Malori mawili aliokamata DC yakiepeleka mahindi Kenya yatozwa faini 20,000 @;DC ahamaki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malori mawili aliokamata DC yakiepeleka mahindi Kenya yatozwa faini 20,000 @;DC ahamaki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Jul 13, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,766
  Trophy Points: 280
  Katika hali isiyokuwa ya kawaida dc mmoja wa rorya bw kitenga amepata mshtuko wa gafla pale alipokuta
  gari alizokamata tena kwa kujificha yeye na mapolisi kuzuia wafanyabiashara kupeleka mahindi kenya
  kulipa sh 20,000 faini kila mmoja,dc huyo amesema kuna michezo michafu sana kati ya polisi mahakama na wafanyabiashara hili zoezi ni gumu sidhan tunaitaj kupoteza muda wetu tena kama unakamata lori lina semi trela yake mbili unakuja kuwalipisha alfu ishirini..mbali na hilo mh kitenga amesema malori hayo upitisha mahindi njia za panya hata hivyo akasema kuna mkono wa mtu si hivi hivi hizi biashara nimezifwatilia sana lakini n aona si hivi hivi...wakimuuliza waandishi pengine unaweza kufatilia sana kunaweza kuota kibarua chako alisema yeye anafanya jukumu lake lakini ikifika wakati na yeye ataondoka atakuja mwingine kama alivyoondoka aliemtangulia...

  Kikwete kazi unayo
   
 2. M

  Misterdennis JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: Jun 4, 2007
  Messages: 1,521
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Nadhani serikali ndio inasababisha watu wasitumie njia halali katika biashara.
  Serikali ina haki gani kuwazuia wenye mazao kuyauza popote pale ... hata nje ya nchi? wakulima wanapokuwa wanalima, serikali huwa inaingia ubia nao?.
  Wakiwazuia kuuza mazao yao kunapo bei nzuri, definitely watatafuta njia mbadala za kufikisha mazao yao kwenye soko walitakalo; na hapo serikali ndipo inapokosa kukusanya kodi mbalimbali kwa maamuzi yake mabovu.

  Kwanza ni kituko, fikiria , et DC amekaa vichakani anategea magari ya magendo yapite ili ayakamate! ... ccm wana vituko kwelikweli!
  Ndio maana tunasema, wakuu wa wilaya hawana kazi yoyote! kazi kula kodi za Watanzania bure. Ni vyeo vinavyotumiwa kupeana ulaji.
   
Loading...