Mama Aliyezikata Sehemu Nyeti za Mwanae Ahukumiwa Miaka 99 Jela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama Aliyezikata Sehemu Nyeti za Mwanae Ahukumiwa Miaka 99 Jela

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Aug 19, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Katherine Nadal Tuesday, August 18, 2009 7:10 AM
  Mama mmoja wa nchini Marekani ambaye alizikata sehemu nyeti za mtoto wake mchanga wa kiume na kusingizia zimeliwa na mbwa, amehukumiwa kwenda jela miaka 99. Mahakama ya Texas, Marekani imemhukumu mama aliyezikata sehemu za siri za mtoto wake mchanga miaka 99 jela.

  Majaji walijadiliana kwa masaa mawili jana jumatatu na kuamua kumhukumu Katherine Nadal mwenye umri wa miaka 28 kwenda jela miaka 99.

  Majaji walitoa hukumu hiyo baada ya kujadiliana kumhukumu vifungo vya miaka mingi kikiwemo kifungo cha maisha. Waendesha mashataka walitaka Nadal ahukumiwe kifungo cha maisha.

  Mama huyo mkazi wa mji wa Houston, Marekani alipatikana na hatia ya kuzikata nyeti za mtoto wake wa kiume miaka miwili iliyopita na kisha kusingizia kuwa mbwa wao ndiye aliyezitafuna nyeti za mtoto huyo.

  Nadal alidai kwamba mbwa wake ambaye alikuwa na uzito wa kati ya kilo 2-3 anayeitwa "Shorty" ndiye aliyezinyofoa nyeti za mtoto wake aliyekuwa na umri wa wiki tano wakati huo alipokuwa amelala pembeni yake.

  Lakini waendesha mashtaka waliiambia mahakama kuwa mama huyo mwenye umri wa miaka 28, alikuwa ametumia madawa ya kulevya wakati alipozikata nyeti za mtoto wake anayeitwa Holden mwezi machi mwaka 2007.

  Mahakama iliambiwa kuwa Nadal alitumia kifaa chenye ncha kali sana kuzikata nyeti za mtoto wake ingawa silaha aliyotumia haikupatikana kwenye eneo la tukio.

  Madaktari walimfanyia uchunguzi Holden na walitangaza kuwa si rahisi kwa mbwa kusababisha majeraha kama aliyokutwa nayo mtoto huyo.

  Holden ambaye hivi sasa ana umri wa miaka miwili, alipoteza nusu ya damu yake kwenye mwili wake ambao ulikuwa na uzito wa kilo nne tu wakati huo. Alinusurika kufariki lakini nyeti zake zilizonyofolewa hazijapatikana hadi leo.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2842838&&Cat=2
   
Loading...