Malipo ya Wabunge ni kufuru

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,820
11,521
Kwa mwaka mmoja mbunge hulipwa takribani million 170, pesa hizo hulipwa kutokana na mshahara ambao ni zaidi ya milioni 11 ambayo ukizidisha mara miezi 12 unapata milioni 132.

Vilevile mbunge hulipwa posho za vikao (sitting allowance) Tsh 220,000/= na posho ya kujikimu (perdiem) Tsh 80,000/=, posho hizi hulipwa kwa kipindi ambacho mbunge anakuwa bungeni ambazo ni zaidi ya siku 130 ikiwemo zile za kamati, kwa vikao tu mbunge hukunja takribani million 39 ikiwa ni nje ya mshahara, lakini pia mbunge ni diwani pia hulipwa posho mbali mbali anapokuwa kwenye vikao vya halmashauri.

Na baada ya miaka mitano hulipwa kiinua mgongo cha zaidi ya milioni 250.
 
Sasa hapo mawaziri wanalipwa ngapi? Rais na makamu wake je?

Aisee!
Halafu hawasaidii wanyonge.

Wanawatuma TRA kuja kutufungia biashara kisa tu kodi, hali ni mbaya biashara hakuna. Tukifunga biashara wanakosa hata hizo SDL na PAYE.

Akili au matope. ? Kumbe wanalipana bei ndefu hivi.

Ndio maana meko yupo tayari kuua na anakuua kweli kudadeki.

Meko anakupiga shaba live mchana kweupe

Na ndio maana Kina halima roho zimewatoka. Mil 11 kwa mwezi sio padogo, na hata ndungai ndio maana kila kukicha anamuwqza Mbowe. Sasa hivi sijui atakuwa anamlalamikia nani kwa sababu Mbowe hayupo.
 
mimi naona wanastahili,kazi ya ubunge ni ngumu sana 🤣
Ni ngumu kweli maana wapiga kura wako lazima wakutafute 'walie njaa' wanapokwama.

Hivyo lazima mbunge awe na pesa za kushughulikia dharura kama hizo.
 
Kila msiba wa jimboni kwako lazima utoe ela
Ni ngumu kweli maana wapiga kura wako lazima wakutafute 'walie njaa' wanapokwama.

Hivyo lazima mbunge awe na pesa za kushughulikia dharura kama hizo.
Kuna hela ya maendeleo ya Jimbo, inayopatikana katika mfuko wa jimbo, pale ndio hutoa pesa za kufanya hayo...ilimradi tu madiwani wameshirikishwa wakatia saini.
 
Back
Top Bottom