Mama Amina Salim Ali: Wapemba watolewe SMZ,hawakumpigia kura Dr. Shein

Status
Not open for further replies.

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
image.jpeg



Mama Amina Salim Ali amenukukuliwa akisema kuwa
WAFUKUZENI WAZANZIBARI-WAPEMBA WOTE KATIKA SMZ.

Aliyekuwa mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015 na kushika nafasi ya pili kati ya tatu bora,Mama Amina Salim Ali amenukukuliwa akisema kuwa "Wapemba wote watolewe kwenye nafasi za juu za serikali kwa vile hawakumpa kura DR Sheni na kusababishwa CCM kushindwa uchaguzi wa October 25. Aibu tulioipata kwa chama chetu lazima tuwafundishe adabu Wapemba kuwa serikali hii ni ya kimapinduzi na wao sio sehem ya serkali hii ya CCM"

Kwanza, tunamkumbusha Amina kwamba walioikataa CCM sio Wapemba bali ni Wazanzibari wote kwa ujumla wao na kwamba Shein ameshindwa na Maalim Seif kwa tofauti ya kura 25,831.

Pili, Hiyo anaoiita Serikali haina uhalali wowote kuwaongoza wazanzibari achilia mbali kufukuza watu; kwakua imekataliwa na wananchi wengi, na kama wanataka kufukuza wafanyakazi wafukuze wa Unguja na Pemba kwani wengi wao wamempigia kura Maalim Seif baada ya kuona Dokta Shein hana uwezo wa kuendesha Serikali na kuwaletea wananchi maendeleo.

Tatu, kama anataka kuisimamia hoja yake vizuri, hoja ambayo pia imekua slogan ya CCM kwa muda mrefu basi waanze kumfukuza Dokta Shein ambae nae ni Mpemba.

Nne, tunamuomba Amina aache ubaguzi, na kwamba hizi nyimbo wanazoimba zimepitwa na wakati kwa ulimwengu wa leo; wazanzibari wanataka maendeleo na sio siasa chafu zilizofeli kuisaidia CCM na kupata anguko la kihistoria Oktoba 25, 2015.

Mwisho tunamkumbusha Amina kwamba Zanzibar imechanganya damu za makabila na watu wa aina zote, hiyo ndio kawaida ya visiwa mara nyingi huwa na mchanganyiko wa damu tofauti. Tusende kwenye ukabila, tuache kupandikiza hizi chuki ili siku moja zisije kuturejea wenyewe tunaozichochea.

Zanzibar ni ya wazanzibari wote.

Chanzo:Mzalendo Net
 
Hichi chama kisipochunga ndimi za wanaoitwa makada wake naona kikipotea kwenye ulimwengu wa siasa kwa speed ya mwendokasi!
 

"Wapemba wote watolewe kwenye nafasi za juu za serikali kwa vile hawakumpa kura DR Sheni na kusababishwa CCM kushindwa uchaguzi wa October 25. Aibu tulioipata kwa chama chetu lazima tuwafundishe adabu Wapemba kuwa serikali hii ni ya kimapinduzi na wao sio sehem ya serkali hii ya CCM"[/QUOTE]
Hapo kwenye red sijaelewa, ina mana walikuwa wanalijua hili au?
 
"Wapemba wote watolewe kwenye nafasi za juu za serikali kwa vile hawakumpa kura DR Sheni na kusababishwa CCM kushindwa uchaguzi wa October 25. Aibu tulioipata kwa chama chetu lazima tuwafundishe adabu Wapemba kuwa serikali hii ni ya kimapinduzi na wao sio sehem ya serkali hii ya CCM"
Hapo kwenye red sijaelewa, ina mana walikuwa wanalijua hili au?[/QUOTE]
ccm wanazidisha moto Zanzbiar hipo siku ccm watajuta.
 
Hawa wanapandikiza mbegu ya chuki za kutisha nchini. Kwa hiyo sasa ni lazima kuwapigia kura CCM vinginevyo kama ajira yako ni Serikalini basi unafukuzwa kazi. Waache waendelee ili hili la kupandikiza mbegu za chuki watakuja kulijutia sana. Na siku zote kubomoa ni rahisi mno kuliko kujenga.

Angekuwa Maneno Hayo Kayasema Mtu Wa Upinzani,Angesha Zingilwa Kitambo na Jeshi la Polisi
 
Wanajua walishindwa kwa nini sasa wanang'ang'ania.
Huyu ndo alipitishwa kugombea urais wa JMT, kazi kweli kwelim
 
Hawa wanapandikiza mbegu ya chuki za kutisha nchini. Kwa hiyo sasa ni lazima kuwapigia kura CCM vinginevyo kama ajira yako ni Serikalini basi unafukuzwa kazi. Waache waendelee ili hili la kupandikiza mbegu za chuki watakuja kulijutia sana. Na siku zote kubomoa ni rahisi mno kuliko kujenga.
Kwani hauoni ata huku bara wanaccm ndio wanapewa kazi?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom