Mama akataa dhamana ili akae rumande na msichana wake wa kazi

mo effect

JF-Expert Member
Aug 27, 2014
567
637
Christina Thomas (28), mkazi wa Sitakishari Dar es Salaam amekataa kudhaminiwa ili arudi rumande na msichana wake wa kazi ambaye alishindwa masharti ya dhamana. Christina jana alifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa tuhuma za kumpiga mtoto wake wa miaka miwili na kumsababishia majeraha makubwa, kuzimia na kushindwa kumpeleka hospitalini.

Mwendesha Mashitaka Hilda Kato, alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ritha Tarimo kwamba mshitakiwa siku isiyofahamika Januari, alimpiga kwa fimbo mtoto huyo na kumsababishia majeraha.

Kato alidai katika mashitaka ya pili, mshitakiwa huyo ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo na msichana wake wa kazi, Blanka Benjamin kwa uzembe walimwacha mtoto huyo bila kumpeleka hospitali huku akiwa na hali mbaya ambayo ilisababishwa na mama mzazi. Baada ya kusomewa mashitaka, mama huyo alijibu kuwa hakumbuki, huku mshitakiwa wa pili ambaye ni msichana wa kazi akikana mashitaka yake.

Mwendesha Mashitaka alimwambia Hakimu Tarimo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, lakini dhamana yao iko wazi kama watakidhi masharti. Hakimu alitoa masharti ya dhamana kwa washitakiwa kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika mmoja akiwa mtumishi kwenye taasisi inayofahamika na kusaini dhamana ya Sh 800,000 kila mmoja.

Baada ya kusomewa masharti hayo ya dhamana mshitakiwa namba moja alikidhi masharti ya dhamana huku wa pili akishindwa kutokana na wadhamini kuchelewa. Hata hivyo, mshtakiwa huyo wa kwanza ambaye ni mama wa mtoto alisema hawezi kuwa nje kwa dhamana akimwacha mshitakiwa wa pili rumande hivyo kumwomba hakimu warudi wote ndani hadi kesho watakapotimiza masharti ya dhamana pamoja.

Hakimu alimwambia mshitakiwa huyo kwamba kwa sababu yeye ana mtoto mdogo hivyo angeweza kutoka na kumwacha mshitakiwa wa pili na kesho (leo) angepata dhamana, lakini akasema mtoto wake ataondoka na baba yake, na yeye atarudi rumande hadi watakapopata dhamana wote wawili.

Chanzo: Mpekuzi

Nb; Nawaza kutoka mbali--- hii sio bure, sio kwa mapenzi hayo, huwenda kuna mengi nyuma yao, husband wa mtu huwenda housigeli alikuwa anakuibia mke kwa style nyingine.
 
mtoto alimpiga yeye halafu ndani awekwe beki tatu hata mimi ningekataa!Mungu amsaidie huyu mama hayo majaribu yamuishe.Mungu ni mwema sana ukiwa muaminifu kwa jambo dogo atakupa baraka nyingi sana.huyu mama mungu atamsaidia sana kwa hilo jambo alilolifanya. ukute beki tatu ni yatima hana wa kumsaidia .kwanini wasingewatoa wote?
 
Sio bure...

Christina Thomas (28), mkazi wa Sitakishari Dar es Salasm amekataa kudhaminiwa ili arudi rumande na msichana wake wa kazi ambaye alishindwa masharti ya dhamana.Christina jana alifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa tuhuma za kumpiga mtoto wake wa miaka miwili na kumsababishia majeraha makubwa, kuzimia na kushindwa kumpeleka hospitalini.Mwendesha Mashitaka Hilda Kato, alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ritha Tarimo kwamba mshitakiwa siku isiyofahamika Januari, alimpiga kwa fimbo mtoto huyo na kumsababishia majeraha.Kato alidai katika mashitaka ya pili, mshitakiwa huyo ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo na msichana wake wa kazi, Blanka Benjamin kwa uzembe walimwacha mtoto huyo bila kumpeleka hospitali huku akiwa na hali mbaya ambayo ilisababishwa na mama mzazi.Baada ya kusomewa mashitaka, mama huyo alijibu kuwa hakumbuki, huku mshitakiwa wa pili ambaye ni msichana wa kazi akikana mashitaka yake.Mwendesha Mashitaka alimwambia Hakimu Tarimo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, lakini dhamana yao iko wazi kama watakidhi masharti. Hakimu alitoa masharti ya dhamana kwa washitakiwa kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika mmoja akiwa mtumishi kwenye taasisi inayofahamika na kusaini dhamana ya Sh 800,000 kila mmoja.Baada ya kusomewa masharti hayo ya dhamana mshitakiwa namba moja alikidhi masharti ya dhamana huku wa pili akishindwa kutokana na wadhamini kuchelewa.Hata hivyo, mshtakiwa huyo wa kwanza ambaye ni mama wa mtoto alisema hawezi kuwa nje kwa dhamana akimwacha mshitakiwa wa pili rumande hivyo kumwomba hakimu warudi wote ndani hadi kesho watakapotimiza masharti ya dhamana pamoja.Hakimu alimwambia mshitakiwa huyo kwamba kwa sababu yeye ana mtoto mdogo hivyo angeweza kutoka na kumwacha mshitakiwa wa pili na kesho (leo) angepata dhamana, lakini akasema mtoto wake ataondoka na baba yake, na yeye atarudi rumande hadi watakapopata dhamana wote wawili.

Source: Mpekuzi

Nb; nawaza kutoka mbali--- hii Sio bure, sio kwa mapenzi hayo, huwenda kuna mengi nyuma yao, husband wa mtu huwenda housigeli alikuwa anakuibia mke kwa style nyingine.
Hapo hakuna suala la msichana kuiba penzi wala nini.
Ukisoma hiyo habari kwa utulivu utaona huyo msichsna hahusiki kwa namna yoyote katika kumpiga mtoto. Mama kwa kulijua hilo, nafsi inamsuta na kushindwa kumwacha H.G rumande wakati hahusiki na kumpiga mtoto. Hayo ya wizi wa mapenzi, hata ukijaribu kuunganisha haiunganiki! House girl kaachwa rumande, mama anatakiwa arudi nyumbani na mme wake, huo wizi wa penzi umekaaje hapo? labda ingekuwa ni H.g aliruhusiwa na mama akabaki rumande hapo ungeweza kuwaza hivyo.
 
Huyu mama ana akili na huruma ya kipekee sana japo alitenda kosa kumpiga mtoto lakini amejua sio vema kumlaza house maid selo ilihali hana hatia, bora walale wote selo kidogo itamtia moyo house maid
 
mtoto alimpiga yeye halafu ndani awekwe beki tatu hata mimi ningekataa!Mungu amsaidie huyu mama hayo majaribu yamuishe.Mungu ni mwema sana ukiwa muaminifu kwa jambo dogo atakupa baraka nyingi sana.huyu mama mungu atamsaidia sana kwa hilo jambo alilolifanya. ukute beki tatu ni yatima hana wa kumsaidia .kwanini wasingewatoa wote?
Duh...hii comment ya mwaka...yaani mtu kamjeruhi mtoto na kumuacha bila kumtibu halafu umeandika hivi
 
Huyu mama ni wakuchunguza akili, ikiwezekana apelekwe milembe
 
Back
Top Bottom