Malori ya michanga usiku wa manane Dar ya nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malori ya michanga usiku wa manane Dar ya nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 15, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kwanza, mdogo wangu alinilalamikia kuwa hawalali usiku kwani kuna malori yanapita usiku wa manane huko Kunduchi yakiwa yamebeba michanga. Tatizo ni kuwa malori haya hupita katika cover of darkness na kuharibu sana barabara na madaraja. Nikamuambia kwanini asifuatilie kwa viongozi wa mtaa pale nyumbani? baada ya kufuatilia akakuta anaambiwa na viongozi kuwa "aliache" suala hilo kwani malori au biashara ni ya mbunge mmoja wa CCM ambaye ni maarufu kwa mambo ya sanaa sanaaa!

  Tukiwa tunafikiria nini cha kufanya kutoka maeneo ya Mbezi Beach nako kisa ni hicho hicho. Mdogo alikuwa anashare yanayotokea huko Kunduchi na rafiki yake ambaye naye akasema kule kwao malori hayo yanaletwa kwenye nyumba za uraiani ambapo yanapakua mchanga huo ambao kwa maelezo yake unadaiwa kuwa unaletwa kutoka "Shinyanga" a.k.a kwenye migodi..

  Baada ya kupewa taarifa hizo nikaanza kuuliza ni nyumba gani zinazopokea mchanga huo na ni kina nani wanaruhusu mambo hayo kufanyika tena kwa kificho jawabu lake limenitisha. Kumbe watu wenyewe hata huwezi kuwapeleka polisi au kulalamika kwani ndio wenye wenyewe kupitia proxies wao.

  Sasa watu kama hawa tunawashughulikiaje? maana kama hadi mchanga wetu ni dili na watu wetu wenyewe kwa tamaa ya fedha wanashiriki kuuza basi sisi yawezekana ni taifa la mazezeta kupita yote yaliyowahi kuwepo duniani - kama yamewahi kuwepo mengine. Au tunaongozwa na magenius wawekezaji!
   
 2. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #2
  Jun 15, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Jun 15, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,555
  Likes Received: 18,245
  Trophy Points: 280
  .
  Mzee Mwanakijiji, mimi naishi njia hii hii ya Bagamoyo, fanya kidogo kautafiti zaidi toka kwa huyo nduguyo, malori haya yapitayo usiku kucha, sio ya kubeba mchanga, ni malozi yanayobeba malighafi ya kiwanda cha Wazo kwa ajili ya kutengeneza sementi. Mzigo huwa unatoka bandarini na kusafirishwa nyakati za usiku mpaka asubuhi wakati hakuna foleni. Ni malozi zaidi ya 100 yanarindima usiku kucha na ni kweli barabara inachafuka sana, japo baadae husafishika yenyewe.

  Hii sio shughuli ya kila siku, ni msimu kwa msimu kila meli ya mzigo ikija. Kiukweli, Wazo walitakiwa wajenge reli ya Malighafi yao kusafirishia mizigo mikubwa hivyo na sio kutegemea barabara zetu hafifu ambazo huishia kuharibika.
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Hiyo material inaitwa clinque na inatoka nje ingawa nasikia kule Dodoma sehemu inaitwa Kibakwe yapo mamilioni ya tani yamelala.Ni kweli kuwa inasafirishwa usiku kuondoa usumbufu wa foleni manake huwa ni malori kwa mamia.Hilo suala la reli kujengwa ni gumu.Katika masterplan ya Jiji letu tukufu ya 1978(vita ikaharibu) ipo njia ya reli toka ubungo(UFI) kupitia Sinza,(Mori mpaka Kakobe church),Makongo,Lugalo,Mbezi mpaka Tegeta.Shida watu wakajenga juu ya njia hiyo na kubomoa itakua balaa kubwa.Ukiiona ile mastapalni unaweza kulia,watu walifanya kazi sio mchezo,four lanes everywhere hata Uhuru road ni four lanes,Mwenge to city centre six lanes.
   
 5. Obuntu

  Obuntu JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wakuu,

  Whether ni clinque or any-cement-production related raw material(s), barabara ya Bagamoyo usiku ni njia ya Magendo. Well, mimi ni mwenyeji sana wa barabara hii na nadiriki kusema malori yanayopita barabara hii USIKU wa MANANE sio ya Wazo tuu - Yanakwenda all the way to-fro Bagamoyo yakisheeni bidhaa ambazo ni "magendo" na mara zote utakuta Land-Rover za POLICE "PT XXX" zikiwa zinasindikiza malori haya - karibia Daraja la Bunju kuna njia inaelekea kushoto (going mabwepande) ni uchochoro mzuri sana ambao malori haya yanapitia.

  Hii njia inapita maeneo ya "Msitu wa Zombe/Pande" na "Off-loading" hufanyika somewhere in between halafu malori hurudi na MCHANGA!
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Mimi bila kuiona hiyo master plan ninalia kila siku. What the hell is going on in our minds!
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Pasco.. nafahamu hilo na wao wanafahamu tofauti ya malori yanayoenda Wazo kwani hatimaye yanaingia Wazo.. na yale ambayo hayaingii Wazo yanaishia uraiani...
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  binafsi ningependa kuiona...
   
 9. Obuntu

  Obuntu JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kiongozi Pasco,

  Kama umesoma vizuri post ya MMKJ, haya malori anayosema siyo yale yanayopita kwenye "MAIN ROAD" pale Mbezi Beach - haya yanaingia "MITAANI" aka kwenye maeneo watu wanayoishi kufanya "LOADING" ya bidhaa fulani. Lori linalopita "MAIN - ROAD" litakuwa na usumbufu mdogo kwa mkazi wa MBEZI BEACH - na kama ulivyobandika ya "msimu" - Haya yanaoingia "mtaani" siyo ya msimu!
   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Mzee wangu(RIP) aliwahi kuwa City Engineer miaka ya 1970 na alikuwa na hiyo kopi....very proudly...vile alishiriki...bahati mbaya sikuwahi kuichukua baada ya umauti wake na kwa kweli inaniuma kuwa jinsi ilivyopotea.....ila niliiona na aliikuwa akinipa expert advise kuhusu miradi ya ujenzi miaka ya 1990 hasa barabara ya Kigogo(Kawawa) ambayo alisema haikujengwa kwa plani ile iliyotakiwa na alijaribu mara nyingi kushauri bila kusikilizwa na alitabiri kuwa muda si mrefu itajaa kwa foleni na kila mara nikishuhudia hili likitokea
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  inawezekana inafichwa sasa maana tukiipata halafu tukalinganisha na ramani ya Google!! tunaweza tukalia kweli.
   
 12. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Ni kweli inafichwa kwa kuwa nilijaribu kuifuatilia pale Jiji bila mafanikio.Unajua moja ya issues alizoniambia mzee ni CCM kujitwalia maeneo ya wazi na ndio maana plani ile inafichwa.Pale Mango Garden ni eneo la wazi UVCCM imelitwaa na mengine mengi.Viwanja vingi hasa Kuanzia Sinza,Mikocheni,Mbezi Beach haviko sawa ndio maana Mbezi beach kuna shule moja tu ya msingi ya umma.
   
 13. Kbd

  Kbd JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2010
  Joined: Oct 9, 2009
  Messages: 1,264
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  My dia hoa watu hatuwezi kuwashughulia chochote maana kwanza wako juu ya sheria na pia ndio hao hao walioinunua hii nchi....... ni yao na ndio maana wanafanya wanachokitaka na hakuna wa kuwauliza.
   
 14. Madabwada

  Madabwada JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2010
  Joined: May 8, 2009
  Messages: 537
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  nitajaribu kwa mzee fulani hivi .... anaweza kuwa nayo hii ... hawa wazee walikuwa expert wa ukweli katika haya mambo ... sijui nini kilifayika hata ushauri wao ukawa unakataliwa kila kukicha ... nakumbuka mzee huyu pia alisukiwa zengwe la hatari (alifuatwa fuatwa na kupekuliwa sana na watu wa usalama) wakati wa mradi kama huo miaka ya 80 mwanzoni mpaka ikamlazimu kuhamia pwani kikazi (toka wizarani) kabla ya kustaafu kabla ya wakati na kuendelea na biashara zake ... nahisi hichi ndio kipindi tanzania ilipoanza kuoza!!
   
 15. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Tulijikwaa 1978 Bigtime na mpaka sasa tunaanguka tu....Dollar moja ilikuwa TZS 5(daladala?)....sasa hivi imefunga turbo kuelekea TZS 2,000 na jamaa wana mpango wa kuprint noti mpya...soon tutakuwa na noti ya 100,000....na hii mastaplani ilitengenezwa mwaka huohuo 1978...ukiipata iweke hapa tafadhali na MMJJ aipate....
   
 16. W

  WildCard JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mambo yanayofanyika usiku kwenye Jiji hili unaweza kudhani DOLA na vyombo vyake HAVIPO kabisa! Ukikosea ukawambia wafanye PATROL umewatajirisha. LiNchi limeoza hili jamani. Makao makuu ya Polisi, UwT, JWTZ yote yako hapa. Kwa nini hali iko hivi? Tunashindwa kukusanya kodi ili tuwalipe vizuri wafanyakazi wetu kwa sababu kama hizi.
   
 17. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #17
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mkuu wewe acha tu!! I support your vocabulary "dollar imefunga turbo" maana sas ni balaa!! Jana wamepitisha bajeti huku wanasema wanatarajia mfumuko wa bei utashuka kufika 5%!! Bila ya kuwa na mikakati!!!!

  Jiji ni chafu kupita kiasi, balaa la foleni linatoa mianya ya kutumia usiku visivyo!!!
   
 18. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #18
  Jun 15, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,844
  Trophy Points: 280
  Asante ndugu yangu.....hiyo avatar yako niemipenda...is it Kiefer?...I like the father Donald....a good actor...as the son is
   
 19. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #19
  Jun 15, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwenye red: samahani -- hapo mjomba una maana 'clinker' bila shaka.
   
 20. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #20
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Ni Kiefer... Naomba yeyote atakaye pata master plan ya jiji 1978 atubandikie hapa. Unajua ukijiuliza ilikuwaje CCM iwe na maeneo makubwa yote mazuri ktk jiji hili utashindwa kuelewa... Now I understand why!! Jiji hili halina standard anymore. Viduka, viosk, groceries, bar everywehre... kila mtu akistaafu anaruhusiwa kufanya chochote; frame za maduka kwenye kuta za majumba. Ni nchii pekee.....

  Wanasiasa, wamekalia drama tu. Bajeti ndo hiyo, hakuna mkakati wowte wa kupunguza muda wa kusafiri ili kuongeza production... Kazi yetu ni wizi tu. Watu sasa ivi wako busy na mbinu mpya za kutudanganya wadanganyika tuwarudishie ULAJI. Mungu na airehemu nchi yetu.
   
Loading...