Maoni: Malipo ya Wabunge yapunguzwe

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Ninatazama Utv Alasiri hapa kwa kweli nchi hii bado tuna changamoto nyingi na pia kundi kubwa la watu hasavijijini wanaishi maisha magumu mno.

Mfano hapa wananchi wa Lindi Njinjo walikua wanaelezea jinsi gani wanavyosumbuliwa na barabara mbovu ambazohupelekea hata kipindi cha mvua wakina mama wajawazito hujifungulia porini, njiani mbovu mno hazipitiki.

Jingine wameongelea zahanati, yaani zahanati haina umeme mzazi akipelekwa pale usiku anaulizwa umekuja na taa?

Daktari ndio huyo huyo mmoja amsikilize mgonjwa akatoe na dawa foleni inamsubiri.

Kwa kweli ukifikiria shida hizi za wananchi vijijini na malipo wayapatayo wabunge havieleweki.

Ifikie pahala mapato yote ya wabunge yakiwemo posho za kamati na pesa ya kustaafu bunge yaani baada ya miaka mitanovipunguzwe hata kwa 50% na waondolewe misamaha ya kodi za magari ili pesa nyingine zikajenge zahanati, barabara, umeme na usafiri gari za wagonjwa vijijini.

Nadhani ili tuendelee ni vema wote tukafunge mikanda.
 
Mkuu unaonaje wakiwamo vigogo wote wazalendo kwa kilipa kodi stahiki kwa kuanzia tu?

Vigogo - rais, vp, mawaziri, jaji, spika, makatibu wakuu, ma RC, ma DC, wakurugenzi serikalini na kwenye mashirika, nk.

Msururu wao ni mrefu hauna mwisho.
 
Back
Top Bottom