Mama anapokiri kumshindwa mtoto aliyemzaa mwenyewe….! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama anapokiri kumshindwa mtoto aliyemzaa mwenyewe….!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Feb 23, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Kuna kesi moja iliwahi kuripotiwa nchini Marekani, Novemba 1996, inayomhusu mama mmoja aliyeshitakiwa kosa la uzembe na utesaji wa mtoto wake wa kike aliyekuwa na umri wa miaka 13, aliyefariki ghafla kwa sababu ya unene. Baada ya mwili wa binti yule kuchunguzwa na madaktari, ilikuja kujulikana kuwa, mafuta yalijaa kwenye moyo na hivyo kupelekea moyo kusimama ghafla na kusababisha kifo chake. Huyo binti ambaye alijulikana kwa jina la Christina Corrigan, akiwa na umri wa miaka 13 wakati huo wa kifo chake alikuwa na uzito wa kilo 308 na walipopima mzingo wa paja lake lilikuwa na ukubwa wa sentimita 127. Mama yake ambaye naye alikuwa na tatizo la unene, alipoulizwa kuhusiana na namna alivyokuwa anamlea mwanaye, alisema kuwa mwanaye alikuwa na tabia ya kupenda kula kupita kiasi tangu akiwa mtoto.

  Aliendelea kusema, kila alipojaribu kumdhibiti au kumshauri ampeleke hospitali, mwanaye huyo alikuwa mkali na alikuwa anavunjavunja vitu hapo nyumbani kwa hasira, kwani pia alikuwa na tatizo la hasira za ziada zinazohusisha uharibifu (tantrum), hivyo akaamua kumuacha kama alivyo na tabia hiyo ya kupenda kulakula. Mwanaye aliongezeka unene ghafla na kufikia hatua ya kushindwa kutembea na hivyo akawa anajisaidia haja zote hapo hapo alipolala na hata shuleni pia alishindwa kuhudhuria. Kesi hiyo ambayo ilivuta hisia za watu wengi nchini Marekani ilikuwa ndiyo ya kwanza kutokea nchini humo, na hivyo kila mtu alikuwa akitoa maoni yake. Wapo waliomlaumu mzazi, wapo waliolaumu uongozi wa shule aliyokuwa akisoma yule binti kwa kutochukua hatua zozote baada ya kuto-onekana shuleni, kitu ambacho labda kingesababisha kuokoa maisha ya binti yule. Pia wapo wengine walilaumu taasisi za kijamii kwa kushindwa kuchukua hatua za kumsaidia mama wa binti aliyejulikana kwa jina la Marlin Corrigan, hata baada ya kupelekewa taarifa ya tatizo la binti huyo na mzazi wake.

  Mshitakiwa alikuwa akitetewa na wakili aliyewekwa na Taasisi ya kutetea haki za Watu Wanene ya nchini humo. Wakili huyo Bwana Michael Cardoza, akitoa taarifa za kitaalamu alisema kuwa marehemu alikuwa akikabiliwa na tatizo la kizalia (genetic) linalohusiana na kichocheo kinachotoa taarifa ya mtu kujisikia kushiba wakati anapokuwa anakula, kushindwa kufanya kazi. Kitaalamu hali hiyo hufahamika kama Prader-Will Syndrome (PWS). Muathirika wa tatizo hili hujisikia kula wakati wote na anapokula huwa hatosheki kamwe, ni mtu wa kubukanya wakati wote. Tatizo hili kama yalivyo matatizo mengine ya kizalia bado halijapatiwa tiba maalum, na wataalamu wengi wamejaribu bila mafanikio tiba hasa ya tatizo hili. Ugonjwa huo ulipewa jina hilo kwa sababu uligunduliwa na wataalamu wawili wa tiba wa Uswizi ambao walijulikana kwa majina ya Andrea Prader na Henrich Will, ndipo lilipopatikana jila la Prader-Will Syndrome (PWS). Hiyo ilikuwa ni mwaka 1956.

  PWS kama inavyojulikana kwa kifupi, hutokea mara chache, kwani humpata mtoto mmoja kati ya kila watoto elfu kumi au elfu kumi na tano wanaozaliwa kwa mwaka. Hii ni kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa nchini Marekani miaka ya hivi karibuni. Pamoja na tatizo hili la kubukanya, pia zipo dalili ambazo mtoto anaweza kuzaliwa nazo, na hizi mara nyingi hujionyesha kabla ya tatizo la kubukanya halijajitokeza. Dalili kama za mtindio wa ubongo na hasira za ziada za zinazohusisha uharibifu, hizi hujitokeza dhahiri, japokuwa zipo nyingine ambazo hujitokeza kwenye maumbile ya mwili wa muathirika akini mara nyingi dalili hizo hutambuliwa na wataalamu wa magonjwa ya watoto. Dalili ya kubukanya mara nyingi hujitokeza kuanzia umri wa miaka minne hadi miaka sita, lakini wengine hupata tatizo hili hata baada ya miaka 20, japokuwa ni mara chache sana.

  Ingawa tatizo hili halina matibabu yaliyo rasmi, lakini inashauriwa mtoto apelekwe kwa wataalamu wa magonjwa ya watoto mara dalili za awali zinapojitokeza kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Pia ni vyema, kwa majumbani, vitu kama vyakula viwe vimefungiwa na hasa majokofu yawe yanawekwa vitasa ili yawe yanafungwa wakati wote, hata ulaji wa watoto wenye matatizo ya aina hii uwe unaratibiwa ili wasije wakawa wanakula kupita kiasi kwani kwa jinsi wanavyopewa chakula kingi ndivyo wanavyotaka zaidi.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  mmmmh, kazi ipo
   
 3. Asabaya

  Asabaya JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 1,317
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  mmmmh! makubwa.
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kwanini tusingeendelea na ule utaratibu wa zamani ya kuwa mtoto ni mali ya jamii popote ulipo ikiosea yeyote yule anaweza kukuadhibu ili kukuweka sawa
   
 5. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Eat til you explode !
   
 6. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu huku kwetu, hususani nchi nyingi za kiafrika tatizo hili si kubwa, balaa nchi za Asia na huko Ulaya.
  Sema hii kubukanya imeniacha hoi, dogo anagonga msosi kama hana akili nzuri. kumbe ni muhathirika wa PWS
  Ni vizuri watoto wachunguzwe mara kwa mara.
   
 7. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kwa watoto wa sasa ni ngumu, unaeza ukadhalilika mtu mzama na masharubu yako...
   
 8. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Pander-Willy Syndrome! Dah! Wonders will never end!
   
 9. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #9
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwani hata wewe si unabukanya.....................LOL
  Ni kweli, lakini mimi binafsi huko kijijini kwetu Havikulongwa nilipozaliwa kuna binti nilisoma naye Msingi, yeye alilipata tatizo hilo akiwa na miaka ishirini hivi, alikuwa anabukanya kila baada ya saa moja na asipopata chakula anachanganyikiwa na anaweza kula chochote kilicho mbele yake kinachofaa kula. ilibidi ndoa yake ivunjike baada ya mume kushindwa kumtimizia mahitaji ya chakula..........Maana alikuwa anakula tu lakini hawezi kufanya kazi yoyote, sina taarifa zake kwa sasa kwani sijui kama yuko hai au amefariki kwa Kubukanya
   
 10. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkuu hii kubukanya nadhani ni kula hadi kupitiliza, geji haisomi hapo maana kama ingesoma angevimbirwa (sijui angevemberwa au angevimbiwa)
  Lakini mimi na wewe tunakula chakula, hakuna kubukanya hapo!

   
 11. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Du!!!mungu epushia mbali maradhi haya!
   
 12. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #12
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ni maradhi ambayo kwa kweli yanatisha maana hayana tiba...................................
   
 13. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #13
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mbali na kuwa unene wa watoto una(weza)sababishwa na tatizo hilo la kizalia au PWS, lakini aina za vyakula na mfumo wa maisha ya watoto wetu leo umebadilika unaweza kuwa sababu kubwa ya "Obesity" au "Anorexia".

  Zamani, wakati jamii zilikuwa na maingiliano, watoto walicheza michezo ya kujihangaisha (mpira, ready, kuruka kamba, kufukuzana...), walikuwa wanaenda shule kwa miguu au baiskeli...wakati sasa watoto wanacheza na Video Consola, kungalia TV; leo mapenzi ni mtoto kwenda shule kwa gari ya baba au basi la shule. Mwisho wa yote, watoto wanakosa harakati. Pia aina za vyakula vyetu vya "Fast Foods, Canned foods etc" vyenye michanganyiko ya mafuta na kemikali, yote haya yanawafanya watoto wavimbiane tu.

  Na yote hayo ni kweli kuwa wazazi tunachangia "kuwalemaza watoto wetu". Nimeshuhudia kesi ambapo Wizara ya Ustawi wa Jamii (nchi fulani), ililazimika kumtenganisha mtoto na wazazi wake kwa sababu nilizozitaja hapo juu. Mtoto wa kiume wa miaka 10 alikuwa na uzitowa zaidi ya kilo 100. Baada ya kulelewa katika kituo cha matunzo ya watoto, alianza kupungua na sasa ana umri wa miaka 12 na uzito wa kawaida kwa umri wake.
   
Loading...