Mama aliungua na moto akijaribu kuokoa maisha yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama aliungua na moto akijaribu kuokoa maisha yangu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Zeddicus, Sep 17, 2012.

 1. Zeddicus

  Zeddicus JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 590
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 60
  Jimmy alikuwa yupo darasa la sita wakati mama yake alikuwa akijishughulisha na uuzaji wa ndizi shuleni kwa jimmy ili kupata ada ya kumsomesha pamoja na pesa ya matumizi mengine nyumbani,baba yake na Jimmy alifariki wakati akiwa na umri wa miaka minne tu.Mama yake na Jimmy alikuwa ni mweusi asilia lakini kwa sasa alikuwa na mabaka mengi ya kahawia mwilini hii inawezekana ilitokana na kuungua na moto,hivyo ngozi yake ilikuwa ikionekana ni ya ajabu na watu wengi walikuwa wakigoma kununua ndizi kwa sababu ya ngozi yake jinsi ilivyo.
  Shuleni rafiki zake na Jimmy walikuwa wakimcheka kutokana na mama yake jinsi alivyo,alikuwa akijisikia mnyonge mpweke na akiaibishwa kwa sababu ya mama yake.
  Akaanza kujenga chuki moyoni mwake dhidi ya mama yake mzazi kwa sababu alimgeuza kuwa mtu asiyependwa na marafiki zake shuleni.
  Jimmy alisoma na kufikia elimu ya sekondari,kutokana na ukata wa familia ilibidi mama yake auze sehemu ya ardhi yake ili apate fedha za kumuendeleza mwanae wa pekee kipenzi Jimmy,alipofika elimu ya juu hakumruhusu kabisa mama yake kumtembelea chuoni kwake na alipomaliza elimu yake ya chuo kikuu alifanikiwa kupata kazi nzuri iliyokuwa ikimuingizia mshahara mzuri,hakuthubutu kwenda kijijini kwake kumuona mama yake mzazi...Mama yake alijaribu kila njia kumfikia mwanae mjini lakini alishindwa kutokana na kutokujua sehemu gani hasa mwanae anapatikana kwa kweli hii ilimuuma mno hasa ukizingatia ndie mwanae wa pekee.
  Jimmy baadae alifanikiwa kuoa na kupata watoto wawili lakini alimdanganya mkewe kuwa mama yake alikwishafariki miaka mingi iliyopita.
  Jaribu kufikiria hali anayokuwa nayo mzazi na hii ilikuwa ni miaka 12 bila ya kumuona mwanae kipenzi.
  Siku moja mama alipata anwani ya kumfikia Jimmy kutoka kwa watu waliokuwa wakimfahamu Jimmy na aliamua kumtembelea mwanae kipenzi.
  Alipofika nyumbani kwa Jimmy watu wakwanza kumpokea walikuwa wajukuu zake.Kutokana na jinsi ngozi yake ilivyokuwa ikitisha watoto walikimbia ndani huku wakilia na kupiga kelele..kweli aliwatisha.Baba yao akatoka kwa hasira na kumuona mama yake mzazi."Umefikaje hapa na kwa sababu ipi umekuja nyumbani kwangu...nilikwambia ukae mbali na mimi nishakuwa mkubwa ninayo maisha yangu wewe kwako hukohuko kijijini,ona sasa umewatisha wanangu hawatalala leo usiku sababu yako,Rudi huko ulikotoka"Jimmy alilalama.
  Mama yake alirudi kijijini akiwa na majonzi makuu na hakuona sababu ya kuendelea kuishi tena hakuna mtu aliyempenda na kumthamini katika huu ulimwengu.Baada ya siku mbili Jimmy aliitwa kijijini na taarifa kuwa mama yake amefariki kwa kujinyonga.Kulikuwa na barua aliyoiacha iliyokuwa ikisomeka hivi;

  Mpendwa Mwanangu JImmy...
  Nilikuwa na wewe tu katika maisha yangu na nilijivunia kuwa na mtoto kama wewe.Wakati ukiwa mtoto mdogo ulikuwa ndani ya nyumba na bahati mbaya ilishikwa na moto.....Nilivyoona hivyo nilikimbia na kujilazimisha kuingia ndani ya nyumba nife au nipone ilimradi nifanikiwe kukutoa ndani ya nyumba iliyokuwa imeshika moto mkubwa..Mungu alisaidia nilifanikiwa kukutoa ukiwa mzima kabisa na moto haukukuunguza hata kidogo..mwili wangu uliungua vibaya kutokana na kuangukiwa na mbao za dali zilizokuwa zina moto mkali..hivyo niliungua nikiwa katika harakati za kuokoa maisha yako sikuweza kuacha nishuhudie ukifa hata ulimwengu hujauona vizuri bado....inaniuma kuona ukiaibishwa na mimi jinsi nilivyoharibika sababu ya kuokoa maisha yako....bado ninakupenda mwanangu na nimefanya hivi ili nikuache huru na maisha yako..
  Ishi maisha ya furaha mwanangu..kutoka kwa mama yako mpendwa.
  Baada ya kusoma barua hii Jimmy alianguka na kupoteza fahamu.

  MORAL LESSON.
  Haijalishi hali gani mzazi wako anayo..usijisikie aibu kujivunia kuwa naye..wengi tumekuwa tumebanwa na mambo yetu binafsi na kufikia hatua ya kuwasahau wazazi wetu...wengine wamewakana wazazi wao kabisa ili kulinda mapenzi na wapenzi wao,acha maisha ya kujifanya(pretending) na ishi maisha yako halisi..alichofanya Jimmy kimetuweka wengi katika aibu hasa mbele ya wazazi wetu jua mtoto kwa mzazi hakui...kuiondoa aibu hii comment thread hii mbele ya wanajamvi wote kwa kuandika "Mom & Dad i love you".
   
 2. L

  LADY JO Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 5, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukweli mtupu! Yeah haijalishi una elimu kiasi gani.,pesa kiasi gani lakini kwa mzazi inabidi tuwajali na kuwapenda na kuwaheshimu! I real love my parents the way um here today is
  Frm hard working of my parents
   
 3. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,986
  Likes Received: 1,043
  Trophy Points: 280
  Yuko Mhadhiri mmoja miaka ya nyuma sana alikuwa pale UDSM. Huyu baada ya kumaliza masomo yake na kuanza kazi, aliona wazazi wake eti ni kama vile wanambuguzi kwa kumtembelea kwake pale Dar. Ndipo siku moja akaamua kulipa fadhira kwa wazazi wake kama ifuatavyo:

  Jamaa: Baba na Mama naomba mpige hesabu ya gharama zote mlizotumia toka mlivyo-nizaa hadi sasa.

  Wazazi: Hebu rudia tena Swali lako

  Jamaa: akarudia tena

  Wazazi: "Mwanangu Baba aliendelea, gharama niliyotumia kwako ni hii ...naomba nirudishie zile sh.h.w. zilizoingia kwa Mama yako ndipo ukazaliwa wewe".

  Jamaa: Kimya ( huku Mama mtu akiangua kilio).

  Toka siku hiyo jama AKACHIZIKA ndipo akahamishwa toka UHADHIRI (UDSM) na kupelekwa MAZENGO SEC DODOMA.

  Jamaa aliendelea hivyo na UCHIZI-CHIZI wake hadi MAUTI.

  Biblia Kupitia Kitabu Cha Pili Cha Mussa Kiitwacho KUTOKA (20:12) inasema:
  "Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa BWANA Mungu wako".
   
 4. T 2015 CDM

  T 2015 CDM Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Love you Dad and my Mom! MUNGU WABARIKI SANA!:love:
   
 5. kande kavu

  kande kavu JF-Expert Member

  #5
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  The Great Wizard, umenena.
   
Loading...