Mama anayejiuza (Mhaya) anaomba msaada wa kusomeshewa mtoto

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
Leo nilikuwa nasikiliza kipindi cha "Njia Panda" cha Clouds Fm, Dr Maro alikuwa anamuhoji mama mmoja wa Kihaya ambaye amefanya kazi ya kuuza "Papuchi" kwa zaidi ya miaka 25. Kazi hiyo alianzia mkoani Morogoro na baadae kuhamia DSM na kuendelea na kuuza huduma hiyo.

Wakati akiwa Morogoro akitoa huduma kama miaka 23 iliyopita, alijikuta kapata mimba bila kujua baba wa mtoto, sababu kwa siku alikuwa anahudumia wanaumekadhaa.Mapaka anapata mimba hakujua ni nani mwenye ile mimba maana anasema kuna watu alikuwa anawapa kwa kondomu, wengine kondomu zinapasuka na wengine kavukavu kutokana na dau wanalompa .Aliendelea na biashara hiyo hadi alipokuwa na ujauzito wa huyu binti yake ambaye sasa ana miaka 23.

Baadae watu wa kanisa la "Jeshi la Wokovu" walimchukua mtoto wake na kumsomesha elimu ya msingi, na alifaulu vizuri kwenda kidato cha kwanza, lakini kutokana na ukata wa Jeshi la Wokovu wakasitisha msaada, binti akawa nae kakatisha ndoto zake maana mama hana uwezo wa kumsomesha.

Ukimsikiliza binti radion anaonekana"mjanja mjanja" sana, ana uwezo wa kujieleza na kujibu maswali kwa ufasaha, binti amekuwa na kugundua kuwa wanaishi na mama yake kwa pesa za kujiuza, yaani huona mama anavyoingiza wanaume ndani na "kushughulikiwa".

Hali hii inamuumiza lakini hawezi kumkataza mama yake, maana mama humwambia hiyo ndio kazi iliyofanya yeye akapatikana na ndio iliyomkuza. Binti anaumia sababu mpaka leo hamjui baba yake na mama hajui baba wa mtoto as alipatikana kwa "short time".

Baada ya kuambiwa ukweli na mama yake jinsi alivyopatikana binti ameumia sana, maana hajui baba wala shangazi zake wa kuumpa msaada, leo anaomba msaada wa kusomeshwa maana anasema mama yake sasa ana miaka 48 na hawezi tena kuendelea na biashara hiyo maana ndio anazeeka na "wateja" wanapungua.Mama huyu ni Muhaya wa Kagera.

Binti anaomba msaada wa kuendelezwa kimasomo,a na ndoto za kuwa "Air hostess" maana ni kazi ambayo amekuwa akiipenda, anajisikia vibaya mama yake kumtoa nje ya chumba ili aingize wanaume, majirani wachache na watoto jirani wanaojuwa "kazi" ya mama yake wamekuwa wakimcheka na kumdhihaki.

Hana raha awapo mtaani, rafiki zake aliosoma nao "Jeshi la Wokovu" sasa wapo vyuo vikuu au katika taasisi mbalimbali za elimu, na yeye angependa kufikia hatua hiyo, ili asitumbukie kwenye "kazi" ya Mama yake.

Wadau, wanaharaki wa makundi maalumu, haki za wanawake na watoto na mashirika binafsi mnaweza kujitokeza ila kumsaidia binti huyu ambaye kWanza ameathirika sana kwa kugundua kuwa alipatikana kwa mama yake kujiuza kwa "shot time" hivyo haujui ukoo wake, lakini pia tabia ya mama yake kuendelea kujiuza ndani ya chumba ambacho wanaishi wote.

Wadau wa MMU, kuna namna ya kumshauri na kusaidia jambo hili? Kweli duniani kuna mengi, hii habari nimeisikiliza ikanifikirisha mambo mengi sana.

ASANTENI...NAWASILISHA
 
Kauza kwa zaidi ya miaka 25?

Mbona mi sijawahi kuona mama [mwenye umri mkubwa] poa....wengi niwaonao ni wadada.

Hao wamama poa huwa wanategesha pande zipi?

Ila hiyo makitu yake itakuwa imetumika hadi imeota sugu!
 
Inaumiza sana. Hasa binti anapoona mama yake akiingiza wanaume ndani. Kituo cha KIWOHEDE wakisikia watampa msaada. Lakini pia mwenyekiti wa mtaa anapoishi huyo mama naona hayupo vizuri. Hii issue ingeanzia kwake mpaka wilayani sidhani kama ingeshindikana na kufikia kwenye radio.
 
Kauza kwa zaidi ya miaka 25?

Mbona mi sijawahi kuona mama [mwenye umri mkubwa] poa....wengi niwaonao ni wadada.

Hao wamama poa huwa wanategesha pande zipi?

Ila hiyo makitu yake itakuwa imetumika hadi imeota sugu!
Milleage ya hio kitu Ni balaa
 
Kauza kwa zaidi ya miaka 25?

Mbona mi sijawahi kuona mama [mwenye umri mkubwa] poa....wengi niwaonao ni wadada.

Hao wamama poa huwa wanategesha pande zipi?

Ila hiyo makitu yake itakuwa imetumika hadi imeota sugu!

Mkuu uko dunia ipi? Ukitaka Ingini ya chombo chako kudumu lazima uifanyie sefisi mara kwa mara na kwa wakati!
 
Ndio maana ni muhimu magu arasimishe hii biashara ili wakatwe kodi na ppf. Angekuwa na pensheni saa hizi khaa
 
Huyo mama aende kwa rugemalila atasaidiwa kma aliweza kumpa judge 200m pole ya msiba...huyo mama hawezi kukosa kupewa 30m ya kuuza maandazi
 
Maisha ni wewe unachugua yawe vp coz uyu mama akuzaliwa anajiuza aliamua kutaweka vile xaxa mtoto wake anapata shida
 
Back
Top Bottom