malumbano ya hoja, tanzania kama wanasheria ndo hawa, basi taifa limekwisha. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

malumbano ya hoja, tanzania kama wanasheria ndo hawa, basi taifa limekwisha.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MBUFYA, Mar 1, 2012.

 1. MBUFYA

  MBUFYA JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Nafuatilia kipindi cha malumbano ya hoja kupitia ITV, mmmh, ijapo mi sio mtaalam wa sheria lkn hawa wanasheria kila wakichangia hoja natamani kuzima tv, wengine ni kama wanajikomba kwa polisi, wengi wanatetea kuwa polisi ni haki kutumia nguvu kwa kutumia risasi za moto.
   
 2. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kwa aina hii ya wanasheria sitoshangaa tena kusikia kwamba Tanzania imesaini mkataba mwingine mbovu!!

  Wanasheria wa nchi hii ni bogus kabisa!
   
 3. MBUFYA

  MBUFYA JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  mchangiaji aliye pita hapa sasa ndo ovyo kabisa, eti anasema wanaharakati ni vibaraka wa watu kutoka nnje ya nchi na nia yao ni kumchafua raisi jakaya kikwete, huyo naye ni mwanasheria, pia anasisitiza kuwa polisi waendelee kuua watu,
  kama hufuatilii kipindi hiki sasa jitahidi kuangalia marudio yake. utalia.
   
 4. MBUFYA

  MBUFYA JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  nina wasi wasi magamba wamesha nunua wacjangiaji.
   
 5. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,163
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  kipindi hiki kimejaa watu walioandaliwa mahsusi,hivi mialiko yao huwa inakuwaje hadi wanapatikana watu wa kuja hapo kwenye kipindi.
  Eti hawa ndio wasomi tunaowategemea kweli kwa mustakabali wa matatizo ya nchi hii? Mimi nasema wazi kuwa bado tuna safari ndefu saana kufikia mageuzi ya kweli. Wengine naona wana makaratasi ya maelekezo ya walichoelekezwa kusema katika mpangilio Rasmi.
   
 6. MBUFYA

  MBUFYA JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 445
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Nakubaliana na hayo mkuu.
   
 7. Q

  Qualbalasad Member

  #7
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  hakika hapa rushwa njii hii nimekubali bila wanafiki wanafiki wasipokatwa vichwa, hakika hii ni komedi
   
 8. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Kipindi kimeisha ila ninahakika kipindi hiki polisi wameamua kupiga propaganda makusudi, wamenunua airtime ili kufanya siasa
   
 9. Q

  Qualbalasad Member

  #9
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 96
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Sio kwamba wanajikomba ni hakika jeshi la polisi limetumia kiasi cha fedha kuununua mdaalo huo, siamini kama hao ni washiriki huru. Siruhusu nafsi yangu kumdharau mtu lakini hawa nimewadharau++. Yawezekana ni mizimu ilitoka dunia isiyo na uelewa
   
 10. N

  NIMIMI Senior Member

  #10
  Mar 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 170
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ndugu zangu wanaJF inakera sana kufuatilia kipindi ambacho kimejaa wachangiaji waliokosa mvuto, Nashindwa kufahamu Uelewa wao wa Kujenga hoJa, kweli nimeamini Maneno ya Wahenga kwamba 'KWENYE MITI MINGI HAKUNA WAJENZI' nikianza na Wanasheria Uchwara wasiojua Tasnia yao kwa Mapana, kumbe Chuo cha Ustawi wa Jamii Wanafundishwa kujenga Uchumi wa nchi kama wale waliokuepo katika Kipindi cha Malumbano ya Hoja walivyotukumbusha eh?

  Kweli pale kuna vilaza asiyeweza hata kufafanua sababu za msingi zinazopelekea wananchi kuandamana? Ama kweli 'vyuo vimekuwa vingi hata kwenye vichochoro kumegeuzwa kuwa vyuo na hatimaye kuzaliza wasomi wasioweza kufahamu sababu za Wananchi kuandamana, Loo hoi?

  Wiki Jana katika taarifa ya habari ya ITV ya saa 2 usiku na iliyorudiwa saa 5 baadae, walitangaza Benki kuu ya Dunia imefadhili kiasi cha dola kadhaa za kimarekani ili kujenga majengo ya Kisasa katika chuo cha Dar es salaam, sasa yule mpuuzi aliyesimama na kuwaponda wapigania haki wanaopoteza Uhai na haki za msingi za kuishi kwa kuuawa na Risasi za moto, kwamba wanafadhiliwa na mataifa ya NJE?

  Hadi bajeti ya nchi yangu yenye amani japo polisi wanawapotezea wengine haki ya kuishi, inafadhiliwa na wahisani kutoka nJe tena robo3 yake sembuse watetea haki za binadamu wanaouawa ovyo?
  Kweli nimemkubali jamaa anaesoma chuo cha Mwl Nyerere alisimama vyema katika kutoa hoja tena za msingi, na hasomi sheria sio 'VILAZA' Wengine wanatokea vyuo vya uchochoroni hata kusimama wakatetea maslahi yao wenyewe hadi wategemee baadhi ya vyuo ambavyo vina wanamapinduzi ya kweli kama IMTU wanafunzi wao walivyotinga hadi wizara ya Elimu kuhakikisha hatima ya wenzao walisimamishwa miezi7 hadi sasa, ndo mambo mabadiliko ya kweli kutoka kwa wasomi, sio kulala na shahada zenu vitandani na kujitangaza eti mmesoma, thubutu!
  Wasomi mahala popote na nchi yeyote ndo waletao mabadiliko sio kuwa vilaza kama kwa baadhi waliojitambulisha ni wanasheria halafu hakuna kitu vichwani mwao.

  Polisi hawapaswi kuua bali kutumia Reasonable force katika kuthibiti ghasia za aina yeyote ile, kama kupiga virungu, maji ya kuwasha, kupiga risasi za baridi ambazo mara zote hutoa mlio ila kudhurika hadi karibu sana na mpigaji kama nusu meta, ama kupiga miguu na sio Kuua.
  Serikali kutambua kero za wananchi na kuzitatua haraka iwezekanavyo hata kama kwa kutoa ahadi, wawe wepesi wa kukubali majadiliano na yawe yenye kuleta tija na kuepuka Danadana kwa waathirika, mfano mafao ya wazee waliotumikia Jumuiya ya A. Mashariki, madaktari, hali ngumu ya maisha kwa wananchi tena waliowengi, walimu na watumishi wengine wote, kuthamini 'utu mtu'
  na walitumia madaraka yao vibaya wamekula rushwa pamoja na kuingiza nchi katika hasara kubwa washughulikiwe na sheria husika,

  swala la ARDHI limeonekana kuleta picha mbaya pia wananchi wasidhulumiwe haki yao,
  kwani yatokeapo yote haya wananchi wanaona serikali imewasaliti ndipo wanaamua kuingia barabarani kwa lengo la kudai haki zao matekeo yake pole wanatumia 'EXCESSIVE FORCE' katika kuwatawanya pasipo kujali haki zao mwishowe wanawang'anya wananchi pamoja kama wanadamu wanajinyima haki ya kuishi.

  Nipo Jukwaa linalofuata.....
   
 11. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,105
  Likes Received: 7,363
  Trophy Points: 280
  Msichoelewa ndugu zanguni ni kua Kuna wachangiaji wengine pale wamevaa kiraia but ni mapolisi hivyo wanajua wanachofanya.
  Pia wengine ndio kama hivyo unawaona kabisa wamenunuliwa.
  Yaani mpaka nikaanza kufikiri kua wale watu wetu hapa JF leo wameamua kutia timu pale ku-support upuuzi,
  maana hata kwa kipindi kile pumba zao ziliadimika humu JF
   
 12. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,473
  Likes Received: 4,752
  Trophy Points: 280
  Mimi nilifuatilia sana .......hata uchangiaji wao ni kama wamekuwa trained kabisa........
   
 13. bht

  bht JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  I had the same feeling, sikuona malumbano ya 'hoja' ila porojo tupu
   
 14. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Wanapaswa kutumia not only reasonable force lakini pia wanapaswa kutumia proportional force,thus action and reaction should at least be equal and opposite.
   
 15. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #15
  Mar 2, 2012
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Mi nilikuta kipindi kimeanza, nikavumilia kusikiliza wachangiaji wawili tu, nikashindwa. Yaani ujinga uliorushwa jana imenifanya nifikirie marambili hii TZ yangu na mwelekeo wake. Kaazi kweli kweli.....:smash::smash::smash::smash:
   
 16. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,891
  Likes Received: 6,085
  Trophy Points: 280
  unajua kilichotokea ndio wenye akili zao inabidi waanze kufikiria upya ni jinsi gani ya kukomboa idadi kubwa ya Watanzania kutoka karne ya 17 na kuwakumbusha kuwa tuko tayari karne ya 21!

  Sio siri kuwa wahudhuriaji wengi jana inawezekana walikusanywa na hata posho watakuwa walichukua, utadhani nchi sio ya kwao. Inasikitisha.

  Nilichojifunza zaidi ni kuwa kuna wasaliti na mamluki wengi sana ambao wanaweza kukwamisha juhudi za ukombozi, wanaamini katika ule mfumo wa KITUMWA kuwa kuna watu waliojaaliwa na Mwenyezi Mungu kuifaidi nchi na wengine wamelaaniwa na ni haki yao kuishi maisha ya taabu kama wanayoishi!
   
 17. C Programming

  C Programming JF-Expert Member

  #17
  Mar 2, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 2,748
  Likes Received: 1,781
  Trophy Points: 280
  mimi huwa nafuatilia sana kipindi hiki na wachangiaji wengi....huwa ni walewale wa kila siku ila kwa jana kile kipindi niliona watu wengi walioenda pale ni wageni .....na kilichonishangaza ni kwamba wanaharakati wa haki za binadamu sikuwaona kama akina ananilea nkya,mkurugenzi wa kituo cha haki za binadamu naye sikufanikiwa kumuona
   
 18. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #18
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Jamani mnaijua tamu chungu????

  Ndo hii ya jana
  Chungu = Inauma sana tu kuona uchangiaji wa aina ile kwa mambo mazito na yenye hatari kama hoja ya jana ila tufute machozi na kuanza upya ilhali tukiwa tumejua kwamba tatizo ni kubwa kuliko tunavyolidhania

  Tamu = Wamejiweka wazi sana na ni rahisi kujua jinsi ya ku deal nao hawa watu wa upande wa pili as bila kufanya vile jana ingekuwa ngumu sana kuwabaini watu wa aina hii. So wana jamvi na wengine wapendao maendeleo ya kweli tutakuwa tumetolewa utando na kuweza kuona kwa ufasaha zaid.....ilisemwa kwamba kituo kile kinatoa air time kubwa kwa mambo wanayoyataka wao.....na sasa imejirudia kwa sura na umbo tofauti dhahir shahir....

  With such wanasheria ndo maana hata state inapoteza kesi nyingi sana na mikataba inakuwa hivi ilivyo. Tanganyika Law Society mpo hapo jamani.....are you still deserving the label "The Learned" .... Law School ????? wanandugu mmechafuka
  khaswa au ni uanasheria wa mahakani tu??? Mbona reasoning za jana zimekuwa kawaida sana ??? Quoting vifungu bila contextual review????

  Congratulations to Kibatalla he did an indepth root establishment and analysis on the topic and its conssociates

  They say time is the best healer ever......so with time we shall heal n remain healthier n wiser
   
 19. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #19
  Mar 2, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mkuu naona unawajumuisha "wanasheria wote" ikiwa suala linahusu watu wachache?
   
 20. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #20
  Mar 2, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  1. Mkuu wanatumia "Tanganyika Law Society" wanataaluma hawa. Kwa kutumia jina hilo adhimu wajue wamebeba majukumu mapana kama jina lenyewe, so kwa umoja wao au mmoja mmoja wajue wameshabeba jukumu la kusimamia haki za Watanganyika na hii iwe ajenda yao unless wabadilishe jina.

  2. Ila kwenye biashara zao huko za "advocacy" wala hatuwajadili as huko soko litasema na tayari linasema nani ni nani
   
Loading...