Mama ajifungulia Baharini kwa kukosa kituo cha Afya

G-Mdadisi

Senior Member
Feb 15, 2018
157
99
Wakati ambapo taifa linajinasibu kufanikisha uboreshaji wa huduma za wananchi kwa kujenga miundombinu na kusogeza huduma muhimu karibu na wananchi, wakaazi wa kisiwa kidogo cha Kokota Wilaya ya Wete Kaskazini Pemba, Zanzibar wanakabiliwa na shida kubwa ya upatikanaji wa huduma ya Afya jambo ambalo linapelekea kupoteza wagonjwa wengi kwa kuhosa huduma hiyo kwa wakati.

Wamesema akinamama wa kisiwa hicho imekuwa ni jambo la kawaida kujifungulia baharini wakati wakipelekwa ng'ambo ya kisiwa hicho katika hospitali ya wilaya ya Wete huku baadhi yao wakipoteza maisha.

Kisiwa cha Kokota ni kati ya visiwa vya mkoa wa Pemba Kaskazini, Zanzibar, ambacho kinapatikana katika Bahari ya Hindi.

VIDEO

 
Hivi ule mgao wa zile pesa za covid kwa nini wasijenge japo kituo cha afya hapo maeneo
 
Back
Top Bottom