Malumbano ya hoja ITV: Madaraka ya Rais katika katiba mpya

Bwana Dovutwa kuna hoja moja nzuri ameijenga! Inawezakana vip Rais wa jamhuri ya muungano anaweza toka zanzibar na akatawala wabara na tanganyika yao wakati mtu wa bara haruhusiwi hata kuwa sheha zanzibar?
 
dovutwa anasema rais wa tanganyika awepo na pia awe na madaraka ya kuweza kuwa rais wa zanzobar pia kama mzanzibari anavyokuja huku na kuwa rais wa bara.
 
Mkuu nipo karibu na tv naangalia cnn huku siipati tbc labda kama utanipa web address yao, nilimaniisha sioni kwa maana ya orodha ya uliyotoa sikuona mwakilishi wa chetu; utagombea wapi chaguzi zijazo?

Chama
Gongo la mboto DSM


Chama mbona unatia aibu. Kipindi cha malumbano ya hoja huwa hakirushwi kupitia hicho kituo ulichokitaja. Unless leo ndiyo umejua uwepo wa kipindi hicho na hukuwa ukikijua kabisa. Ambayo itakuwa ni ajabu sana. Lakini pia, kumbe wewe ni mmoja wa wale wachache mliobaki kuhalalisha matumizi mabaya na ubadhirifu mkubwa wa mali ya umma kupitia hicho kituo cha tv ulichokitaja, asalaaaaaaale, kweli huko uliko asubuhi mnazi ni bora zaidi ya chai?
 
Fahmi Dovutwa naona amepotea hapa, anazungumzia mzanzibari kuwa raisi wa jamhuri kwamba ni kinyume cha katiba. Pamoja na watangazaji kujitahidi kumrudisha kwenye mstari lakini bado amekomaa na hoja yake ya mzanzibari kutoruhusiwa kuongoza serikali ya jamhuri ambayo inaiongoza Tanganyika kwakuwa anapofanya mambo ya Yanganyika wakati yeye si raia wa Tanganyika.
Kazi kweli kweli...
 
Du huyu jamaa mwenye kibandiko chekundu. Na gwanda jeusi wanambana (ni nani Dovutwa?) kwani anadai Rais wa Zanzibar hawezi kuiongoza Tanganyika au virse versa ni kwelli katufumbua tunapoteza muda kujadili marekebisho hayo
Du kweli wamemkata Dovutwa ITV hamtendi haki mnawaMINYA wasema ukweli
 
Naona dovutwa amekaza anataka wamuelewe wenyewe nadhani wamepigwa kamemo wasimamishe kipindi!
 
Mjadala unaoendelea kwenye kipindi cha malumbano ya hoja kuhusu madaraka ya rais katika katiba mpya ijayo! Hoja mbali mbali zinatolewa na waalikwa, wengi wao wakiwa ni viongozi wa vyama vya siasa! Wengi wao wamekosoa sana madaraka Makubwa sana aliyonayo rais hasa kwenye uteuzi wa nafasi mbalimbali za uongozi, wakiwemo Dk. Emmanuel Makaidi, Julius Mtatiro, Mwita Mwikwabe Waitara, Dovutwa... Makaidi ameazima msamitati wa prof. Shivji kwamba rais wa Tanzania ni 'Imperial President'. Waalikwa ambao ni Makada wa CCM wanakubaliana na madaraka hayo na msimamo wao ni kwamba yaendelezwe kwenye katiba inayokuja! Mjadala unaendelea!
 
Sasa hivi kuna kichapo kikali kinaendelea matangazo wamesitisha ili kulinda watoto wasione!
 
Wanasheria wa ccm wameamua kuwakilisha kile ambacho wamekisambaza nchi nzima kama mwongozo kwa wanachama wao.
Hawataki madaraka ya raisi yaguswe.


Kuna wanasheria ambao hawatataka kuona mabadiliko yoyote yanatokea, kuanzia madaraka ya rais, hadi tume ya uchaguzi. Hawa wanafaidika na mfumo wa sasa, wanapata kazi za kuandaa mikataba mibovu na ya kuhujumu uchumi. Na bado serikali itajitokeza na kusema mikataba mibovu ni kwa sababu ya elimu ndogo ya wataalam.

Pengine huyo mwanasheria angesema sifa za mtu anayetakiwa kuwa jaji wa mahakama ya rufaa ni zipi? Elimu inahusika?
 
Chama mbona unatia aibu. Kipindi cha malumbano ya hoja huwa hakirushwi kupitia hicho kituo ulichopkitaja. Lakini pia, kumbe wewe ni mmoja wa wale wachache mliobaki kuhalalisha matumizi na ubadhirifu mkubwa wa mali ya umma kupitia hicho kituo cha tv ulichokitaja, asalaaaaaaale, kweli huko uliko asubuhi mnazi ni bora ya chai?

Samahani Makene sina chochote ninachojua kuhusu vipindi vya tv Tanzania; nilichotaka kujua kama chadema kina mwakilishi kwenye malumbano ya hoja na si zaidi!ahaa haaa mnazi nayo ni pombe au sumu umeshawahi kuona mnywa mnazi ana akili nzuri?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Haka kajamaa ka ssm kanakojiita ni kamwanasheria, naona katakuwa nashida.. Maana kanaleta upedeshee wa lugha kanatumia vingereza katikati ya kiswahili... Haaaah... Huyu jamaaa kama ndiye anashauri kesi za ccm basi hata tukimpa asimame na mrema mzee wa vunjo atamshinda tu
 
Mkuu nipo karibu na tv naangalia cnn huku siipati tbc labda kama utanipa web address yao, nilimaniisha sioni kwa maana ya orodha ya uliyotoa sikuona mwakilishi wa chetu; utagombea wapi chaguzi zijazo?

Chama
Gongo la mboto DSM

Chama wacha kujishebedua hiyo tv yenu mnaiangalia ninyi wenyewe sisi tulishaachana nayo siku nyingi.
Halafu nimegundua kwamba huwa unakurupuka kuandika hapa JF kwani kama ungesoma heading usingeandika hayo madudu yako.
 
Matatiro anatiririkaanadai kuwepo kwa madaraka makubwa ya raisi, yamesabisha kuwepo kwa umungu mtu hapa duniani, mfano raisi amnamteua mkuu wa mkoa, leo watu wakiandama tu tayari mkuu wa mkoa (mwanasiasa) anamuamrisha rpc (proffesional) kuamuru polisi kupiga watu.. Hii ni hatari sana
 
Kunamchangiaji anauliza nini lilikuwa lengo kubwa la kudai uhuru???? Dahaaa nimelipenda hili swali, coz lengo tulitaka tuwe huru, tujitawale, leo mtu mmoja tu analala anasema anzisha mkoa, hivyo hivyo mkoa unaanza... Anasema akiona kijana anatamka wazi kuwa raisi aendelee na madaraka yake huyu mzee anasema anatilia mashaka sana uwezo wa huyo huyo kijana, huyu mzee anaitwa mzee ndegu kama sijakosea
 
huyu kunambi ni kizazi cha magamba na baba yake alikuwa mmoja wa waanzilishi wa ccm ndio maana bado naye anaota kuwa nape mwingine.
 
Back
Top Bottom