Malori yaliyokamatwa yakivusha mahindi kwenda Kenya??

victor11

Member
Feb 24, 2011
67
7
DSC01632.JPG

Kama kweli tunataka kuendeleza kilimo haya mambo tunatakiwa tuyaangalie kwa uangalifu. Haiwezekani mkulima alime kwa juhudi zake zote, leoa anataka kuuza matunda ya kilimo chake ili ajipatie kipato umwambia hapa nchi itakuwa na njaa, hivyo sivyo.

Ili kukifanya kilimo kivutie wengi ni lazima kuwafanya wao fanya kilimo waonekane wanamabadiliko fulani katika hali zao za maisha. Haiwezekani watu wanalima miaka nenda miaka rudi hawana mabadiliko maisha yao yako vile vile, hali hii haitawavutia vijana kufanya kilimo. Wafanyakazi wanapopata mishahara yao hakuna mtu anayewapangia watumie vipi mapato yao, kwa nini wakulima.

Suluhi la tatizo hili ni sarekali kuongeza akiba ya chakula, ili kupambana na upungufu utakao jitokeza.

Kisha kuwaruhusu wakulima kuuza mazao yao bila bunguza, kipato watakacho kipata kitakuwa motisha kwa wao kuongeza juhudi, pia kuifanya sekta hiyo kuwavutia watu wengi zaidi haswa vijana.
 
hiyo kweli kabisa!eti serikali inataka mkulima auze humu humu nchini kwa sh 300 kwa kilo,wakati akiuza kwa mganda atapata sh 700 kwa kilo.mbona wahindi wanapeleka mbaazi,dengu india hawakatazwi?licha ya pamba,katani,korosho,kahawa etc
 
DSC01632.JPG

Kama kweli tunataka kuendeleza kilimo haya mambo tunatakiwa tuyaangalie kwa uangalifu. Haiwezekani mkulima alime kwa juhudi zake zote, leoa anataka kuuza matunda ya kilimo chake ili ajipatie kipato umwambia hapa nchi itakuwa na njaa, hivyo sivyo.

Ili kukifanya kilimo kivutie wengi ni lazima kuwafanya wao fanya kilimo waonekane wanamabadiliko fulani katika hali zao za maisha. Haiwezekani watu wanalima miaka nenda miaka rudi hawana mabadiliko maisha yao yako vile vile, hali hii haitawavutia vijana kufanya kilimo. Wafanyakazi wanapopata mishahara yao hakuna mtu anayewapangia watumie vipi mapato yao, kwa nini wakulima.

Suluhi la tatizo hili ni sarekali kuongeza akiba ya chakula, ili kupambana na upungufu utakao jitokeza.

Kisha kuwaruhusu wakulima kuuza mazao yao bila bunguza, kipato watakacho kipata kitakuwa motisha kwa wao kuongeza juhudi, pia kuifanya sekta hiyo kuwavutia watu wengi zaidi haswa vijana.

Sidhani kama hayo ni mahindi ya mkulima! hayo kuna mfanya biashara kawalangua wakulima kwa bei poa yeye anapeleka nje so kama ni utetezi watetee wafanyabiashara utaeleweka.
 
Mkulima ana mtegemwa mfanya biashara kupata soko bora la mazao yake hivyo kadri mfanya biashara anapo pata soko zuri mkulima nae atanufaika ,serekali kuzuia Mahindi kuuzwa nje nikupingana na kauli mbiu ya kilimo kwanza, lakini pia Raisi amekua akihimiza wa Tanzania watumie fursa zilizoko kwenye soko la afrika mashariki leo kumetokea fursa ya soko la nafaka kwenye nchi za pembe ya Afrika lakini serekali ina zuia hiyo fursa hilo ni kosa kubwa,
 
Serikali iache wakulima wauze mazao kwa bei nzuri huko Kenya labda wanaweza kupata kipato cha kuwakwamua hapo walipo.
 
Nadhani tatizo hapo ni ushuru. Je hao walionunua hayo mahindi na kutaka kuyapeleka nje ya nchi wamelipa ushuru stahiki??
 
Kazi kweli.nani wa kukaumiwa?wakati mwingine wakulima wanajisahau wanauza chakula chote then wanaitegemea serikali iwalishe.tuangalie pande zote mfanyabiashara anachoangalia ni faida tu kwake na si kwamba anamjali mkulima,
 
Ni muhimu kutowachukulia wakulima kama watu wasio na akili bali serikali ndiyo inayojua yote. wakulima wanauza mazao ili walipie ada watoto wao na kujipatia mahitaji mengine. kama serikali inaona wakulima wanalanguliwa na hao wafanyabiashara basi serikali iyanunue hayo mahindi kwa bei ileile wanayotoa walanguzi. Hakuna mlaliaji mkubwa wa wakulima Tanzania zaido ya serikali.
 
Back
Top Bottom