Mama achoshwa ! atoa radhi hadharani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama achoshwa ! atoa radhi hadharani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jun 22, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [TABLE]
  [TR="bgcolor: #E1E1E1"]
  [TD]KATIKA hali ambayo iliwaacha watu wengi wakiwa hawaamini macho yao mwanamke mmoja [51] amejikuta akisaula nguo zake zote na kutoa radhi hadharani kwa mwanae wa kike aliyefahamika kwa jina moja la Feti[22] kwa kile kilichodaiwa kuchoshwa na tabia zake[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Tukio hilo la aina yake lilitokea jana majira ya jioni huko maeneo ya Buguruni Mnyamani ambapo imedaiwa mama huyo alichoshwa na vitendo vinavyofanywa na mwanae huyo ambavyo vilikuwa havimridhishi.

  Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa, mama huyo jana majira ya jioni aliamua kumtolea uvivu mwanae huyo kwa kusaula viwalo alivyokuwa amevaa akiwa na lengo la kumtolea radhi.

  Awali imedaiwa kuwa Feti alikuwa na tabia za kumdhihaki Mungu kwa kufanya matendo maovu yanayodaiwa yanaenda sambamba na ukahaba ambapo mama huyo imedaiwa alikuwa akimpigia kelele kila kukicha mwanae huyo ambaye alikuwa hataki kufuata yale anayoambiwa.

  Pia imedaiwa kuwa Feti amekuwa na tabia za kugombana na wake za watu ikiwa ni pamoja na kufumaniwa na waume za watu mara kwa mara katika mtaa anaoishi hali iliyopelekea kuidhalilisha familia yake.

  Hata hivyo kutokana na vitendo na tabia chafu za Fet, mama huyo alijitoa kimasomaso kumlaani mwanae huyo jana wakati binti yake huyo alipokuwa katika matayarisho ya kutoka safari zake za usiku.

  Ilidaiwa na shuhuda wa tukio hilo kuwa mama huyo alianza hivi” Yaani ukitoka tu hapa ndani kwenda katika biashara zako za kishenzi naomba ugongwe na gari ufe papohapo” hata hivyo imediwa kuwa Fet hakutishika na kauli hizo na alitoka kinguvu na mama huyo alianza kulia kwa uchungu na kuanza kusaula viwalo alivyokuwa amevaa huku akishikwa na baadhi ya majirani zake waliomsihi kuacha kufanya hivyo huku Feti akitimua mbio na kutokomea kusikojulikana.

  Hata hivyo imedaiwa kuwa msichana huyo alikwenda kuomba hifadhi nyumba ya jirani kutokana na aibu aliyoipata kutoka kwa mama yake huyo.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hv huyo mtoto wa kike huyo siyo mamaye? Kama kweli ni mamaye hakika hb fuatilia km jana ile amerudi home salama. Usicheze na radhi. HEBU FUATILIA U2JUZE YALIYOJIRI LABDA AKAJIREKEBISHE HALAFU HUYO MAMA AKAMPATIE TENA BARAKA. Yani huyo FEKI ataona Dunia chungu.
   
 3. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #3
  Jun 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Miaka 22 dahhhhh
  Kama hashikiki ni kummuacha tutu
  Yakimfika shinngoni atarudi tu
  .
   
Loading...