Malipo ya madeni kwa wanafunzi na nyongeza ya mishahara kwa wafanyakazi kipindi hiki ni rushwa ya CCM kwenu, msidanganyike

mcoloo

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
921
1,000
Ndugu Wana bodi kitendo Cha serikali ya CCM kuanza kulipa madeni ya wafanyakazi na kuwapandisha madaraja inadhihirisha wazi kuwa huu Ni ukiukwaji wa maadili na kanuni za uchaguzi mkuu.

Nawakumbusha wafanyakazi wote kuwa hizi ni dharau kubwa Sana kwa miaka mitano mmesoteshwa halafu leo anajifanya kutambua umuhimu wenu eti kwa sababu tu anataka kura zenu,. Ukweli Ni kwamba Mara tu baada ya uchaguzi ,mkisha mpatia kazi hata wakumbuka kabisa.

Ebu muwakumbuke wenzenu mliofanya nao kazi na wamestaafu bila ya kuongezwa mshahara wameathirika kwa kiwango gani.

Huu si muda Tena wa wafanyakazi wa nchi hii kugeuzwa Kama karai linalo tumika kubebea zege kipindi Cha ujenzi Mara tu ujenzi unapokuwa umemalizika hutupwa na kusahaulika, nalitakuja kumbukwa kipindi ujenzi mwingine unapoanza, hapo Lita safishwa na kuonekana la thamani.

Huu Ni upuuzi kwa wafanyakazi na dharau isio pimika. 28/10/2020 kila mwananchi wa nchi hii anatakuwa na Jambo lake nalo si kingine isipokuwa iwe Ni kuikataa CCM kwenye sanduku la kura.
Iwe Ni siku ya ukombozi kwa Tanzania mpya.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
12,813
2,000
Very true mkuu, kama aliweza kuwanyima stahiki zao kwa miaka mitano ya uongozi wake atashindwa nini kuwanyima tena stahiki zenu kwa miaka mingine mitano??? Tena akijua haitaji tena kura zenu as anamaliza muda wake... ndio kabisaa hatajishughulisha...poleni watanzania kama hamuoni kiongozi wenu ni bomu
 
MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,639
2,000
Magufuli achia FAO la kujitoa

Watu walipwe Pesa zao zote

33% ya mshahara... kwani mtu analipa Kodi ya Nyumba Nusu, au Sukari ananunua Nusu Bei?
 
Mhadzabe

JF-Expert Member
May 20, 2009
2,931
2,000
Serikali lazima iendelee na kazi zake nyakati zote iwe wakati wa kampeni ama wa kutekeleza ilani ya chama kilichopo madarakani.

Hakuna muda ambao KATIBA inasema serikali isifanye kazi zake!...maana kufanya hivyo kuruhusu uvunjaji wa amani.

Kuhusu serikali kuwapa stahili zao watumishi wa umma ni jambo jema sana na la kupongezwa.

Swala libaki kwa mpiga kura mwenyewe natambua hayo yafanywayo na serikali ni HAKI yake na si fadhila au rushwa!

Waingie na mentality hii ndani ya chumba cha kupiga kura!
 
Bia yetu

JF-Expert Member
Apr 14, 2020
6,936
2,000
Nyie chadema mtaongea kila lugha chafu mwaka huu ila October kichapo kipo pale pale

Mkipata hata wabunge wawili mkatambike
Very true mkuu, kama aliweza kuwanyima stahiki zao kwa miaka mitano ya uongozi wake atashindwa nini kuwanyima tena stahiki zenu kwa miaka mingine mitano??? Tena akijua haitaji tena kura zenu as anamaliza muda wake... ndio kabisaa hatajishughulisha...poleni watanzania kama hamuoni kiongozi wenu ni bomu
 
Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
12,813
2,000
Nyie chadema mtaongea kila lugha chafu mwaka huu ila October kichapo kipo pale pale

Mkipata hata wabunge wawili mkatambike

Sababu ya kupandisha mishahara kipindi hki cha uchaguzi ni nini?? Think, lady think!
 
Ben Bella

JF-Expert Member
Dec 3, 2019
510
1,000
Mimi ni mtumishi wa umma. Sitakubali kurubuniwa kifala hata siku moja.
Huyu si alijifanya mwamba kwa yale madaraja yake aliyojenga. Sasa maji yamefika shingoni anaanza kuturubuni.

Mwambieni haturubuniki ng'o! 28 October Pombe must go.
 
Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
12,813
2,000
Unawaonea wivu wafanyakazi wazalendo wa Tanzania ?
Mwambieni na Mbowe awapandishe hapo ufipa

Eti wazalendo!?! Muulize jiwe yeye ni mtumishi wa umma aka mzalendo na amekuwa hivyo kwa miaka mingi, je ni haki alichofanyia ‘wazalendo’ wenzie kwa miaka mitano?, Kisha kuwalipa wakati huu wa uchaguzi sio dhihaka ?
 
jiwe angavu

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
2,778
2,000
Very true mkuu, kama aliweza kuwanyima stahiki zao kwa miaka mitano ya uongozi wake atashindwa nini kuwanyima tena stahiki zenu kwa miaka mingine mitano??? Tena akijua haitaji tena kura zenu as anamaliza muda wake... ndio kabisaa hatajishughulisha...poleni watanzania kama hamuoni kiongozi wenu ni bomu
Nani anamaliza muda wake..?kama aligoma kubadili katiba jiandae kwa mabadiliko ya katiba muhula ujao..we unadhani kwa nini wanalazimisha mbogamboga wazee wa ndio mzee wajazane bungeni..we subiri hutaamini kinachokuja.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
White party

JF-Expert Member
May 5, 2015
826
1,000
Mimi sijaongezwa bado na hata akiongeza tarehe23 SITAMCHAGUA!kwa kuwa kanichelewesha sana na kwa tabia hii nina hakika itakua ndo nyongeza ya mwisho na pengine akipita atakata kama alivyofanya madaraja ya 2017 kwa kisingizio cha uhakiki mwingine
##WATUMISHI TUSIDANGANYIKE##
 
Bia yetu

JF-Expert Member
Apr 14, 2020
6,936
2,000
Watu kila mwaka wanalipwa ! Usifananishe mambo ya ufipa na serkali makini ya Rais Magufuli
Eti wazalendo!?! Muulize jiwe yeye ni mtumishi wa umma aka mzalendo na amekuwa hivyo kwa miaka mingi, je ni haki alichofanyia ‘wazalendo’ wenzie kwa miaka mitano?, Kisha kuwalipa wakati huu wa uchaguzi sio dhihaka ?
 
Nazgur

JF-Expert Member
Apr 19, 2020
2,750
2,000
Ndugu Wana bodi kitendo Cha serikali ya CCM kuanza kulipa madeni ya wafanyakazi na kuwapandisha madaraja inadhihirisha wazi kuwa huu Ni ukiukwaji wa maadili na kanuni za uchaguzi mkuu.

Nawakumbusha wafanyakazi wote kuwa hizi ni dharau kubwa Sana kwa miaka mitano mmesoteshwa halafu leo anajifanya kutambua umuhimu wenu eti kwa sababu tu anataka kura zenu,. Ukweli Ni kwamba Mara tu baada ya uchaguzi ,mkisha mpatia kazi hata wakumbuka kabisa.

Ebu muwakumbuke wenzenu mliofanya nao kazi na wamestaafu bila ya kuongezwa mshahara wameathirika kwa kiwango gani.

Huu si muda Tena wa wafanyakazi wa nchi hii kugeuzwa Kama karai linalo tumika kubebea zege kipindi Cha ujenzi Mara tu ujenzi unapokuwa umemalizika hutupwa na kusahaulika, nalitakuja kumbukwa kipindi ujenzi mwingine unapoanza, hapo Lita safishwa na kuonekana la thamani.

Huu Ni upuuzi kwa wafanyakazi na dharau isio pimika. 28/10/2020 kila mwananchi wa nchi hii anatakuwa na Jambo lake nalo si kingine isipokuwa iwe Ni kuikataa CCM kwenye sanduku la kura.
Iwe Ni siku ya ukombozi kwa Tanzania mpya.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Kwa hiyo unataka shughuli za serikari zisimame kwa akiri ya siasa?
Basi wekeni sheria hata kulipa mishahara na huduma ya majina afya zisimame wakati wa kampeni ili usikie raha.
Jambo hili lilitamkwa mapema hata kabla ya kampeni kuwa litafanyika na watalipwa madeni na kupanda madaraja kabla ya mwaka huu kuisha sasa wewe ulitaka wafanye lini?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom