Malipo ya Mamilioni Parastatal Pensions Fund (Invoices): Rewarding and Defending Corruption

Status
Not open for further replies.
Yaaaani inachosha kabisa .Unashindwa kutofautisha haya mashirika yenye FFF na Taaasisi kama TRA. they dont do nything really social kuwasadia wanachi wa kawaida. Kwenye kundi hili pia kuna Bima ya afya.

Hizi performance criteria wanazotumia kuchota hayo mafedha ni zipi?
 
Mwanakijiji.
Hongera kwa kuendelea kufundisha jamii kile ambacho CCM na serikali yake haipendi kufanya.
Nimejaribu kuangalia risiti ya kwanza jina limewekwa Baduru Msangi, lakini kwenye maelezo ya malipo wameweka Badru Msangi. Sasa sijui kuna kamchezo kama kale ka Rostam ka kubadilisha herufi kwenye majina yake kupoteza ushahidi!!

No matter what...huu ni ufisadi uliokubuhu.
Tanzania, tunahitaji nchi yetu.
 
Nahisi kichwa kuuma na kizungu zungu!

Kwa nini watumie scale za marekani na ulaya kujilipa?? hii nchi ni maskini jamani..
 
Mwanakijiji.
Hongera kwa kuendelea kufundisha jamii kile ambacho CCM na serikali yake haipendi kufanya.
Nimejaribu kuangalia risiti ya kwanza jina limewekwa Baduru Msangi, lakini kwenye maelezo ya malipo wameweka Badru Msangi. Sasa sijui kuna kamchezo kama kale ka Rostam ka kubadilisha herufi kwenye majina yake kupoteza ushahidi!!

No matter what...huu ni ufisadi uliokubuhu.
Tanzania, tunahitaji nchi yetu.

Mbona haya tumedokeza kidogo tu jamani... tutajitahidi kulimaliza kabla ya wiki, inshallah.
 
Si siku watu huwa wanamjibu Mwanakijiji na JF. Ngoja tusubiri watuandalie hayo majibu!! I hope hawatafanya mistake ya ndege ya serikali wakati wa uchaguzi!!
 
Ile thread ya rais mwizi nilipoifungua watu walisema tunamwonea JK, madudu yanavyoibuka sijui wale watetezi wako wapi? Tanzania do not deserve this type of leadership, haiwezekani uingie madarakani kwa wizi na kazi yako kubwa iwe ni kufikiria jinsi ya kujitajirishe wewe na maswaiba zako kwa kutumia cheo cha wizi na kutafuna kodi yao bila kuwajibika. The time is now or never. Nasubiri siku tutakapomuona anakwenda Segerea kutumikia kifungo chake.
 
Halafu majina ni yaleyale. Nimechoka mwili na roho. Halafu leo hii wanaleta fyokofyoko. Pumbavu.
 
Yaaaani inachosha kabisa .Unashindwa kutofautisha haya mashirika yenye FFF na Taaasisi kama TRA. they dont do nything really social kuwasadia wanachi wa kawaida. Kwenye kundi hili pia kuna Bima ya afya.

Hizi performance criteria wanazotumia kuchota hayo mafedha ni zipi?

Haichoshi mkuu Nyani kashikwa pabaya .... ..... then wanasema hatuna umeme kwa sababu hatutaki kumlipa Dowans or Tanesco wana madeni mengi hivyo hawana uwezo wa kununua majenerator yao JK na serikali yake hawana nia wala uchungu wa kulinasua hili taifa kwenye matatizo yake dawa yao ni kama Libya, Tunisia , Misri nk hatuwezi kuendelea na group la wezi. Sasa sijui wapi kwenye nafuu ... .... khe khe kheeeeeeeeee kuanzia kwenye miradi ya madini Sin bin Clair, Utalii, loliondo kulikouzwa kwa waarabu .... ..... ..... ..... ...... ..... then kuna nguchiro watakuja na kutetea .... ...
 
Hii kali kuliko,

Sasa wana JF hizi taarifa ni nzito sana yaani siamini na macho yangu huku USA watu kama hao Serikali ingechukua hatua ya kuwafuta kazi mara moja bila kuchelewa na bila kujali eti huyu mtoto si wa chifu kiumbe au jalala sheria ni msumeno. Kwakweli chikawe anasubiri nini badala ya kumpa boss wake JK kufanya maamuzi ya haraka kuliokoa shirika. Nafikiri Erio amepenyeza rupia kwa Chikawe, Hosea, Usalama wa Taifa lakini kwa sasa Erio habebeki kwa mpeleko ya aina yeyote kwani asubiri kilichowakuta wanene waliotangulia wengi waliokosa maadili. Mimi yangu macho kilio cha wengi kina madhara makubwa wabadhilifu, utemi, uwizi, uzinzi, na ufisadi.
 
Mwanakijiji ajuacho ni ufataani tu, kunamengi kachakachuwa na kutia yake na zionekane ni habari za kweli. Uongo mtupu.

Ili uonekane japo una hekima kati ya werevu, unahitaji kuonesha japo kidogo tu ni kipi kimechakachuliwa. Vinginevyo, unaweza kujidhania umesema hekima.
 
Mwanakijiji ajuacho ni ufataani tu, kunamengi kachakachuwa na kutia yake na zionekane ni habari za kweli. Uongo mtupu.

Walewale wenye agenda zao. Unahusika na hili bila shaka! Na miaka hii mtateseka sana. Imefikia pahala Wadanganyika watasema hapana. Kilichobakia ni ninyi kutubu na kurudisha mali za watu. Hakika kila jiwe litapinduliwa na yale yaliyouchagoni yatajulikana tu!
 
Nilikuwa mfanya kazi wa shirika la umma kwa kipindi cha miaka 16 hivi, lakini niliondoka na kuanza shughuli zangu mwenyewe. Kipindi hicho nilikuwa nakatwa michango ya PPF kutoka kwenye mshahara wangu kila mwezi, lakini baada ya kuondoka sikurudishiwa michango yangu hiyo eti kwa vile wanadai niliacha kazi kwa hiari yangu mwenyewe, hivyo sikuwa na haki na hela zangu zilizokatwa kama michango ya PPF; uonevu gani huo jamani, ile ilikuwa nji hela yangu! To the best wangenirudishia hela yangu halisi hata bila interest wakabaki na ile contribution ya mwajiri wangu. Kumbe hivyo ndivyo wanavyotumia pesa zetu?
 
Hii kali kuliko,

Sasa wana JF hizi taarifa ni nzito sana yaani siamini na macho yangu huku USA watu kama hao Serikali ingechukua hatua ya kuwafuta kazi mara moja bila kuchelewa na bila kujali eti huyu mtoto si wa chifu kiumbe au jalala sheria ni msumeno. Kwakweli chikawe anasubiri nini badala ya kumpa boss wake JK kufanya maamuzi ya haraka kuliokoa shirika. Nafikiri Erio amepenyeza rupia kwa Chikawe, Hosea, Usalama wa Taifa lakini kwa sasa Erio habebeki kwa mpeleko ya aina yeyote kwani asubiri kilichowakuta wanene waliotangulia wengi waliokosa maadili. Mimi yangu macho kilio cha wengi kina madhara makubwa wabadhilifu, utemi, uwizi, uzinzi, na ufisadi.

Hivi huyu Chikawe si ndo naye kakumbwa na dhahama ile ya kuzuwiwa akielekea na ndege yake kuelekea kule kwa Babu loliondo!
 
Mbona hata chenyewe hatujakiweka...? Halafu wapo wanaosema ati niko Usalama wa Taifa! I hate them with a passion aisee!

Na hata ungekuwa Usalama wa nini umeonyesha kukerwa na upuuzi huu. Mzalendo wa kweli hawezi kukaa na kamsitu ka watu wanaokula damu na nyama za watu! Ukomavu wa kweli ni kuweka hadharani yale yanayoizunguka jamii yako. Kuna kipindi huwa namfikiria huyu IGP wa sasa ingawa kafungwa mdomo. Wakati fulani kidogo tu na yeye aropoke! wakati ule alienda mbali aliposema kuna majina ya watu wengine ukiyatamka hadharani nchi haitakalika! angebanwa kidogo tu angesema kweli! Jicho la mtu mmoja lilikuwa kali sana naye akasita kutamka. Akiwa kama mzalendo ana wajibu wa kumsema lakini akaogopa. Sasa naye anashiriki kula nyama za watu. Damu na nyama hizi zitawaangamiza. Sijui kwa nini watu hawasomi alama za nyakati na kugundua kuwa sasa watu wameamka na wala hawajafumba macho tena! Mwisho wa mwanzo unakaribia ndugu zangu! Kama sio leo ni kesho asubuhi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom