Malisa:katibu mkuu mpya, shirikisho la vyuo vikuu katoloki tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malisa:katibu mkuu mpya, shirikisho la vyuo vikuu katoloki tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Alfu Lela Ulela, Jul 28, 2012.

 1. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Rais wa Chuo Kikuu cha St.Augustine Mwanza Bw.Malisa Godlisten EJ, amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa shirikisho la vyuo vikuu vinavyomilikiwana baraza kuu la maaskofu Tanzania (TEC), na vilivyo chini ya Chuo Kikuu cha St.Augustine yaani SU-SAUT.


  Malisa ambaye anafahamika kwa harakati zake za kupigania maslahi ya wanyonge na kukosoa udhaifu wa serikali alipata kura 16 dhidi ya kura 4 alizopata Bw.Donath Salla aliyekuwa mpinzani wake.

  Uchaguzi huo ulifanyika juzi katika chuo kikuu kishiriki cha Elimu Mwenge kilichopo Moshi, wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa SU-SAUT (Annual General Meeting). Jumla ya vyuo tisa vilishiriki katika mkutano huo, isipokuwa Chuo Kikuu kishiriki cha Jordan Morogoro,na Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Bugando ambavyo vilikosa uwakilishi.


  Malisa ambaye alishinda urais wa SAUT kwa kishindo licha ya hujuma nyingi zilizofanywa dhidi yake, alikuwa Katibu Mwenezi wa Chadema (CHASO-SAUT) chuoni hapo, kabla ya kugombea Urais. Pia amewahi kuwa mjumbe wa mkutano mkuu wa CHADEMA wilaya ya Moshi Mjini.


  Pamoja na kuwa kiongozi Malisa amekuwa mwanaharakati wa muda mrefu, ambapo makala zake nyingi zimekuwa zikiibua gumzo miongoni mwa jamii. Mwaka 2009 akiwa kidato cha sita alivamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa kichwani kwa panga, ikiwa ni siku chache tu baada ya makala yake kuchapwa gazeti la MwanaHalisi yenye kichwa ‘[FONT=&quot]MTOTO WA MKULIMA AMEANZA KUPOTEZA IMANI’

  [/FONT]

  Viongozi wengine waliochaguliwa katika mkutano huo ni Malima Silas (Mwenyekiti), Joseph Rufili (Makamu Mwenyekiti), Donath Salla (Naibu Katibu Mkuu) na Ephraim Kababaa (Mweka Hazina).
   
 2. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Sijakuelewa unazungumzia uongozi katika ngazi ya wamiliki wa hivyo vyuo au unazungumzia uongozi katika ngazi ya ushirikiswaji wa wanafunzi?
   
 3. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #3
  Jul 28, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Upande wa Wanafunzi. Rais wa chuo hawezi kuwa mmiliki.
   
 4. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,143
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  amani na salama... Waamini,
  Mungu wa yakobo ampe nguvu
   
 5. D

  DR. RICHARD Senior Member

  #5
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 127
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mtetea wanyonge huyu, mbona hajasema chochote hata tangazo tu pale ofisini kwake kuwajulisha nini kinaendelea kuhusu pesa za mfunzo kwa vitendo na watu wamepigika huku mitaani balaa na field yenyewe inaisha week ijayo?
   
Loading...