Je, Malkia anamiliki eneo ndani ya nchi yetu?

Mimi nimepita mara nyingi eneo hilo na simulizi ni nyingi mno, kuwa ni la malkia ingawa limeendelezwa sana. Kuna mashamba ya chai pamoja na miwati na miti mingine kwa kweli ni eneo zuri sana, natokea ktk mkoa ulio na ukijani mwaka mzima lakini pale ni pazuri mno n a ukijani wake ni mzuri sana, kila kitu karibu wanatumia mashine na wanazalisha umeme wao wenyewe. Kuwa haturuhusiwi kuingia siyo kweli wafanyakazi wengi ni watanzania wenzetu na ni wakarimu sana ukifika watakutembeza na unaweza ambulia majani ya chai pia.
 
Kwa namna ninavyofahamu, hiyo ardhi unayoizungumzia ni kampuni ya miwati(Tanganyika Wattle Company) iliyopo Kibena Njombe.

Awali inavyosemekana ilikuwa ni mali ya Royal family ya Uingereza na ambapo CDC(Commonwealth Development Co-operation) walikuwa na hisa na TDFL pia nao walikuwa na hisa(sifahamu % ya hisa ilivyokuwa). Baadae(mwishoni mwa miaka ya 80 kama sijakosea), Royal family waliachia hisa zao zote kwa CDC n kufanya CDC kumiliki 85% ya hisa na TDFL Kuwa na 15% ya hisa.

Baada ya hapo sijui kilichotokea, lakini 2005, ikaonekana kama CDC ilikuwa inamiliki 100% ya hisa na hivyo ikauza hisa zake zote kwa Kampuni ya Kenya ijulikanayo kama KALDORA International, inayomilikiwa na masingasinga ambao asili yao ni Iringa na ndiyo wanamiliki Mufindi Paper Mills(zamani SPM Mgololo)

Katika kipindi chote cha mabadiliko TANWAT ilijipanua hadi Kilombero na kujishughulisha na upandaji wa Mi Tiki wakiwa na kampuni ya KVTC, so KVTC ikatenganishwa na TANWAT na ika fall kwa African Forestry ambayo ina misitu Uganda, Gabon na pia South Sudan.

Kwa hiyo nadhani Malkia alishaiacha hiyo ardhi ya Njombe na kama ana ardhi anayomiliki kwa sasa labda itakuwa hiyo ya Kilombero.

mkuu hongera kwa kazi nzuri.
 
Liko sehemu gani? Iringa au Mbeya? na nipatie jina la kijiji ili niweze kutembelea huko siku moja.

Mimi nimepita mara nyingi eneo hilo na simulizi ni nyingi mno, kuwa ni la malkia ingawa limeendelezwa sana. Kuna mashamba ya chai pamoja na miwati na miti mingine kwa kweli ni eneo zuri sana, natokea ktk mkoa ulio na ukijani mwaka mzima lakini pale ni pazuri mno n a ukijani wake ni mzuri sana, kila kitu karibu wanatumia mashine na wanazalisha umeme wao wenyewe. Kuwa haturuhusiwi kuingia siyo kweli wafanyakazi wengi ni watanzania wenzetu na ni wakarimu sana ukifika watakutembeza na unaweza ambulia majani ya chai pia.
 
Hilo eneo analomiliki malkia si liko pale Njombe ! ukiwa unatoka kama Makambako unaelekea songea liko upande wako wa kushoto.Hapo hata Prince Charles aliwahi kulala miaka ya nyuma
 
Kama wanayatumia kwa maendeleo ya nchi na kukuza uchumi, hamna tatizo lolote! Tanzania ina maeneo mengi sna ambayo ni Productive lakini watanzania tumeshindwa kuyatumia! Kwahiyo tusiwalaumu wawekezaji as long as na sisi tunafaidika kutikana na uwepo wao!
 
Musoma mjini pale kati kati ya mji pia inasemekana malkia anamiliki eneo. Lipo karibu na stendi kuu ya mabasi mjini Musoma.
 
Ndugu wana JF

Kuna taarifa ambazo sijazithibitisha kwamba, Malkia wa Uingereza anamiliki Eneo Kubwa sana Ndani ya Nchi yetu, ambapo Hata Serikali yetu haina Mamlaka ya Kuingia.

Eneo linasemekana liko Mkoa wa Iringa

Naomba mwenye taarifa kamili anijuze
Kwa nini usifanye utafiti wa kutosha kwanza angalao uwe na taarifa za kutosha kabla hujaanza kusambaza uvumi tu?
 
Amekuwa Mmiliki wa ENEO hilo tangu enzi na enzi - hata wakati "Saint-to-Be" anataifisha mashamba kule Arusha ilo shamba/eneo halikuguswa.. Lipo Wilaya/MKOA? ya/wa? NJOMBE.
Tangu lini Njombe ikawa Mkoa wa Arusha? Jamani mbona kiwango cha ignorance hapa JF kinaenda over the roof.
 
Nchi zote zilizowahi kuwa makoloni ya Uingereza.
Siyo nchi zote zilizokuwa makoloni bali ni nchi za Commonwealth ambazo ziliamua kufuata mfumo wa Westminster ambapo mkuu wa serikali ni Waziri Mkuu na mkuu wa nchi ni Malkia. Nchi ambazo ziliamua kufuata mfumo wa Presidential ambapo rais ni mkuu wa nchi na serikali kama Tanzania Malkia hana wadhifa wowote isipokuwa kama mkuu (wa heshima) wa Commonwealth (Jumuiya ya Madola).
 
Uwezekano ni mubwa usisahau kule zenji jamaa wa oman anamiliki eneo kubwa sana!

Loliondo je? Bora Waingereza kuliko waarabu maana Waingereza watatusaidia japo kidogo, waarabu msaada wao mkubwa ni kutuharibia kaka zetu wa kiume na dada zetu! Nyambaf!
 
.....Ni kweli malkia ana mashamba IRINGA na TANGA..kuna aliyeelezea vizuri sana ishu ya TANWAT na KVTS ...namuunga mkono..

kwa upande wangu sioni ubaya ..kama hayo mashamba yalikuwa yake na wakati wa uhuru tukaamua kumuachia kama zawadi hatuwezi kumnyanganya ..haitakuwa ustaarab,...tena afadhali yeye anayo na analima chai na miti .....wengine wanamiliki mapori na kuiba wanyama wetu....
 
Kwa namna ninavyofahamu, hiyo ardhi unayoizungumzia ni kampuni ya miwati(Tanganyika Wattle Company) iliyopo Kibena Njombe.

Awali inavyosemekana ilikuwa ni mali ya Royal family ya Uingereza na ambapo CDC(Commonwealth Development Co-operation) walikuwa na hisa na TDFL pia nao walikuwa na hisa(sifahamu % ya hisa ilivyokuwa). Baadae(mwishoni mwa miaka ya 80 kama sijakosea), Royal family waliachia hisa zao zote kwa CDC n kufanya CDC kumiliki 85% ya hisa na TDFL Kuwa na 15% ya hisa.

Baada ya hapo sijui kilichotokea, lakini 2005, ikaonekana kama CDC ilikuwa inamiliki 100% ya hisa na hivyo ikauza hisa zake zote kwa Kampuni ya Kenya ijulikanayo kama KALDORA International, inayomilikiwa na masingasinga ambao asili yao ni Iringa na ndiyo wanamiliki Mufindi Paper Mills(zamani SPM Mgololo)

Katika kipindi chote cha mabadiliko TANWAT ilijipanua hadi Kilombero na kujishughulisha na upandaji wa Mi Tiki wakiwa na kampuni ya KVTC, so KVTC ikatenganishwa na TANWAT na ika fall kwa African Forestry ambayo ina misitu Uganda, Gabon na pia South Sudan.

Kwa hiyo nadhani Malkia alishaiacha hiyo ardhi ya Njombe na kama ana ardhi anayomiliki kwa sasa labda itakuwa hiyo ya Kilombero.

Mkuu Walionunua SPM-Mgololo ni wahindi kutoka kenya kupitia kwa Mungai ambaye inasemekana pia ana hisa kwa majina ya ndugu zake wa kenya, bado kuna mgogoro unafukuta pale Mgololo mpaka sasa.

Jua pia kuna eneo ana miliki Karume wa Zanzibar huko Iringa
 
Ndugu wana JF

Kuna taarifa ambazo sijazithibitisha kwamba, Malkia wa Uingereza anamiliki Eneo Kubwa sana Ndani ya Nchi yetu, ambapo Hata Serikali yetu haina Mamlaka ya Kuingia.

Eneo linasemekana liko Mkoa wa Iringa

Naomba mwenye taarifa kamili anijuze

La kushangaza lipi hapo Mkuu Egongos, kwani si nayo Tanganyika inaimiliki Zanzibar?
 
Ndugu wana JF

Kuna taarifa ambazo sijazithibitisha kwamba, Malkia wa Uingereza anamiliki Eneo Kubwa sana Ndani ya Nchi yetu, ambapo Hata Serikali yetu haina Mamlaka ya Kuingia.

Eneo linasemekana liko Mkoa wa Iringa

Naomba mwenye taarifa kamili anijuze

Mbona hujasema GWB kapewa kigamboni karibu robo tatu yake! Na bado. Jamaa wakija hata kwako wanaweza kufuta hati yako kwa kile kiitwacho maslahi ya nchi.
 
Mkuu Walionunua SPM-Mgololo ni wahindi kutoka kenya kupitia kwa Mungai ambaye inasemekana pia ana hisa kwa majina ya ndugu zake wa kenya, bado kuna mgogoro unafukuta pale Mgololo mpaka sasa.

Jua pia kuna eneo ana miliki Karume wa Zanzibar huko Iringa

Ni kweli kabisa Mungai ni Mkenya! siwezi kuwaeleza zaidi. Nchi yetu ni shamba la bibi. Nashangaa wa zenji sijui wamelewa nini wanataka kutuacha!
 
Back
Top Bottom