Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,973
Salam Wadau,
Nimepata mwaliko wa kushiriki kipindi cha leo cha malumbano ya hoja katika kituo cha television cha ITV, kitakachoanza kuruka hewani ''live" kuanzia saa tatu usiku.
Mada itakayokuwa mezani ni Nafasi ya vijana katika siasa za Tanzania: Je, vijana wanatumika kama madaraja katika vyama vya siasa Tanzania?
Kwa taarifa ambazo sijazithibitisha zinapasha kwamba miongoni mwa waalikwa ambao watakuwa meza kuu ni pamoja na viongozi wa vijana toka vyama vikubwa vya siasa nchini; Chadema, CCM na CUF. Pia nimedokezwa kuwa Adam Chagulani (Kijana aliyekuwa diwani wa Igoma kupitia Chadema) anatarajiwa kuwepo pamoja na vijana wengine wenye nyadhifa mbalimbali katika vyama vya siasa na mashirika/taasisi mbalimbali za kijamii na kisiasa.
Ningependa kupata mawazo yenu katika mada iliyoko mezani, wakati tukisubiri kuingia ulingoni. Je kuna ukweli kiasi gani katika mada husika? Karibuni kwa mjadala.