Malipo ya watumishi wa umma kuhuishwa kielektroniki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malipo ya watumishi wa umma kuhuishwa kielektroniki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 23, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  SERIKALI imesema katika muda wa miezi saba itakuwa imekamilisha kuhuisha malipo ya mishahara ya watumishi wa umma kwa njia ya elektroniki.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Hawa Ghasia, aliyasema hayo juzi mjini hapa wakati akizungumza kwenye mafunzo ya programu ya maboresho ya utumishi wa umma awamu ya pili kwa viongozi wa Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera.

  Ghasia alisema katika muda wa miezi sita au saba ijayo, hakutakuwa na sababu za kusaka mchawi katika malipo ya watumishi yakiwemo malimbikizo mbalimbali kwa sababu kumbukumbu zote zitakuwa katika mfumo wa elektroniki.

  “Tumeanza na halmashauri za Mkoa wa Pwani, kati ya Januari hadi Juni, kila kitu kitakuwa kimekamilika katika mikoa mingine,” alisema Waziri Ghasia na kuongeza: “Orodha ya malipo itaonesha mfanyakazi anadai nini.

  Karibu tutamshika mchawi maana ile hali ya kudai Utumishi ndio wanakwamisha itakwisha.”

  Alisema yapo malimbikizo ya mishahara yanayosababishwa na uzembe wa watendaji wa halmashauri kwa kushindwa kufuatilia vyema matatizo ya watumishi wao wenye madai mbalimbali.

  Akizungumzia maboresho hayo ya utumishi wa umma, Waziri Ghasia alisema yameletwa kwa nia ya kuongeza ufanisi na tija kwa watumishi wa umma katika kuwatumikia wananchi.

  Alisema nia ya Serikali kuona utumishi wa umma unatukuka na watumishi wanatimiza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu na kutoa huduma kulingana na matakwa ya kazi zao.
   
 2. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #2
  Jan 24, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  itapendeza kama tu haitakaa kifisadi

   
 3. H

  HAM Member

  #3
  Jan 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni mzuri lamsingi uboreshaji (up date) ya takwimu za watumishi ufanyike mara kwa mara ili kuwawezesha watumishi wa umma kupata haki zao
   
Loading...