Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 50,872
- 21,951
SPIKA wa Bunge, Samuel Sitta amemuelezea mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema kuwa amekwisha kisiasa na kipesa na sasa anahangaika kujinasua kutoka katika hali hiyo.
Spika, ambaye anaonekana kuwa kwenye mapambano makali na wapinzani wake wa kisiasa ndani ya chama chake, alidiriki hata kumtuhumu waziri huyo wa zamani wa serikali ya awamu ya pili kuwa anapata fedha ili kuipigia debe CCM.
Sitta alitoa kauli hiyo baada ya Mwananchi kutaka maoni yake kuhusu madai ambayo Mrema aliyatoa katika mkutano wake na waandishi wa habari jana kuwa spika huyo wa Bunge la Jamhuri ya Muungano amekiuka maadili ya uongozi kwa kuendeleza mjadala wa kashfa ya Richmond pamoja na kushiriki katika ziara ya baadhi ya wabunge wanaojipambanua kuwa ni wapambanaji wa ufisadi.
Akizungumzia madai hayo ya Mrema, Spika Sitta alisema: “Mrema ni mhuni na amepitwa na wakati... pia amefilisika kisiasa na kipesa sasa anatafuta njia ya kujinasua kutoka katika hali hiyo.
"Kutokana na maneno yake hayo ninajipanga kumshtaki ili athibitishe hicho anachokisema"
Spika Sitta alisema kuwa madai na shutuma zote alizozitoa Mrema ni za uongo na zimejaa uzushi na alishangazwa na kauli za Mrema kuhoji sababu za kiongozi huyo wa TLP kuzungumzia masuala ya CCM sasa.
"Kinachoshangaza yeye ni mwenyekiti wa TLP lakini ndiye wa kwanza kuzungumzia matatizo yaliyomo ndani ya CCM, kama ameshindwa huko ni bora arejee CCM ili tupambane huku" alisema Sitta.
"Kuna uwezekano huyu bwana anapata pesa ili kuipigia debe CCM."
Sitta alisema anajiandaa kumfikisha mahakamani Mrema ili athibitishe matamshi yake ya kwamba alishirikiana na wabunge wanaojipambanua kama makamanda wa vita dhidi ya ufisadi pamoja na wafadhili wao kufanya ziara mikoani. na si muda mrefu mtasikia kahamia CCM,atuna kinyongo tunamkaribisha
Awali akizungumza na waandishi wa habari Mrema, ambaye ameshaeleza bayana kuwa atampigia debe Rais Jakaya Kikwete kwenye uchaguzi mkuu ujao, alisema Sitta anatumia makanisa kutangaza kuwa alitaka kufukuzwa uanachama kwa sababu ya msimamo wake katika suala la Richmond.
Katika mkutano huo Mrema, ambaye alivuliwa uwaziri baada ya kukiuka kanuni ya uwajibikaji wa pamoja mwaka 1995, alikwenda mbali na kumtaka Sitta ajiuzulu au aondolewe ili asiendelee kuwa spika katika Bunge lijalo.
"Kitendo cha Sitta kuamua kuendeleza mjadala wa sakata la Richmond wakati Bunge limeshafunga ni cha uchochezi na kinaweza kuvuruga amani ya nchi," alisema Mrema ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa Temeke kwa tiketi ya NCCR baada ya kupoteza ubunge wa jimbo la Vunjo kutokana na kuihama CCM baada ya sakata hilo la uwajibikaji wa pamoja.
"Pia Sitta alishirikiana na wabunge wanaojipambanua kama makamanda wa vita dhidi ya ufisadi pamoja na wafadhili wao kufanya ziara mikoani na kudhihirisha kuwa ana kundi ndani ya chama chake huku akiwa kama mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kitu ambacho ni kinyume na taratibu za Bunge na kiongozi mkubwa kama yeye," alisema Mrema.
Mrema alisema kitendo cha Sitta kuendelea kujadili suala la Richmond ni kukiuka na kwenda kinyume na taratibu za Bunge na kuwalaghai wananchi wamuone kwamba yupo mstari wa mbele katika vita dhidi ya ufisadi.
"Ni yeye Sitta ndiye aliyetangaza kuufunga rasmi mjadala wa Richmond na kuonya kwamba atakayeufufua mjadala huo atachukuliwa hatua, lakini badala yake amekuwa mstari wa mbele kuongelea mjadala huo. Hii ni sawa na kuwalaghi na kufanya uchochezi kwa wananchi. Ni lazima ajiuzulu," alisisitiza Mrema.
Akitoa mfano wa kuendelea kwa mjadala huo, Mrema alisema Sitta amekuwa akipita makanisani na kusema kuwa walitaka kumfukuza uanachama kwa sababu ya msimamo wake juu ya mjadala wa Richmond.
Mrema alidai kiongozi huyo wa Bunge hadi leo ameendelea pamoja na kunusurika kufukuzwa CCM, haogopi na ataendelea na mapambano na kusisitiza kuwa huo ndio msimamo wake.
"Spika kama mwamuzi anayesimamia haki ndani ya Bunge hakupaswa kuonyesha ushabiki au kujionyesha kwamba anaunga mkono upande fulani na badala yake alipaswa asiwe na upande wowote," aliongeza mwenyekiti huyo.
Mrema alidai Sitta ameweka kitu moyoni hivyo ajiuzulu ili awe huru kukitoa na si kuendelea kuzungumzia kitu ambacho mjadala wake ulishafikia mwisho.