Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,316
- 33,125
Angela Sullivan, mwanamama mwenye umri wa miaka 36 aliyefanya mapenzi mara 200 na mtoto wa miaka 12
Mama wa mtoto mmoja ambaye alifanya mapenzi na mtoto wa miaka 12 takribani mara 200 na kisha kuweka alama ya nyota kwenye daftari lake kila wanapomaliza kufanya mapenzi, amehukumiwa kwenda jela miaka tisa. Angela Sullivan mwenye umri wa miaka 36 alikuwa akiweka alama ya nyota kwenye daftari lake kila alipokuwa akimaliza kufanya mapenzi na mtoto wa miaka 12.
Angela pia alimpa pea ya viatu mtoto huyo wakati alipomaliza kufanya naye mapenzi kwa mara ya 100.
Katika mojawapo ya maelezo ya tarehe 1 mwezi wa nane, yaliyoambatana na alama ya nyota ya 174, Angela aliandika "Tunakaribia kutimiza mara 200".
Angela alianza uhusiano na mtoto huyo kwa kumnywesha pombe na kuzichezea sehemu zake za siri kabla kuanza kufanya naye mapenzi karibia kila siku ya uhusiano wao wa miezi 10.
Taarifa zaidi zilisema kuwa mtoto huyo alikuwa akiwatambia wenzake kuhusiana na uhusiano wake na mwanamama huyo.
Uhusiano huo ulifikia tamati baada ya Angela kutiwa mbaroni kufuatia uvumi kusambaa shuleni kwa mtoto huyo kuwa Angela amepata ujauzito.
Akisomewa hukumu yake, Angela aliambiwa kuwa alifanya kitendo hicho kiovu kwa kumhadaa mtoto huyo mwenye umri mdogo sana.
Jaji wa kesi hiyo alimwambia Angela kuwa amesababisha matatizo ya kisaikolojia si kwa mtoto huyo bali pia kwa mtoto wake mwenyewe ambaye naye ana umri wa miaka 12.
Mahakama iliambiwa kuwa Angela alikuwa akimnunulia zawadi mbalimbali mtoto huyo ili kumfanya awe mwenye furaha.
Mahakama iliambiwa pia kuwa kulikuwa na video kwenye simu ya Angela ikimuonyesha jinsi alivyokuwa akifanya mapenzi na mtoto huyo.
Kutokana na kitendo chake hicho kiovu cha kuwaharibu watoto wenzake, jaji wa kesi hiyo alimhukumu Angela kwenda jela miaka 9.