mama anapofungwa na kichanga

Niezzle

Member
Jan 26, 2011
19
1
mama mwenye mimba anapohukumiwa kifungo na kisha akajifungulia jela , hapo inabidi atumikie kifungo yeye pamoja na mtoto wake mchanga ili aweze kumpa mahitaji yake muhimu.. je hapa si sawa na kumfunga mtoto ambaye hajafanya kosa? kama kuna mdau ana ufumbuzi au anajua sheria juu la hili tafadhali nisaidieni maana nimekuwa najiuliza sana juu ya hil
 
Mtoto atakuwa hajafungwa maana kisheria yuko huru kutoka au kutolewa nje ya gereza muda wowote. Yupo na mama yake ili kupata mahitaji muhimu. Natoa hoja
 
Hilo dada liko wazi, mwanamke mjazito akijifungulia jela basi ataendelea kutumikia kifungo hadi pale atakapomaliza kifungo chake na mwanae ambae kisheria hana kosa lakini kutokana na mahitji yake kumtegemea mama 100%. Mwisho nakukumbusha jela siyo kama ofisini eti umesikia mwanao anaumwa unaomba ruhusa kwenda kumuuguza! Akiumwa hata akifa kama haupo naye jela hutapata nafasi ya kumuuguza labda kama bado yupo hai wakuletee ndugu zao ndiyo utokee jela ukamuuguze na akifa watazika ndugu zako wewe unakwenda kuendelea na kifungo chako jela. Jela ni hatari.
 
mama mwenye mimba anapohukumiwa kifungo na kisha akajifungulia jela , hapo inabidi atumikie kifungo yeye pamoja na mtoto wake mchanga ili aweze kumpa mahitaji yake muhimu.. je hapa si sawa na kumfunga mtoto ambaye hajafanya kosa? kama kuna mdau ana ufumbuzi au anajua sheria juu la hili tafadhali nisaidieni maana nimekuwa najiuliza sana juu ya hil
Kisheria na kwa kuzingatia haki ya kila kiumbe, na haswa binadamu, huyo mama anapaswa afungwe kifungo cha nje (parole) mapaka pale mtoto atakapoacha kunyonya, muda usiopungua miaka miwili. Kisha ndio arudishwe kumalizia kifungo chake.
 
Back
Top Bottom