viongozi wa juu wa chama,na kisa cha ugomvi huo ni juu ya mama anna malecela alikuwa anamtambia mama mkapa kuwa zamu yake(mama malecela)first lady imefika na hivyo mama mkapa aaanze kufungafunga virago na kuondoa ofisi yake kabisaa kwenye maeneo ya ikulu.kwani mama malecela alikuwa anajua kuwa mumewe atakuwa mgombea wa urais kwa ticket ya CCM na hivyo kuwa RAIS.hivyo nasi tuwe makini ktk kuwashabikia hawa wabunge kwani wengi kwa sasa wanajifanya wanayaweka maslahi ya nchi mbele kwa sababu ya hasira zao,ina maana kipindi chote walichokaa kwenye bunge walikuwa wamefungwa midomo?tuendelee kuwamulika ili tuone kama wataendelea kukemea?au ndio wanajitengenezea mazingira ya kula vizuri?

Nadhani hasira za Mama Ann Malecela sisi watanzania ndiyo tunazozitaka, maana ameweka maslahi mbele ya taifa ...sasa mwenzet unataka kutuambia tuwe makini kwa lipi wakati mama anafanya yale yaliowashinda wengi....? Kama umekuja safisha mtu hapa ingia kwa style nyingine
 
mambo ya jikoni hayo ndugu yangu,habari ambazo hazina maslahi kwa taifa saa hizi hazina nafasi kabisa,watu tunafungua thread kumbe umeandika mipasho ya mwaka 2004,thibitisha basi ulikoitoa.

Tafadhali tuokoe muda kwa kukataa wazembe kama hawa,mipasho yao iliigharimu nchi kiasi gani tuambie basi!!!!!!!!
 
mtimti,tafadhali nenda kwenye mipasho km una beef na mama kilango
hapa si maala pake.kwani unalotupasha hapa halina uhusiano wa aina yoyote na yale ambayo mama kilango kayasema bungeni.akili tunazo na tunaweza kabisa kupima na kujua km ni mbege ama la.sasa wewe mtimti peleka hii hoja yako kwenye udaku.hivi wewe kweli umetokea wapi hasa!!!mtimti kweli mkavu huu na wala hauchimbwi dawa.
 
watanzania sasa wamekuwa na matumaini sana na wabunge wao kwa ujasiri waliounesha bungeni kwa kuweka maslahi ya taifa mbele bila ya kujari itikadi ya vyama,lakini ni jambo la kusikitisha kama baadhi ya wabunge watakuwa wanafanya hivyo kwa sababu ya jazba au chuki binafsi.nasema hivi kwa sababu kuna ushahidi tosha kuwa mama malecela(anna kilango)alikuwa na ugomvi mkubwa na mama anna mkapa kiasi kwamba mama anna mkapa aliwahi kumlipoti kwa viongozi wa juu wa chama,na kisa cha ugomvi huo ni juu ya mama anna malecela alikuwa anamtambia mama mkapa kuwa zamu yake(mama malecela)first lady imefika na hivyo mama mkapa aaanze kufungafunga virago na kuondoa ofisi yake kabisaa kwenye maeneo ya ikulu.kwani mama malecela alikuwa anajua kuwa mumewe atakuwa mgombea wa urais kwa ticket ya CCM na hivyo kuwa RAIS.hivyo nasi tuwe makini ktk kuwashabikia hawa wabunge kwani wengi kwa sasa wanajifanya wanayaweka maslahi ya nchi mbele kwa sababu ya hasira zao,ina maana kipindi chote walichokaa kwenye bunge walikuwa wamefungwa midomo?tuendelee kuwamulika ili tuone kama wataendelea kukemea?au ndio wanajitengenezea mazingira ya kula vizuri?

HALAFU baada ya hapo??
 
Bila shaka aliyeanzisha hii hoja ameishasikia na kuelewa...tunaongelea yaliyotokea 2008yeye anatuletea mambo ya 1995 na 2004. Kwa sasa hayatuhusu na huyu Mama Kilango alituonyesha kwamba yeye ni mzalendo yawe yalitokea sisi hayatuhusu. Kwa sasa tunacheza ngoma kwa kwenda mbele.

Basi chambueni yale mazuri aliyoyasema bungeni...hata kama ilikuwa ni hasira mbona yote yalikuwa mambo ya maana na yaliyotugusa wote...

Tunasonga mbele katika kupambana na mafisadi...na hii vita tutaishinda kwa kukemea vitendo vyote viovu na kwa njia ya amani kupitia vyombo vyote....

Mungu wabariki wabunge wote jasiri wanaokuwa imara kutetea maslahi ya Tanzania na si maslahi ya "Chama cha mafi...""

Onyo: Kabla ya kuleta umbea hapa fikiria mara ishirini basi...
 
naona kama tulivotarajia baada ya matatizo yaliyotupata last week kwamba member wangeongezeka mara dufu tunawakaribisha sana lakini hapa pana miila yake yakutozungumzia watu kwa hoja kama ya huyu bwana hapa zaidi tunapenda kutaja watu openly but tunakua tunajadili maswala huo umbea wa kitoto peleka kwenye magazeti ya udaku.

Other wise kama unajifunza kutoa hoja karibu sana lakini nenda kwa hatua kua makini lasivyo utaichukia JF
 
Huu ndo umbeya wenyewe.

Kama anahasira au ana ghubu sisi hatujali ili mradi ameamua kusema yote yaliyo ya kweli mwache aseme.
Huo umbeya wa nani ni mke rais na nani ni mke wa kabwela huko huko kwenye mitaa ya mipasho.

Sidhani kama huu ni umbeya hata kidogo. Kiukweli sote tumefurahishwa na hatua ndogo (hii ni kwa mujibu wangu mwenyewe) iliyopigwa mathalan ktk bunge lililopita na ktk mambo ya Richmond, Mh.Lowassa kujiuzulu, EPA etc..

Lakini hasa nimeguswa na munkari wa ghafla uliojitokeza haswa kwa wabunge wa kutoka chama kitukufu cha CCM..Kiufupi ni kuwa grafu ya 'uzalendo' imepanda kwa ghafla sana kiasi cha kutisha, na hivyo kuibua maswali muhimu kama Je, maovu na ulaji serikalini na uzembe umeanza hivi majuzi tuu? Je munkari wa uzalendo upo to stay au ni kiini macho? Je hakuna 'sababu' ya ziada kuhusu 'ari' hii mpya ya 'uzalendo' miongoni mwa wabunge ambao kikawaida nyendo na misimamo yao inaenda ikibadilikabadilika?

Let us ponder this one..
 
Mtindiowaubongo,

Hapa tunachokipigania ni mabadiliko ya wanasiasa wetu ili walete maisha bora kwa waTanzania. Sasa kama watu kama akina Kilango, Selelii wanabadilika, je, si tutakuwa wa ajabu tukianza kuhoji kasi yao ya mabadiliko? Ulitaka graph ipande pole pole, halafu iweje?

Alichokisema Kilango ni uongo? Mbona tunaanza kujikana wenyewe sasa? Kama kila hoja atoayo mtu haitasikilizwa, na badala yake anaanza kuchambuliwa mtu aliyeitoa hoja, tutasikiliza nini na toka kwa nani? Sasa Nchi hii hatimaye si itakuwa ya wanafiki tu sasa?
 
Mkuu, tusisahau kuwa hawa wote ni wanasiasa na hivyo wanatakiwa kufanya kile kitachowapa umaarufu kwa wapiga kura. Hiyo sio dhambi. Kuna watu walimponda Obama lakini walipoona mambo yanavyoenda wamegeuka na kumuunga mkono. Ndiyo siasa. Huyu mama inawezekana kabisa kuwa ameona namna ya yeye kutambulika na kukubalika katika jamii ni kuwa mstari wa mbele katika kuonyesha uzalendo wake. Hii ni haki yake na hakuna anayeweza kumlaumu kwa hili. Sasa kama anafanya hivi ili kuficha maovu yake hapo atastahili kukemewa. Aliyeleta mada hii hakuonyesha maovu yeyote isipokuwa kuwa alimtambia mwenzake kuwa zamu yake imefika. Hili ndilo tunalopinga na kusema kuwa ni umbeya. Hatuwezi hata siku moja kumhukumu huyu mama kwa hilo. Itakuwa ni kumuonea. huyu mama ahukumiwe kwa vitendo vyake ambavyo kwa upande wangu naona anastahili pongezi kwa kuwa muwazi na mkweli. Kama ndiyo anajijenga ili awe rais wa kwanza mwanamke,au anamfagilia mume wake, sioni tatizo lolote. Walio na busara kuliko mimi walisema,"ili mradi paka anakamata panya, hatutojali rangi yake".
 
Sawa ndugu Mbalamwezi,

Mama Kilango na wenzake kusema ukweli au la, I'm not the one to determine. Suala la msingi ni timing ya waliyoyafanya na motive (s) behind it..Sijui kama uliielewa posting #1.

Binafsi mimi sio myopic kiasi cha kutaka kuamini kirahisirahisi na wala siamini ktk sanaa inayoendelea hivi sasa ya grafu ya 'uzalendo' kupanda exponentially. Najua kuna watanzania wenzangu ambao ni wepesi sana kushawishika na usanii mdogo tu kama huu tulioushuhudia..siwalaumu kwa hilo..

Sisi wanasayansi tunapofanya observation ya variable fulani with time, halafu variable ikapanda kwa ghafla saaana kutoka mamoja mpaka mamilioni, huwa tunakaa chini na kutrace source(s) of such an incredible trend..

Thats is important than the graph itself..
 
Mkuu, tusisahau kuwa hawa wote ni wanasiasa na hivyo wanatakiwa kufanya kile kitachowapa umaarufu kwa wapiga kura. Hiyo sio dhambi. Kuna watu walimponda Obama lakini walipoona mambo yanavyoenda wamegeuka na kumuunga mkono. Ndiyo siasa. Huyu mama inawezekana kabisa kuwa ameona namna ya yeye kutambulika na kukubalika katika jamii ni kuwa mstari wa mbele katika kuonyesha uzalendo wake. Hii ni haki yake na hakuna anayeweza kumlaumu kwa hili. Sasa kama anafanya hivi ili kuficha maovu yake hapo atastahili kukemewa. Aliyeleta mada hii hakuonyesha maovu yeyote isipokuwa kuwa alimtambia mwenzake kuwa zamu yake imefika. Hili ndilo tunalopinga na kusema kuwa ni umbeya. Hatuwezi hata siku moja kumhukumu huyu mama kwa hilo. Itakuwa ni kumuonea. huyu mama ahukumiwe kwa vitendo vyake ambavyo kwa upande wangu naona anastahili pongezi kwa kuwa muwazi na mkweli. Kama ndiyo anajijenga ili awe rais wa kwanza mwanamke,au anamfagilia mume wake, sioni tatizo lolote. Walio na busara kuliko mimi walisema,"ili mradi paka anakamata panya, hatutojali rangi yake".

Shukrani kwa mchango wako:

Mimi binafsi sipingi manouvres za wanasiasa as long as recipient wa effects zake si mlalahoi. Suala la upotevu wa pesa halihitaji political manouvres ,it is a criminal offence..Kama mtu atajipatia umaarufu down the process si kosa..hapo nafikiri tunakubaliana..Hilo la kwanza.

Nafikiri kwa kiasi kikubwa kazi ya kamati ya Dr. Mwakyembe haikuwa ya kisiasa na ndio maana watu tupo sensitive nayo na mapendekezo yake yapo wazi na si ya kisiasa. Kwa maoni yangu mpaka sasa kazi ya kamati na efficiency yake haijafikia hata 30% kwani pesa haijarudishwa, mkataba haujavunjwa, wahusika hawajaitwa hata polisi kutoa maelezo ya awali..n.k.

Mfano wako wa paka kukamata panya haujaumalizia vizuri, ni hivi: Suala la kuzingatia hapo ni kuwa baada ya huyo paka kumkamata panya anamfanyaje? Je anachanachana vipandevipande na kumtupa 'nje' kwenye kilio na kusaga meno? Au 'panya' na wafuasi wake wanatukuzwa na kutungiwa mapambio kuwa 'wameiva kisiasa' kwa kujiuzulu? etc Kwa jinsi 'panya' (au 'mapanya') (w)alivyokamatwa majuzi inaonekana dhahiri kuwa kuna kila dalili 'mapanya' wakapewa gunia jingine la wananchi, tena nono zaidi siku za usoni wazidi kulitoboatoboa. Na vilevile 'paka' wetu hajaonyesha mkakati wake wa kudumu kuwashughulikia mapanya wote waharibifu na kuwa na clear cut consistence..

Suala la kupima motive(s) behind any move si suala la mzaha au la kulipuuza. Motives za mwanasiasa ni muhimu kuliko hata modality anayoihubiri..
 
Hakuna mtu anayekataza kuangalia motive za wahusika. Tunachopinga ni hili suala la kusema kuwa huyu mama anafanya hivi kwa vile alimtambia mwenzake!

Hiyo ya panya, cha msingi ni kuwa panya amekuwa si tatizo tena. Atakayofanya paka baada ya hapo ni ishu nyingine lakini haiondoi ukweli kuwa alimkamata panya. Huyu panya tuliyemuona tatizo tutaanzaje tena kumuimbia pambio? Watakaofanya hivyo si watakuwa mapanya wengine? Dawa si itakuwa kutafuta paka wengine na kujumuisha nguvu zao kuwashughulikia badala ya kuanza kusema kuwa ati wewe kwa sababu ni paka wa kijani hatukuhitaji? Awe wa kijani au bluu apimwe kwa uwezo wake wa kumshughulikia panya na si vinginevyo.
 
Sasa una maana kwamba aliyosema ni ya uongo? Muhimu amesema mambo ambayo yapo na ametumia jukwaa sahihi. acha kutumiwa na hao mafisadi, nilazima tuwe macho, mbona tukisismama pamoja tutafanikiwa kuwaondoa, TUWE MAKINI!!!!!!!!!!
 
Suala si kasema uongo au la! Hata kama ni kweli, umuhimu wake katika kupima credibility ya huyu mama uko wapi? Au unataka kutuambia kuwa kutambiana nako kumekuwa UFISADI? Kwa jinsi mnavyolitumia neno hili, mnaondoa uzito na ukali wake!
 
Hiyo ya panya, cha msingi ni kuwa panya amekuwa si tatizo tena. Atakayofanya paka baada ya hapo ni ishu nyingine lakini haiondoi ukweli kuwa alimkamata panya. Huyu panya tuliyemuona tatizo tutaanzaje tena kumuimbia pambio? Watakaofanya hivyo si watakuwa mapanya wengine? Dawa si itakuwa kutafuta paka wengine na kujumuisha nguvu zao kuwashughulikia badala ya kuanza kusema kuwa ati wewe kwa sababu ni paka wa kijani hatukuhitaji? Awe wa kijani au bluu apimwe kwa uwezo wake wa kumshughulikia panya na si vinginevyo...

Paka anatakiwa awe paka tu iwe ni jana, leo au kesho..Lakini ktk hili inaonekana hawa 'paka' tulionao leo walikuwa usingizini huko nyuma tena usingizi wa pono..Hili linanistusha..

Labda niseme pia kuwa 'mapanya' wamesha sio wata-imbiwa mapambio ya kuwasifu kwa kujiuzulu kishujaa! Mimi ningeomba tu tukubaliane kuwa 'mapaka' wetu lazima vilevile tuwascrutinize kwani isije ikawa kiundani ni 'mapanya' ila wamekwaruzana na 'mapanya' waliopo kwenye kikaangio na serikalini kwa sababu ambazo sio valid. Hoja hapa ni kwamba kama hawakuwa na sababu valid pindi tutakapowapa uaminifu wetu watatutenda mabaya zaidi kuliko hata 'panya' wa mwanzo..
 
Back
Top Bottom