Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla...! SEHEMU YA MWISHO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla...! SEHEMU YA MWISHO

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, May 22, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280

  View attachment 54352
  Picha hii haihusiani na habari hii.........



  Nilipelekwa hospitlini na wale wanakijiji. Dada na wanae hawakujali kabisa. Kale kabinti kake ka mwisho yaani Msekwa, kalilia sana kalipoona nimeunguzwa. Nakumbuka nilipolazwa hospitalini ndiko pekee kutoka nyumba ile kalikokuja kunitazama.

  Nililazwa hospitalini kwa wiki mbili na wale wanakijiji walionipeleka hospitalini ndio waliochangishana na kunilipia gharama za kukaa hapo hospitalini. Nilitoka nikiwa na nafuu kubwa, ingawa shavu langu lilikuwa na alama kubwa ya kuunguzwa kule. Hata hivyo nilijua kwamba, hata baada ya kupona ningebaki na kovu hilo mileleNilipotoka hospitalini sikuweza kurejea kule kwa dada yangu na wale wanakijiji walionisaidia pia waliogopa kunipokea. Waliogopa kwa sababu dada yangu alikuwa akiwatisha kwamba nikifa watanila nyama. Ilibidi nifikirie namna mpya ya kuishi. Kumbuka wakati ule, tena vijijini, watu hawakuwa wanjua kitu kinachoitwa haki za binadamu, achilia mbali haki za mtoto. Watu walikuwa waoga kuingilia mambo ya familia za watu, hata kama mtu anakufa.

  Unajua ni kwa nini nimekuuliza kuhusu maono? Ni hivi. Saiku ile nilipotoka hospitalini nililazimika kwenda kwenye mashamba yampunga ambapo niliomba kibarua cha kufukuza ndege kwa wenye mashamba hayo. Nakumbuka watoto wengi na watu wazima walikuwa wakifanya kibarua hicho. Kwa bahati nzuri mama mmoja aliniambia angenisaidia lakini malipo yangu ningepata baada ya mavuno. Aliniambia ningekula na kulala kwake hapo hapo shambani. Niliona kama vile nimepata dhahabu. Nilikubaliana naye.

  Ilikuwa ni usiku wakati nikiwa bado sijapata usingizi vizuri, nilipokiona kitu hicho. Hapo kwenye kibanda cha shambani nilimokuwa, niliona kitu kama kivuli kidogo. Kivuli hicho kililkuwa mbele yangu. Kwa sababu ya giza sikujua kama ni kivuli cha mtu au hapana.

  Niliogopa kupindukia na nilikuwa natetemeka pale kwenye godoro la sufi nilipokuwa nimelala. Halafu nilisikia kama sauti, ambayo sikujua kama inatoka kichwani mwangu au kwenye kile kivuli. Ilikuwa ikisema 'Muone tu mama mkubwa, ni lazima usome, ile sauti ilirudia tena na tena. Ilikuwa ni sauti niliyokuwa ninaifahamu.

  Ilizidi kunisisitiza tena na tena. Nilishindwa kuvumilia ambapo nilipiga yowe kubwa na kuamka. Nilipapasa hapo chini na kuchukua kiberiti. Niliwasha kibatari huku mikono yangu ikitetemeka. Nilitazama mle kibandani na sikuona kitu. Nilikumbuka sauti ile kwa mbali sana. Ilikuw ni sauti ya mama yangu au mdogo wangu, sikuwa na uhakika sana.

  Nilianza kufikiria kuhusu huyo mama mkubwa. Mimi sikuwa na mama mkubwa, sasa ni mama mkubwa yupi ambaye huenda sauti zile zilikuwa zikinielekeza kwake. Nilijiuliza karibu usiku mzima. Hatimaye kwa njia fulani ya ajabu nilikumbuka kwamba, wakati nikiwa nimelazwa pale hospitalini Bwagala, kulikuwa na watu waliokuwa wakimtaja mtu aliyeitwa mama mkubwa, ambaye wengine walisema ndiye mwenye hospitali ile.

  Nilichukuliwa na usingizi kwenye saa kumi na nilishtushwa na mama mwenye shamba. Alikuwa akiniita huku akitukana kwani mpunga ulikuwa unashambuliwa na ndege. Nilitoka kibandani kwa kasi na kukutana naye mlangoni. ‘Samahani mama nimechelewa kuamka…'Hakusubiri nimalize kwani alinitaka niondoke pale shambani kwake saa ile ile. Niliondoka bila kuhitaji kujitetea, labda nilishazoeshwa kuishi kwa amri.Nilitembea asubuhi hiyo hadi hospitalini. Nilikwenda upande wa utawala na kuomba nimwone mama mkubwa. Ilikuwa ni vigumu sana kwa sababu ya watu ambao siku hizi wanitwa ‘wapambe' Walikuwa wananizuia kwa maelezo kwamba mama mkubwa haonwi hovyo tu. Wakati tunabishana, kwani nami nilikuwa mkali nikiwa sijui nilitoa wapi nguvu hiyo ya kubishana, alitokea mamammoja mzungu aliuliz kulikoni, ambap walimweleza. Alinisogelea na kuniambia nimweleze shida yangu. Sikumwambia kuwa niliota kuhusu mama mkubwa bali nilimsimulia kwa kifupi madhila yangu na kumwambia nilikuwa nataka msaada w kusoma.Alinisikiliza sana na baadae alisemaangepanga nionane na huyo mama mkubwa. Saambili baadae nilikuwa ofisini kwa mama mkubwa. Alikuwa ni mama wa kizungu mtu mzima sana, lakini mjanja na msikivu sana. Nilizungumza naye kwa kirefu nikimweleza kia kitu. Alishindwa kuvumilia kwani alimwaga chozi.Hapo nikafanikiwa kupata mfadhili wa kunisaidia kusoma. Nilikwenda shuleni na kuendelea na masomo.

  Nilikuwa ninaishi chini ya uangalizi wa mzee mmoja aliyekuwa anaitwa Alois, ambaye nimeambiw ameshafariki. Nilikuwa nikiishi kwenye chumba kimoja karibu na wodi ya wagonjwa hapo hospitalini. Wale ambao bado wapo hospitalini pale kama watumishi wanakumbuka, bila shaka. Nilimaliza darasa la saba na kuanguka kwa njia ambayo bado ni mshangao kwangu, hadi leo. Mama mkubwa alisikitika sana. Alimwomba Mzee Alois anitafutie shule nirudie. Nilirudia shule nyingine ya jirani. Mwaka mwaka uliofuatia nilifaulu peke yangu shuleni hapo.

  Niliendelea na masomo. Bila shaka huhitaji kujua habari za shule ya sekondari. Lakini nilimaliza kidato cha sita mwaka 1987 na kumaliza masomo ya chuo kikuu nchini Uholanzi mwaka 1992. Nilirudi nchini na kuanza kazim kwenye kampuni9 moja ya madini kule shinyanga.

  Mwaka 1994 nilikwenda Turiani, lengo likiw ni kwasalimu wote ambao nilikuw nafahamiana nao pamoja na dada yangu. Kwa kweli nilikuw nimemsamehe dada yangu yule kutoka ndani kabisa ya moyo wangu. Niliamua kwa makusudi niende nikashukie kwake. Nilipofika pale nyumbani kwake kulikuwa na mabadiliko sana. Ile nyumba ilikuwa imechakaa karibu kuanguka na palionyesha ukiwa wa wazi. Nilibisha hodi na mama mmoja mtu mzima sana alifumgua mlango kutokea ndania na kusimama mlangoni.

  Kwa muda sikuweza kumjua. Lakini htimaye nilijua kuwa ni dada yangu.
  ‘Dada shikamoo, habari za siku' nilimsalimia, lakini yule mama pale mlangoni alishindwa kujibu na kwa muda fulani ilionekana kama vile hakuwa anajua kinachoendelea. ‘Marahaba' Alijibu, lakini ilikuwa ni kwa mazoea tu. ‘Nani mwenzangu, maana na huu uzee nao,' Alisema akijichekesha.


  ‘Ni mimi Joseph, mdogo wako Joseph, mtoto wa mzee Richard Mbega wa Sindeni.' Nilisema kwa kumfafanulia. Nilimwona dada akijishika vizuri pale mlangoni, lakini hakuweza. Alienda chini pole pole na kukaa kati kati ya mlango. Kw muda fulani nilijua alikuwa hajui alipo na kinachoendelea.

  Wakati nikiwa najiuliza nifanye nini mama mwingine aliingia kutokea huko nyuma ya nyumba. Nilimtazama lakini sikumfahamu. Yeye alipiga kelele. ‘Kaka Jose jamani, kaka Jose,wala siamini…….' Ilikuwa zamu yangu kushngaana laijua hilo kwani aliniambia, ‘Ni mimi mpwa wako Msekwa.' Nilihisi kitu kikilipuka huko moyoni na matumbo yangu yalishikw na kubana ghafla.

  Msekwa, alikuwa ni mama mzima, amechakaa na kuchoka kabisa. Kati yetu, yeye angeonekana kuwa mkubwa sana kuliko mimi. ‘Mungu wangu nashukuru nimekukuta…'
  Halafu tulimsikia dada yangu akipiga yowe la kilio akidai kwamba hakuwa anajua alichokuwa anakifanya. Akiwa anaongea Kizigua alisema, ‘Mungu wangu mie nifanyeje sasa, naumbuka ….' Nilimbembeleza, ingawa Msekw alisema nimwache augulie kwa sababu anastahili.


  Baada ya kupumzika, nilijua kwamba wale wapwa zangu watatu wengine, aliyekuwa hai ni mmoja tu wa kike. Mmoja alifariki kwa kuajribu kutoa ujauzito na yule wa kiume alikuwa amefariki kwa kunywa sana pombe. Huyu mwingine alikuwa ameolewa na kuachwa na alikuwa eneo linaloitwa Dakawa. Nilikaa Turiani siku tatu na nilimwomba Msekwa tuondoke wote aje Dar ajifunze kozi yoyote. Hapa ninaposimulia makala haya, ni muuguzi siku nyingi. Dada yangu alikataa katakata kuja kwangu kwa aibu.

  Inasikitisha hata hivyo kwamba, miezi mitatu tu tangu nilipofika kwake alifariki.Wanasema kila wakati alikuwa akijilaumu kwa yale aliyokuw amenitendeana alianza kujiambia kwamba, hana sababu ya kuishi kwa sababu hana maana. Naamini tunapanda nguvu hasi na huja kuturudia wenyewe.

  Tulienda kuzika na kurejea Dar. Juhudi yangu yote ilikuwa ni kumpata yule shemeji yangu, iwe yuko hai au kaburi lake lilipo ili angalau nilijengee kama zawadi yangu kwake. Lakini juhudi zangu ziligonga ukuta kwa kadiri nilivyojitahidi. Nilikwenda hadi TPC, Moshi lakini sikumpata.

  Hata hivyo hatimaye nilimpata katika mazingira ambayo sitaweza kuyasimulia hapa.
  Naamini kwa simulizi hii, kuna jambo ambalo umejifunza. Katika maisha haya tunayoishi ni vyema tukawa tunapanda mbegu chanya na sio hasi, kwani kwa kupanda kwetu mbegu hasi, ndio hatimaye huturudia mara tatu zaidi ya kile tulichopanda na maumivu yake kihisia huwa ni makubwa sana. Lakini kama tukipanda mbegu chanya, hakika mavuno yake huwa makubwa kuliko kawaida, hebu jaribu uone.
  Jambo lingine ni kusamehe, kusamehe ni muhimu kwetu, hata kama utakuwa umefanyiwa jambo baya kiasi gani. Kwa kusamehe kwetu tunakuwa tumejipa nafuu dhidi ya maumivu ya kihisia pale tukumbukapo juu ya yale tuliyotendewa na wenzetu. Zipo faida nyingi sana tunazopata pale tunaposamehe, lakini kubwa zaidi ni kule kumudu kusahau yale tuliyotendewa na hivyo kuwaza mambo mazuri ya yenye tija katika maisha yetu, badala ya kufikiria mabaya au kulipiza kisasi dhidi wale waliotutendea kinyume na matarajio yetu.


  *******MWISHO********

  Sehemu ya kwanza ya habari hii, bofya hapa:
  Mama anauawa kisha unashuhudia njia ya maisha yako inapofungwa ghafla.............!



  Ndugu wana JF, habari hii hainihusu mimi MTAMBUZI, bali iliwahi kuandikwa katika gazeti la Jitambue. Hii ni habari ya kweli kabisa ambayo ilimpata msomaji wa gazeti la Jitambue, ambapo kwa hiyari yake aliamua kuiweka habari ya maisha yake katika gazeti hilo ili wasomaji wapate kujifunza kupitia uzoefu wake.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sasa kwanini hujaziunganisha?

  Nwy hayo ni mambo yanayowakuta watu kila siku. . .na wakuumbuka wanaumbuka si kidogo.
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Mhh siyo mchezo. Kufa kufaana.
   
 4. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Asante Mtambuzi kwa uzi mzuri. Ni kweli tunatakiwa kupanda mbegu chanya na kuwa na roho za kiungwana na kuwajali wenzetu. Tuko duniani, na yule tunayemuona leo yuko hivi au uwezo wako uko chini, kesho anaweza kubadilika akawa mtu tofauti kabisa na wa msaada katika maisha yako. Ni vyema tupendane na kutendeana mema.

  Thanks Mtambuzi.
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  May 22, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Lizzy nilitaka kufanya hivyo, lakini nikaona ingekuwa ndefu sana...........................
  Nadhani kwa kufanya hivi, nitawapa wavivu kama kina fazaa wasome kwa utulivu huku wakinywa chai na mkate wa Boflo.........................................
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  daaah huo ndio ukristo wa kweli
   
 7. TaiJike

  TaiJike JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2012
  Joined: Dec 14, 2011
  Messages: 1,475
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Mhh..malipo ni hapahapa duniani, kile usichopenda wewe kutendewa usimtende mwenzio.
   
 8. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hahaha utani pembeni mimi ni mvivu sana wa kusoma line zikisha zidi 10 au kuandika line 10, nilipokuwa collage kuna instructor mmoja alikuwa hapendezewi kabisa nikiwa nandika assignments zangu in short akawa ananipa B tu, badala A au A+ mpaa kuna siku nikamueleza are you looking for quantity or quality, akasema quality, nikamuambia mimi naona wewe unatazama quantity zaidi kuliko quality, nda akanza kunipa A+:biggrin:
   
 9. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mtambuzi kuna siku na ww utatambuliwa
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Duh!mpaka nimeshindwa kula lol!inasikitisha na kufundisha,
  Km vp wape wataalam wa kuandika script maana ni story nzuri inayoweza tengenezwa bonge la movie!!!
   
 11. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #11
  May 22, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Cantalisia Nimesha-andaa script tayari, bado natafuta Casting kwa ajili ya shooting..................
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #12
  May 22, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mbona hujanitonya kama unavibwagizo katikati ya wiki?
   
 13. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Nikikosekana humo hiyo movie haitafanyika walahhh baba!
   
 14. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Teh teh teh jamani nimecheka !
   
 15. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  Mwenzangu ! Mtambuzi AMECHAKACHUWA ! .... well done mtambuzi , story nzuri sana sana ! inasikitisha ila mwisho wake ni mzuri sana ispokuwa sijapata picha BABA YAKE ! aliishia wapi? na huyu shemeji ?
   
 16. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #16
  May 22, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  mkomatembo........ Baba hajulikani alipo mpaka leo, lakini katika hitimisho, Joseph alimuona shemeji yake katika mazingira ambayo hakuyasimulia.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  May 22, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Cantalisia .....Wewe utacheza kama MSEKWA
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #18
  May 22, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  NATA sikutaka usome hii habari kwani nilihisi ungelia kwa huzuni...............!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. bulldoza

  bulldoza Senior Member

  #19
  May 22, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli hili ni darasa.
   
 20. zimwimtu

  zimwimtu JF-Expert Member

  #20
  May 22, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 1,889
  Likes Received: 621
  Trophy Points: 280
  I salute you mtambuzi, asante sana
   
Loading...