Malori yakwama bandarini Dar, madereva walalamikia ukiritimba na rushwa kurudi kama zamani

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,052
28,239
Mwananchi online linaripoti kukwama kwa malori bandarini.

Je wapo wanaopima kina cha maji?

========

Mwananchi Digital imeripoti kuwa katika bandari ya Dar es Salaam kuna maroli (magari makubwa ya mizigo) yamekwama kwa siku kadhaa hivyo kusababisha madereva wa maroli kulala na kuamka hapo hadi kufikia siku nne, madereva hao wamedai kulala na kula kwenye magari yao na kuomba kujisadia katika vyoo vya ofisi za jirani kwa kuwa hapo bandarini hakuna vyoo.

Madereva hao wamedai chanzo cha uchelewashaji huo wa mizigo unatokana na ucheleweshwaji wa kupakua na kupakia mizigo na na ucheleweshwaji wa vibali vinavyoruhusu mizigo kusafirishwa.

Hata hivyo juhudi za kumpata mkurugenzi wa mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Eriki Hamisi ziligonga mwamba baada ya kujibiwa kuwa yuko kikaoni na baadae simu yake ilipiwa bila kupokelewa. Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Leonard Chamriho aliahidi kumuunganisha mwandishi na watu wanaohusika jambo ambalo pia halikufanyika.

Dereva aeleza, "mimi toka nipo hapa siku ya nne ushushaji wa kopa bandarini ni mbovu ukimuuliza ajenti anakwambia gari zimejaa, mwenye mzigo anasema nimekodisha godauni natumia foko za bandari ukimwambia nilete foko zangu anasema hakuna sheria ya kuleta foko zako. Kwa hiyo bandarini ukiritimba umerudi kama zamani na rushwa imerudi. Tunaomba serikali iingilie kati swala hili madereva tunateseka bandarini kumeoza tunaomba msaada".


 
Mwananchi online linaripoti kukwama kwa malori bandarini.
Je wapo wanaopima kina cha maji?

E0NhMwdXIAAW0HL (1).jpeg
 
Hii habari nimeisikia tangu jana na inadaiwa kuna urasimu unafanyika.

Mama Samia huenda anahujumiwa na tatizo lake ni kutoweka watu wake kuanzia serikali kuu bali kaamua kurithi aliowakuta.

Hata huyo boss mpya wa bandari aliyemuweka hawezi timiza majukumu yake vizuri kama amezungukwa na watu wenye lengo la kuharibu/kuhujumu kuanzia huko juu.

Mawaziri wa Magu sidhani kama wanajitoa kiasi cha kutosha kumsaidia huyu mama.

Habari yenyewe ni hii:

 
Mwananchi online linaripoti kukwama kwa malori bandarini.
Je wapo wanaopima kina cha maji?
Hao Mwananchi wameanza kujitokeza walikokuwa wamejificha,walikuwa wameufyata mkia miaka yote sita ya mwendazake,kutwa walikuwa wanaimba na kusifia awamu ya 5, utafikili waliungana na TBC ,Uhuru na mzalendo,

Kwa Sasa Mwananchi hawana hata sofa ya kifungia vitumbua.
 
Hao Mwananchi wameanza kujitokeza walikokuwa wamejificha,walikuwa wameufyata mkia miaka yote sita ya mwendazake,kutwa walikuwa wanaimba na kusifia awamu ya 5, utafikili waliungana na TBC ,Uhuru na mzalendo,

Kwa Sasa Mwananchi hawana hata sofa ya kifungia vitumbua.
Hakili za hovyo hizi. Jifunze kuhimiza utendaji sio simulizi. Maadereva wenyewe wanasema afu wewe umekaa kwenye key board unaaandika tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom