Malumbano ya viongozi wa kisiasa majukwaani si afya ktk kujenga umoja wa kitaifa

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490
Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa mikutano,uzinduaji,uwekaji mawe ya msingi,kupokea wageni wa kimataifa na mingine mingi tu kupitia vyombo vya habari au mubashara na kumekuwa na hotuba mbalimbali,risala mbalimbali,na salamu za utangulizi kwa viongozi mbalimbali.

Mara nyingi sana ukiwasikiliza viongozi mbalimbali katika hotuba na salamu zao kumekuwa na malumbano sana katika ya viongozi wa pande mbili yaani chama kinachotawala kwa sasa na vyama vingine vya siasa.

Sidhani kama watanzania kwasasa hawajui kwamba kuna chama kinachotawala na kinatekeleza ilani yake baada ya kushinda uchuguzi mkuu 2015 na ukisikiliza sana maneno ya viongozi ni kama vile kufafanua sera za chama kila kukicha kuliko kujenga wananchi kuwa wazalendo wa taifa lao na hayo mambo ya chama ni matokeo tu kwasababu sio lazima kisheria kila mwananchi kuwa mwanachama wa chama fulani.

Malumbano ya kisiasa yametawala sana hotuba za viongozi kuliko kuwapa wananchi namna kupiga vita umasikini,namna bora ya kupata elimu na namna bora ya kuishi ili kuepukana na maradhi mbalimbali kitu ambacho Mwl Nyerere alikifanya sana katika ziara zake na hasa alipokuwa anaongea na wataalam mbalimbali.

Imefika hatua kiasi kwamba wananchi wengi katika hotuba mbalimbali za viongozi wamekuwa wanasubiri kusikia kiongozi akitoa tamko la 'KUTUMBUA''kumtia mtu ndani saa24' 'kumtisha mkandarasi' na mengine mengi yanayofanana na hayo.

Tunakata kusikia kutoka kwa viongozi namna gani wananchi wafanye kilimo cha kisasa cha umwagiliaji,namna gani watoto wetu wasome ili kuwa wataalamu waliobobea katika nyanja mbalimbali,namna gani wananchi masikini huko chini kabisa waepukane na maradhi njia za kinga kama magonjwa ya kuharisha,malaria,HIV TB na kadhalika.

Haya mengine ya kitaifa ya kujenga reli ya kisasa,kununua ndege,ufuaji wa umeme,ujenzi wa barabara na mengine kama hayo makubwa yawe ni mambo ya misingi ya maendeleo kwa taifa lakini siyo kama ndiyo kila kukicha tunasikia hayo tu kwenye vyombo vya habari kama vile hakuna mambo mengine muhimu kwa taifa.

Kama taifa na viongozi lazima tuangalia namna gani tunawajenga wananchi kuwa wataifa zaidi na kuipenda nchi yao na kuwa wazalendo kwa nchi yao hiyo itasaidia sana kupunguza malumbano ambayo sasa ndo yamekuwa kama ndiyo mambo muhimu sana kwenye majukwaa na hata pia katika vyombo vya habari na hasa mitandao ya kijamii.
 
Siku zote huwa tunaona ccm huwa wanafanya siasa za wazi kwenye hizo zinduzi, hujawahi kukemea tabia hiyo. Lakini leo Mnyika kaongea mambo ya msingi na kumtoa rais kwenye reli yeye na wenzake, kwa aibu ndio inakufanya kushauri. Ni hivi Rais wetu hawezi siasa za ushindani na ndio kisa cha kupiga marufuku mikutano ya siasa. Leo watu wamepata ladha tofauti na rais akapotea mpaka akajionyesha kabisa hatetei wanyonge bali huwa anahubiri tu, na kinachombeba akiongea huzungukwa na watu wanaomsifia tu bila kusikia ukweli.
 
Kwa jinsi Magufuli alivyo panic leo kwa
hoja ya dakika 2 tu ya Mnyika, nimeelewa
kwa nini watawala wengi wanaogopa siasa
za ushindani!

Maana imebidi wote waliosimama,
Ndungayi, Makonda, Waitara na waziri wa
ujenzi watetee kuokoa jahazi.

Nahisi Mheshimiwa hatapata usingizi
vizuri leo!
 
Back
Top Bottom