Malisa GJ anasema unapotaka mabadiliko hakikisha unakuwa sehemu ya mabadiliko hayo

MusuKuma

Member
Jan 30, 2021
25
75
Kwa muda mrefu sasa tumesaidia watu wengi kupitia ukurasa huu. Pamoja na kuwa na majukumu mengine mengi lakini nimejitahidi mara kwa mara kuwa na muda kidogo kwa ajili ya jamii. Ilifika mahali kila mtu mwenye shida alielekezwa kwenye ukurasa huu. Japo hatukuweza kusaidia wote lakini tulijitahidi kwa kadri ya uwezo wetu kugusa maisha ya wale tulioweza kugusa.

Kutokana na wahitaji kuwa wengi ninyi wenyewe mkapendekeza tuwe na Foundation ili tuweze kusaidia watu wengi zaidi. Kwa miaka zaidi ya miwili nimekua nikishauriwa kuwa na Foundation lakini nikasita. Mwaka huu "kelele" za foundation zikawa nyingi sana. Baada ya kutafakari nikaona umuhimu wa kufanyia kazi wazo hilo.

Kwa kuwa sauti za kuanzisha foundation zilitoka kwenu nilitegemea muwe mstari wa mbele kuhakikisha wazo hilo linafanikiwa. Lakini ni bahati mbaya sana imekuwa kinyume. Mwitikio ni mdogo sana, kuliko challege yoyote ambayo tumewahi kuifanya hapa.

Hii imenifundisha kuwa watu wengi wanapenda mabadiliko lakini hawataki kuwa sehemu ya mabadiliko hayo. Mtu akipata shida anataka aje kuomba msaada hapa, lakini hataki kusaidia wazo la kuwa na taasisi itakayomsaidia yeye na wengine wengi zaidi. Hali hii sio kwamba tu inakatisha tamaa, bali pia inavunja moyo kusaidia wengine.

Anyway, kesho tutahitimisha challenge yetu, na tutaeleza msimamo wetu kuhusu huduma yetu ya kusaidia jamii, ambayo tumekuwa tukiifanya kwa muda mrefu sasa. Tujifunze kwamba, unapotaka mabadiliko hakikisha unakuwa sehemu ya mabadiliko hayo. Usipofanya wewe, hakuna wa kufanya kwa niaba yako.

Kama unataka kuona huduma ya #GiftedHeart ikikua na kugusa maisha ya watu wengi zaidi tuma mchango wako kwenda (M-PESA) 0743339247, Gwakisa Mwakitega AU (Tigopesa) 0715568653, Samson Charles Kamnde AU (AirtelMoney) 0787568653, Samson Charles Kamnde.

#GiftedHeart #RudishaTabasamu #LetLoveLead #MalisaGJ
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom