Mama aanguk a shauri ya njaa-maisha bora kwa kila mtanzania?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama aanguk a shauri ya njaa-maisha bora kwa kila mtanzania??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Original Pastor, Oct 25, 2010.

 1. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  NA DUNSTAN SHEKIDELE,MOROGORO
  MAMA mmoja Fatuma Hasani,(pichani, aliyekaa) mkazi wa eneo la Bwawani mkoani Morogoro wiki iliyopita alianguka katikatika ya reli ya kati eneo la Tanesco na kupoteza fahamu,baada ya kuzidiwa na njaa pamoja na maumivu ya mkono yaliyosabaishwa na kipigo kikali alichodai kupigwa na mumewe.

  Mama huyo aliokotwa na wananwake wenzake wawili eneo hilo la reli baada ya kujikwaa kwenye moja ya reli hizo na kupoteza fahamu akiwa katikati ya reli hiyo.

  Alipohojiwa na mwandishi wetu Bi Fatuma alidai alipigwa na mumewe aliyemtaja kwa jina la Abdallah Rashid aliyekuwa akiishi naye maeneo ya Bwawani Morogoro na kwamba kipigo hicho kilisababisha mkono wake huo wa kushoto kuvunjika,

  Wakati wa mahojiano na mtandao huu, Fatuma alitia simanzi kina mama wenzake ambao nao walianguka vilio, hata hivyo baada ya kunywa chai pamoja na uji Bi Fatuma alichangamka na alipoulizwa anahitaji nini alidai anachohitajini ni msaada wa kufikishwa stendi ya Msamvu na kuongezewa nauli ya kurudi kwao Mpwapwa.

  Mwandishi wetu alitoa kiasi cha pesa na kuwaomba watu wengine waliokuwepo eneo hilo kumsapoti ambapo zilipatikana shilingi elfu 15 ambapo elfu 3 zilitumika kukodi taksi ya kumfikisha Msamvu na zilizobaki alikabidhiwa kama nauli na posho ya kula njiani.

  [​IMG]
  ..bi Fatuma akisaidiwa kupewa uji kutuliza njaa

  [​IMG]
  ...eneo la tukio maeneo ya reli
   
Loading...